Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
mkewe Mama Asha Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mwilongo na Makamu
Mwenyekiti wa Chuo cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African
Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, kwa pamoja
wakifurahia mtandao wa mawasiliano kwa njia ya Video unaowawezesha
wanafunzi kuonana na kuzungumza na kuchangia masomo kutoka sehemu
tofauti ndani na nje ya mkoa huo wa
Arusha, wakati Makamu alipofika chuoni hapo leo, kutembelea na kukagua
chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni.
Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo
hicho.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Chuo kipya cha Nelson Mandela
‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof.
Burton Mwamila, wakati leo akitembelea mazingira ya Chuo hicho
kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni kilichopo Jijini
Arusha. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa
Chuo hicho.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha Nelson
Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’,
Prof. Burton Mwamila, wakati akimfafanulia kuhusu kazi za maabala mpya
inayoandaliwa katika Chuo hicho wakati Makamu alipofika chuoni hapo leo,
kutembelea na kukagua chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili
wanafunzi hivi karibuni. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya
Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho. Kushoto kwake ni mkewe Mama Asha
Bilal.
No comments:
Post a Comment