Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)
Press Release
Mabondia Alpjonce Joseph
(Mchumiatumbo) na David Michael Mlope (Zola D – King) watapambana katika
Tamasha la Watani wa jadi litakalofanyika katika Sikukuu ya Idd El
Fitri kwenye Uwanja wa Chuo cha Bandari Temeke.
Pambano hilo
ambalo limeandaliwa na SHIWATA ili kukusanya fedha za Ujenzi wa nyumba
za kisasa za gharama nafuu kwa ajili ya Wasanii, Waandishi wa Habari na
Wanamichezo katika Kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.
Kamisheni ya Ngumi za kulipwa nchini Tanzania (TPBC) ambalo inasimamia pambano hilo la Mabondia hawa watakaocheza katika uzani wa juu (Heavy weight) raundi nane (8) pia kutakuwa na pambano moja la utangulizi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Viwango vya mabondia wa kulipwa wa TPBC, Boniface Wambura amethibitisha kuwepo kwa pambano hilo wakati wa Sikukuu za Iddi el fitri, Agosti, 2012.
Mwenyekiti wa SHIWATA
Cassim Taalib alisema pamoja na pambano hilo, kutakuwa na mechi ya mpira
wa miguu kati ya Simba na Yanga (Veteran) katika Uwanja huo huo wa Chuo
cha Bandari Temeke na mshindi wa mchezo huo atazawadiwa ng’ombe dume.
Taalib alisema kwamba
kikundi cha Mchiriku cha Jagwa kitatumbuiza, Roman Mg’ande wa Msondo
atapigana mieleka na Lumole Matovolwa (Big na upande wa wanawake Sophia
Lubuva wa Simba atapambana na Mwajuma Jimama wa Yanga huku washangiliaji
wa Mpira Pesa (Simba) watapambana katika mpira wa miguu na Watani wao wa jadi Yanga Bomba.
Tamasha litapambwa na mechi
ya Mpira wa Kikapu ya Ngongoti pamoja na mashindano ya Pikipiki ambayo
yanatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa watoto na wakubwa ambao siku hiyo
watakuwa wakisherekea Sikukuu ya Idd el fitri baada ya kumalizika kwa
mwezi wa Ramadhani, Wasanii wa Bongo Flava nao watakuwepo.
Peter Mwenda
0786/0752/0715 – 222677
Ofisa Habari wa SHIWATA
No comments:
Post a Comment