Wapenzi
ambao walifanya mapenzi nje ya ndoa wamepigwa mawe hadi kufa mwishoni
mwa wiki na wapiganaji wa kiislam katika mji wa Aguelhok kaskazini mwa
Mali, maafisa wamesema.
Mwanamume na mwanamke huyo walizikwa mpaka kwenye shingo na kupigwa mawe hadi kufa.
Kaskazini mwa Mali nusu yake inaendeshwa na waasi wa Tuareg na wapiganaji wa Kiislam baada ya mapinduzi katika mji mkuu wa Mali.
Aguelhok katika eneo la Kidal alikuwa ni wa kwanza kukamatwa na waasi wa Tuareg .
Waislamu katika eneo la Aguelhok waliwapiga mawe mpaka kufa watu hao mbele ya watu 200 maafisa wamesema.
"Nilikuwepo.
Wapiganaji hao wa Kiislamuwaliwachukua watu hao katikati ya Aguelhok.
Watu hao waliwekwa kwenye mashimo mawili na wakapigwa mawe mpaka
wakafa." Afisa wa serikali eneo hilo alisema.
"Mwanamke alizimia mara baada tu ya mapigo," alisema, akiongeza kuwa mwanaume alipiga kelele mara moja tu na baadaye akanyamaza.
Uasi
wa Tuareg kaskazini ulichangia mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi na
kusababisha vurugu za makunbdi ya wapiganaji wa kiislam na kasha
kuchukua udhibiti wa miji kadhaa ya kaskazini.
Bw
Traore alisema ataongoza mazungumzo kuunda serikali ya umoja wa kitaifa
nchini Mali na kuongoza juhudi za kuanzisha mazungumzo na Waislamu.
"Wananchi
wa Mali hawana budi kuungana dhidi ya wavamizi,” alisema, akimaanisha
wapiganaji wa kigeni wa jihadi ambao wanatuhumiwa kudhibiti eneo la
kaskazini.
"Kutokana
na ugumu wa mgogoro huu na ukubwa wa mateso ya watu wa Kaskazini, kwa
pamoja, nasema pamoja, tunaweza kusafisha njia mbele yetu kuiweka huru
nchi yetu kutoka kwa wavamizi hawa, ambao wanaacha uharibifu na huzuni,
na kuwasababishia watu wetu maumivu, " alisema Bw Traore.
Kumekuwa
na shutuma kutoka jumuiya ya kimataifa kwa wapiganaji wa kiislam katika
mji wa zamani wa Timbuktu wakilaumiwa kwa kuharibu kumbukumbu za karne
nyingi za viongozi muhimu wa dini ya Kiislam ambao wanaheshimika kwa
Waislam wa madhehebu ya Sufi.
No comments:
Post a Comment