Irene Isaka, Mkurugenzi wa SSRATAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUSITISHWA KWA FAO LA KUJITOA |
Mamlaka
ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), inapenda
kutoa ufafanuzi juu ya mafao ya kujitoa. Ufanunuzi huu unakwenda
sambamba na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na vyombo vya
habari na kuleta mkanganyiko miongoni mwa Wanachama na Wadau wa Sekta ya
Hifadhi ya Jamii.
Kufuatia hali hiyo, Mamlaka inatoa ufafanuzi ufuatao:
- Marekebisho
kuhusu kusitisha fao la kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na
madhumuni ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama
anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu hali ya maisha
uzeeni.
- Ni
kweli kuwa Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya
Mamlaka zimefanyiwa marekebisho. Mchakato wa marekebisho hayo ulihusisha
wadau kwa kuzingatia utatu yaani wawakilishi kutoka Vyama vya
Wafanyakazi, Chama cha waajiri pamoja na Serikali.
- Kwa
kutambua tofauti ya ajira, tofauti ya mazingira ya kazi, tofauti ya
sababu za ukomo wa ajira, na umuhimu wa Mwanachama kunufaika na michango
yake wakati angali katika ajira, Mamlaka inaendelea na mchakato wa
kuandaa miongozo na kanuni za mafao ambazo lengo lake ni kuboresha
maslahi ya Wanachama. Miongozo na kanuni hizo zitajadiliwa na Wadau
wakiwemo Wafanyakazi, Waajiri na Serikali kabla ya kuanza kutumika.
- Kufuatia
kuanza kutumika kwa Sheria hiyo maombi mapya ya kujitoa yamesitishwa
kwa kipindi cha miezi sita hadi pale miongozo itakapotolewa ili
kuiwezesha Mamlaka na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutoa elimu kwa Wadau.
- Tangazo hili halitowahusu Wanachama waliojitoa kabla ya tarehe 20/07/2012.
- Mamlaka
inakanusha vikali kwamba, sitisho la fao la kujitoa si kwa sababu za
Kiserikali au kwa sababu mifuko imefilisika. Tunapenda kuwahakikishia
kwamba Mifuko yote ipo thabiti na michango yote ya Wanachama ipo salama.
- Hivyo,
Mamlaka inawaomba Wanachama na Wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
kuwa na utulivu wakati mchakato huu ukiendelea kwa lengo la kulinda na
kutetea maslahi ya Mwanachama.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji
SSRA-Makao Makuu
No comments:
Post a Comment