Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 22, 2012

SIMBA YATOKA DROO YA 1-1 NA AS VITA KOMBE LA KAGAME SASA KUKIPIGA NA AZAM



 Kiungo mshambuliaji wa Simba, Amri Kiemba (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa As Vita, Mfongang Alfred, wakati wa mchezo huo.Timu ya AS Vita, inazaminiwa na Kampuni ya Tigo nchini mwao kama anavyonekana akiwa amevaa jezi yenye nembo ya wadhamini wao katika Soka
 Juma Nyoso wa Simba (kushoto) akimchezea rafu mcheaji wa As Vita, Etekiama Taddy, wakati wa mchezo huo leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa.
 Mshambuliaji wa As Vita, Magola Mapanda (kulia) akiwania mpira na beki wa Simba, Juma Nyoso, wakati wa mchezo huo.
Kipa wa Simba, Juma Kaseja, akichungulia mpira uliopigwa kwa mkwaju wa penati na Etekiama Taddy na kuandika bao katika dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza. Simba wamekosa penati katika dakika za majeruhi baada ya Sunzu kupiga fyongo na kuokolewa na kipa wa AS Vita na kufanya matokeo kuwa 1-1.

YANGA KUCHEZA NA MAFUNZO, SIMBA NA AZAM
WAKATI huo huo tayari Shirikisho la mpira wa miguu Tff, limekwishatoa maamuzi kwa kurusha shilingi na kumpata mshindi wa kwanza na wa pili katika kundi B, ambapo Yanga sasa itacheza na Mafunzo siku ya jumatatu na Azam kuchea na Simba na As Vita watacheza na Atletico.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...