MISS UTALII TANZANIA WAJIIMARISHA KANDA YA KASKAZINI, WAKURUGENZI WA KANDA NA MIKOA WATEULIWA
Bodi
ya taifa ya Miss tourism Tanzania Organisation , imefanya na
kuthibitisha uteuzi wa wakurugenzi wa kanda na mikoa ya kanda ya
Kaskazini, ambao pia watakuwa na jukumu la kusimamia na kuandaa
mashimdano ya Miss Utalii Tanzania , katika ngazi za mikoa ya
Arusha,Manyara , Kilimanjaro na kanda ya Kaskazini. Bodi ilipokea zaidi
ya maombi 12 kutoka kwa watu binafsi na makampuni mbalimbali, ambao
waliomba ukurugenzi na uandaaji wa mashindano ya
Miss
Utalii Arusha, Manyara na Kilimanjaro, ambopo waliofanikiwa kupitishwa
na kuteuliwa ni Mr. Job lay Mr. Zephaniah Tumbo wa NAMAN 2010 LTD (
Arusha na Kanda ya Kaskazini) Mosses Method Komba wa NEW VISION PLAN
COMPANY LTD (Manyara) na Kilimajaro).
Bodi
imezingatia vigezo vyote vya kanuni na taratibu za mashindano ya Miss
Utalii Tanzania,katika kufanya uteuzi huo, ikiwemo kigezo cha kuwa na
ofisi ya kudumu katika mkoa au kanda husika, kigezo kingine ni
waombaji
kuwasulisha mpango mkakati wa kuimarisha na kukuza mashindano,Utalii na
utamaduni katika mkoa au kanda husika kupitia mashindano haya.
Bodi
inaendelea na mchakato wa kupitia na kupokea maombi mapya na ya zamani
ya kuandaa na kusimamia mashimdano ya Miss Utalii Tanzania , katika
mikoa yote na kanda zote za Kusini, Kusini Nyanda za Juu,Mashariki,
Kati, Zanzibar, Ziwa, Magharibi na kanda za Vyuo Vikuu. Mikoa ambayo
maombi yanakaribishwa ni pamoja na mikoa ya RUVUMA, RUKWA, NJOMBE,
KIGOMA, SHINYANGA, SHIMIYU, GEITA, TANGA, PWANI, SINGIDA, MTWARA,
MWANZA, DODOMA, ZANZIBAR, MOROGORO NA TABORA. Kanda ambazo maombi
yanakaribishwa ni pamoja na KANDA ZA KUSINI, KUSINI NYANDA ZA JUU,
MASHARIKI, KATI, MAGHARIBI, ZIWA. Upande wa vyuo Vikuu maombi yanayo
pokelewa ni ya kanda za MISS UTALII TANZANIA VYUO VIKUU KUSINI,
KASKAZINI, MASHARIKI, MAGHARIBI, KATI, KUSINI NYANDA ZA JUU NA ZIWA
Mwisho
wa kupokea maombi ni tarehe 30-7-2012. Wakati huo huo kamati ya Taifa
ya uratibu na ufundi ya mashindano ya Miss Utalii Tanzania , imetangaza
kalenda mpya ya mashindano ya ngazi zote za Wilaya hadi taifa, kwa
kuzingatia kalenda na utaratibu mpya wa fainali za Taifa za Miss Utalii
Tanzania kila mwaka kuwa zinafanyika,9-12-2012 sambamba na sherehe za
uhuru wa Tanzania kuanzia mwaka huu.
Kalenda
ya fainali za Wilaya na Mikoa yote sasa itakuwa imekamilisha mashindano
ya ngazi zao hadi kufikia Oktoba 2012 na Kanda zote zutakuwa
zimekamilisha fainali za kanda zote kufikia Novemba 12 ,2012.
Miss Tourism The Symbol Of National Heritage
Maombi yote yatumwe kupitia: missutaliitanzania@gmail.com
No comments:
Post a Comment