Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, September 30, 2015

MABONDIA THOMAS MASHALI NA FRANSIC CHEKA WASAINI KUZIDUNDA DESEMBA 25 JAMUHURI MOROGORO


Promota Kaike Silaju katikati akiwainuwa mikoni juu mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka wakionesha mikataba yao baada ya kusaini kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Fransic Cheka kushoto na Thomas Mashali wakisoma mkataba kabla ya kutia saini kwa ajili ya kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS
Wakili Paul Kalomo kutoka Mega Attorneys akiwafafanulia kifungu kwa kifungu mabondia Thomas Mashali wa pili kushoto na Fransic Cheka kulia kabla awajasaini
Promota Kaike Silaju katikati akipitia mkataba kabla ajawasainisha mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka ambapo wamekubaliana kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS
Wakili Paul Kalomo akiwaelekeza mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka jinsi ya kusaini mkataba wa pili kushoto ni promota Kaike Silaju  mabondia hawo watapigana desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

 Na Mwandishi Wetu
Mabondia Thomasi Mashali na Fransic Chaka Jana wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro

akisimamia utiaji saini huo
Wakili Paul Kalomo kutoka Kampuni ya  Mega Attorneys amesema mkataba huo ni rasmi kwa mabondia hawo watapambana siku hiyo kwenye mpambano wa raundi kumi kwa dakika tatu kila raundi na kupumzika kwa dakika moja mpambano utakuwa wa raundi kumi na mabondia watapimwa afya zao siku moja kabla ya mchezo ili kujiridhisha kuwa wako fiti

nae promota wa mpambano uho ambaye amekuwa akiandaa mapambano makubwa makubwa na yenye msisimko nchini amesema kuwa mpambano uho unasubiliwa na mashabiki lukuki na nimeamua kuweka katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro ili kuwapa fursa nyingine kwa wakazi wa morogoro kumwona Cheka ambaye kwa mda mrefu ajacheza

nae bondia Fransic Cheka amewaomba wapenzi na mashabiki wajitokezekwa wingi ili kuja kujionea kichapo atakachompa Mashali ambapo ndio kitamfanya ajutie kabisa kucheza mchezo wa ngumi

kwa upande wa Mashali amesema amefurai kupata nafasi nyingine ya kucheza na cheka kwani anataka kuonesha kiwango chake kilivyo kikubwa kwa sasa na yeye ni nambari wani katika ngumi nchini

katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo bondia Vicent Mbilinyi atapambana na Deo Njiku wakati Mohamed Matumla atakabiliana na Cosmas Cheka

Friday, September 11, 2015

NGUMI KUPIGWA CHANIKA SEPTEMBA 26


Na Mwandishi Wetu


BONDIA Said Mbelwa anatarajia kupanda uringoni kwa mara nyingine tena kungombania mkanda wa taifa wa chama cha ngumi za kulipwa PST dhidi ya bondia George Dimoso mpambano utakaofanyika Septemba 26 katika ukumbi wa Butihama Villa Club uliopo chanika mpambano huo wa raundi kumi ulioratibiwa na 

Kocha wa kimataifa nchini Rajabu Mhamila 'Super D' utakuwa ni wa kumaliza ubishi baada ya mpambano wa kwanza Dimoso kudundwa kwa point

Super D aliongeza kuwa siku iyo pia kutakuwa na mipambano mingine mikali itakayowakutanisha mabondia mbalimbali nchini ambapo 

bondia Seleman Zugo atapambana na Abdallah Ruwanje na Adam Ngange atakabiliana na Shabani Mtengela na Said Uwezo atapambana na Hassan Mgosi uku Hamza Mchanjo ataoneshana kazi na Ally Maiyo mipambano yote ya utangulizi ni ya raindi sita

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

NGUMI KUPIGWA CHANIKA SEPTEMBA 26

Rais Kikwete aagana na Wafanyakazi wa Mahakama ya Afrika

MGOMBEA MWENZA WA UKAWA JUMA DUNI HAJI AHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI IRINGA VIJIJINI

DAWASCO SACCOS YAZINDULIWA RASMI

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...