Waandishi wa habari waliofika kuhudhuria uzinduzi wa ‘Elimu yao, Wajibu wetu” kampeni iliyoandaliwa na mabalozi waliojitolea kwa hiari kuhakikisha fedha hizo zinapatikana. Kiasi chote kitakachopatikana katika kampeni hiyo kitaingizwa katika mradi huu.
Kikundi cha wasichana
maarufu watano katika nyanja mbalimbali nchini wameungana kwa pamoja na kuamua
kwa hiari kuunga mkono jitihada za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) za kutafuta
kiasi cha shilingi za kitanzania billion 2.3 zitakazotumika kujenga hosteli 30
ambazo zitahudumia wasichana wa shule za sekondari 1,504.
Kikundi hicho cha mabalozi
wa kampeni hii kinaundwa na Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA) Faraja
Nyalandu (Miss Tanzania 2004), Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Jokate
Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na Mariam Ndaba(Mwana mitindo na
mmiliki wa blog) kiliguswa kwa namna ya kipekee na na jitihada za TEA na hivyo
wakaamua kwa hiari kuungana na TEA katika kuhamasisha watu kujitokeza na
kuchangia kampeni hii.
Mabalozi hawa wameiita
kampeni yao “Elimu Yao. Wajibu wetu” maana ya usemi huu ni kwa kila mtanzania ana
wajibu wa kuhakikisha mtoto wa kike anapewa haki yake ya kuwa na elimu bora. Haki
hii ya elimu inajumuisha mazingira mazuri ya kusomea. Hivyo huu ni wito kwa
watanzania, wafanyabiashara, wafanyakazi, wanawake watanzania waliofanikiwa na watanzania
wa ughaibuni kujitokeza kwa wingi na kuhusika moja kwa moja na jitihada hizi.
Changamoto ambazo mtoto wa
kike anakumbana nazo hususani anayetokea nyumbani kwenda shule ni pamoja na
kukosa muda wa kujisomea kutokana na kazi za nyumbani ambazo zinapelekea kuathiri
maendeleo ya elimu kwa mtoto wa kike, mimba na ndoa za utotoni ni kati ya
changamoto kubwa zinazowakumba wale waliopanga karibu na maeneo ya shule,
kutokana na hayo, Mabalozi hawa wameamua kujitolea kwa kuweka mpango mkakati
utakaosaidia ujenzi wa hosteli tano na kuendelea kati ya hizo 30 ambao TEA
imepanga kujenga.
Mpango mkakati huo ni pamoja
na kufanya kampeni katika vyomba mbalimbali vya habari nchini na kuandaa mbio za hisani ambapo hela zitakazopatikana
zitapelekwa katika mradi huo. Mabalozi hawa wanaamini kuwa tofali moja kutoka
kwa kila mtanzania linaweza kuleta mabadiliko “changia Tofali”. Unaweza kuchangia kwa kutuma neno "Changia
Tofali"kwenda namba 15564, na utakuwa umechangia Tshs 250/-. Changia mara
nyingi uwezavyo.
No comments:
Post a Comment