Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 22, 2012

Airtel donates text books to Mpita Secondary School-Singida.


Airtel yatoa msaada wa vitabu shule ya secondary Mtipa wilaya ya Singida Mjini - Singida Dar Es Salaam, Jumapili - Julai 22nd 2012, Airtel Tanzania kampuni ya simu za mkononi yenye kutoa huduma bora nchini kote, leo imetoa msaada wa vitabu katika shule ya sekondari Mpita ikiwa ni sehumu ya shughuli zao za kusaidia jamii.
 
Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za Airtel mjini Dar Es Salam kwa ajili ya shule ya sekondari ya Mtipa wilaya ya Singida mjini. Mwawakilishi wa shule hiyo ambaye ni mzawa wa eneo hilo  bi Mary Hiki alikabidhiwa msaada huo wa vitabu na Meneja wa huduma kwa  Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayuni.  Shule imepewa msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilling milioni mbili. Vitabu vilivyotolewa ni pamoja na Hisabati, Phisikia, Biolojia, Kiswahili. ambapo vimekuwa na uhitaji mkubwa shuleni hapo.
 
Akiongea wakati wa makabithiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za Airtel mjini Dar Es Salaam  Meneja Huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayuni alisema"  Airtel kwa kupitia kampeni yake ya kusaidia jamii imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule nyingi nchini Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya shule ya sekondari wilayani Singida na kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa shule hii Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwanitunatambua elimu ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya kesho. Aliongeza Bayuni.
 
Mwakilishi wa Shule hiyo bi Mary Hiki mzawa wa Singida alisema tunayo fuhara kuona Airtel inajito katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu nchini, moja kati mikakati ya elimu halmashauri yetu iliyojiwekea ni kuhakikisha kwamba kila nyumba moja ya mkazi wa Singida anatoka
graduate na ili kufikia malengo yake kuna mahitaji makubwa ya vitabu vya kufindishia, tunashukuru sana Airtel kwa kutusaidia katika kutimiza malengo tuliojiwekea.
 
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, mwezi uliopita Airtel ilitoa msaada wa kutoa computer 4  na Vitabu vyenye dhamani ya millioni tano kwa shule ya sekondari Mazombe iliyokokilomita nne kutika Iringa mjini
Hii ikiwa nikatika kurudisha faida inayoipata na kuchangia katika huduma kwa jamii

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...