Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Regina Chongo (watatu kulia mrefu) akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukutana na makundi ya kijamii likiwemo kundi la kina mama wa wilaya hiyo ikiwa ni kwenye harakati zake za kuhimiza maendeleo Wilayani humo. |
Baadhi ya kinamama waliohudhuria mkutano huo wakiongoza na Mee Mashuhuri tangu wakati wa harakati za kudai Uhuru Binti Kanduru (Mwenye Fulana ya Njano) wakifuatilia Mkutano huo Mjini Nachingwea. |
OFISI ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea imeandaa maombi na kuyapeleka Serikalini kupanga mipango ya Kurudisha usafiri wa
Reli ambao ulikuwapo miaka ya nyuma katika wilaya hiyo ili kusaidia
Usafirishaji wa Mazao kama ilivyokuwa
awali ambapo tuta la Reli hiyo bado lipo.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rigina Chonjo wakati
akizungumza na wananchi wa Nachingwea ikiwa ni sehemu ya harakati zake
za kuhimiza maendeleo.
Kupitia
kauli mbiu yake ya Amani na Maendeleo amewahimiza wakazi wa Wilaya hiyo
kufanya kazi kwa juhudi ili kujiongezea kipato. Pamoja na kuwahimiza
wawekezaji kujitokeza kuwekeza kwenye Wilaya hiyo kuna fursa nyingi
ikiwemo madini ya aina mbalimbali.
Alihimiza
kila kijana mwenye uwezo wa kufanya kazi afanye kazi asikae bila ya
kazi hasa ukizingatia shughuli kuu za kiuchumi wilayani humo ni kilimo,
Kwa upande wa wazazi wao wamehimizwa kufuatilia na kusimamia elimu ya
watoto wao
Lakin wilaya yetu ya Nachingwea miundombinu yake hata suala la elimu kwa mazungumzo alisaidii,jambo la msingi ni vitendo,ukiangalia wilaya ya Nachingwea hakuna hata shule 1 ya form 5-6,na hakuna hata elimu kwa wananch,je tutafika?
ReplyDelete