Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 22, 2012

VAN PERSIE ATAKA PAUNI MILIONI 10 KWA MWAKA


Robin van Persie
LONDON, England

Dau analotaka kama litakubaliwa na klabu yoyote litamfanya Van Persie kuwa mmoja wa wachezaji wanalolipwa kiasi kikubwa zaidi duniani.

MHOLANZI Robin van Persie atahitaji dau la pauni milioni 10 kwa mwaka kwa klabu itakayohitaji kumsajili kiangazi.

Wakala wa mshambuliaji na nahodha huyo wa Arsenal, Kees Vos alikuwa na kikao kifupi na mabingwa wa soka nchini Italia Juventus na kufichua kuwa nahodha huyo wa Washika Bunduki anahitaji mshahara wa pauni 195,000 kwa wiki.

Dau analotaka kama litakubaliwa na klabu yoyote litamfanya Van Persie kuwa mmoja wa wachezaji wanalolipwa kiasi kikubwa zaidi duniani.

Awali Juventus ilimtangaza RVP kama kipaumbele chao cha usajili wa majira ya joto, kabla ya sasa kuonekana kurudi nyuma katika jaribio hilo linalohitaji pesa kubwa, huku klabu hasimu za Manchester City na Manchester United zikiwa tayari kupata saini ya nyota huyo mwenye miaka 28.

Mchezaji Bora huyo mara mbili mfululizo, alishakataa kurefusha mkataba wake Emirates kwa mshahara wa pauni 130,000, lakini sio Man City wala Man United anayeweza kuiwa mgeni wa dau analohitaji nyota huyo kwa sasa.

Man City inamlipa Yaya Toure mshahara wa pauni 225,000 kwa wiki, huku Wayne Rooney akiigharimu Man United kiasi cha pauni 200,000 kwa wiki pia.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amemuacha RVP katika ziara ya kikosi chake kujiandaa na msimu mpya huko Mashariki ya Mbali na kuna fununu kwamba Lukas Podolski anatarajiwa kukabidhiwa rasmi jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na Van Persie.

Na Wenger ambaye tayari keshawasajili washambuliaji wawili, Podolski na Olivier Giroud, huku akimfukuzia Fernando Llorente, amekiri kuwa RVP ni muhimu: “Van Persie ni mmoja wa washambuliaji bora duniani.”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...