Mkurugenzi
mkuu wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul Maganga (Kulia)
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu tamasha
maalum la siku ya Wachaga lililodhaminiwa na Pepsi, litakalofanyika
siku ya Jumamosi Julai 28,Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ambapo
pia litasindikizwa na bendi za Msondo Ngoma, Twanga Pepeta na vikundi
vingine vya ngoma ya asili, (Kushoto) Ni Fredrick Mtaki, Ofisa Mahusiano
wa kampuni hiyo.
********************************************
BENDI
Kongwe na zenye ushindani mkubwa nchi za Twanga Pepeta na Msondo Ngoma
zinatarajiwa kupiga shoo ya aina yake kwenye tamasha la siku ya
Wachaga, (Chagga Day 2012), Julai 28, viwanja vya Leaders.
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema leo ukumbi wa Idara ya habari Maelezo,
jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul
Maganga, walioandaa tamasha hilo lililoadhaminiwa na kampuni ya SBC
Tanzania Limited, kinywaji cha Pepsi, alisema siku hiyo itakua ya aina
yake kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza kufurahia kwa
pamoja tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine
yatakayoshiriki tamasha hilo.
“Siku
hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya utamaduni wa kabila
hilo la Chaga, na makabila mengine na burudani kutoka kwa bendi hizo za
Twanga na Msondo, pamoja na vikundi vingine vya ngoma ya asili ”
alisema Maganga
Pia
alisema kua, kutakua na wazee wa mila ambo watazungumzia asili la
kabila la wachaga huku vyakula na vinywaji vya asili kutoka mkoa wa
Kilimanjaro, Kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo,
ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.
Aidha,
Siboka alisema baada ya Tamasha la hilo la ‘Chaga day’, litafuatia
tamasha lingine litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo
litapambwa na sherehe mbalimbali
Aidha,
Maganga alisema kua, wataendelea kufanya matamasha haya kwa karibu
makabila yote yaliyopo hapa nchini ilikuwezesha jamii kutambua mila zao
sambamba na kudumisha utamaduni wa Mtanzania kwa kuwakumbusha tamaduni
zao hii pia itakua ikijenga na kudumisha mahusiano baina ya makabila
mbalimbali nchini Tanzania.
Pia
anasema kua, watazania watakao hudhuria tamasha hilo, watapata kujua
chimbuko la kuweko kwa tamaduni zao yaani mashujaa wa makabila yao,
viongozi na machifu waliotawala jamii zao.
Maganga
pia aliwataja wadhamini wakuu wa tamasha hilo kua ni pamoja naTBL
kupitia bia za Safari na Kilimanjaro, SBC Tanzania (Pepsi),
Dstv,Homeshopping Centre,Canocity,Kishen Enterprises, Zizou Fashion, CXC
Africa,Giraffe Hotel,BM barber shop,Mlonge Bi Makai, Chili Chili
Restaurant, Auckland Safaris &Tours, Clouds Fm, and Alleys Travel
&Tours, Dotnata Decorations.
No comments:
Post a Comment