SAMSUNG YAZINDUA OFA YA MSIMU HUU WA SIKUKUU
“Ni Draw ya zawadi kubwa kwa wateja watakaonunua bidhaa za Samsung”
KAMPUNI ya SAMSUNG Tanzania leo imezindua rasmi ofa maalum ya kipindi hiki cha sikukuu ijulikanayo kama “Samsung Season’s Offer!”. Uzinduzi huu umefanyika katika duka la Samsung lililoko Quality Centre, Dar Es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania Bwana Kishor Kumar alisema, “Ofa hii inalenga kuwazawadia wateja wetu zawadi hizi katika msimu huu wa sikukuu. Ofa hii imeanza rasmi leo Ijumaa tarehe 30 Nov na itaisha Jumamosi tarehe 5 Januari 2013.”
Bwana Kishor alielezea zaidi kwamba wateja wote watakaonunua bidhaa za
Samsung zilizo katika ofa hii watapata zawadi za papo kwa hapo na pia
watapata nafasi ya kujishindia zawadi kubwa katika Draw ya mwisho. Draw
ya mwisho itashuhudiwa na wasimamizi kutoka bodi ya Taifa ya michezo ya
kubahatisha na itafanyika katika duka la Samsung Quality Centre Jumapili
tar 06 January mwakani.
Naye meneja usambazaji wa Samsung Mobile Tanzania Bwana Sylvester Manyara alisema kwamba, “Pamoja na bidhaa nyingine za Samsung, bidhaa zilizo katika ofa hii kabambe ni aina ya Galaxy Note 2, Samsung S3, Galaxy Note 10.1, Samsung S Duos, Samsung ACE Duos, Galaxy Pocket na Galaxy Pocket Duos.”
Bwana Manyara aliendelea kuelezea kwamba wateja watakaonunua bidhaa za
Samsung kipindi hiki watapata kuponi maalum ambazo watajaza na
kuzikusanya ili kujaribu bahati yao katika Draw kubwa ya mwisho. Ofa hii
inaendeshwa katika maduka ya Dar Es Salaam, na maduka ya Samsung
yaliyoko Mbeya, Arusha, Dodoma na Mwanza.
Bwana Kishor Kumar alimaliza kwa kutaja zawadi zitakazotolewa kwamba ni;
1. Zawadi ya Kwanza; Samsung LED TV ya Inchi 42’.
2. Zawadi ya Pili; Samsung Galaxy S3 Mobile Phone.
3. Zawadi ya Tatu; Samsung Galaxy Note 10.1.
4. Zawadi ya Nne; Samsung Home theatre.
5. Zawadi ya tano; Samsung Smart Camera.
Pamoja
na zawadi hizi, Samsung itatoa zawadi kwa wateja mbalimbali
watakaokutwa wakinunua bidhaa za Samsung, miongoni mwa zawadi hizi ni TV
tatu za inchi 32 zitakazotolewa moja kila wiki kwa wiki tatu mfululizo
kuanzia wiki hii.
Naye
bwana Manyara alimaliza kwa kuwashukuru wateja wa Samsung kwa kuchagua
bidhaa hizi bora, aliwaomba waendelee kufurahia bidhaa hizi hata baada
ya kipindi cha msimu huu wa sikukuu. Aliwakumbusha kwamba miongoni mwa
manufaa ya bidhaa za Samsung ni kwamba bidhaa zake ndio tu zina warantii ya miezi 24
yaani miaka miwili. Aliwakumbusha pia kupiga namba ya huduma kwa wateja
endapo wakihitaji ufafanuzi kuhusu jambo lolote kuhusu bidhaa za
Samsung. Namba ya huduma kwa wateja wa Samsung ni +255 685 88 99 00.
Samsung
inaendesha kampeni hii ikiwa ni wiki chache baada ya kufanya maonyesho
makubwa ya bidhaa zake jijini Dar Es Salaam yaliyofahamika kama “Samsung Week”.
Samsung inafanya pia shughuli nyingi za kujitolea, hususani msaada wa
udhamini wa mafunzo kuinua vipaji vya wanariadha katika shule ya Winning
Spirit Arusha, msaada kwa shule na matibabu katika kijiji cha Ilmorijo
Monduli Arusha na Lyamungu Moshi nk.