Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 24, 2015

ALLY BAKARI CHAMPION ACHUKUWA JIKO

Refarii wa mchezo wa masumbwi nchni kushoto akiwa na mke wake Aisha Chilumba  baada ya kuowa hivi karibuni maendeo ya Vingunguti Dar es salaam


Refarii wa mchezo wa masumbwi nchni kushoto akiwa na mke wake Aisha Chilumba  baada ya kuowa hivi karibuni maendeo ya Vingunguti Dar es salaam

BALOZI MISS KILIMANJARO KUTAFUTWA MWEZI UJAO KATIKA UKUMBI WA KILI HOME RESORT

Baadhi ya warembo watakawo wania taji la Kilimanjaro Ambassador litakalofanyika julay 24 katika ukumbi wa Kili Home Resort mkoa wa Moshi wakiwa katika pozi wakati wa utambulisho wa mashindano hayo
Baadhi ya warembo watakawo wania taji la Kilimanjaro Ambassador litakalofanyika julay 24 katika ukumbi wa Kili Home Resort mkoa wa Moshi wakiwa katika pozi wakati wa utambulisho wa mashindano hayo

Mlatibu wa mashindano ya urembo ya Kilimanjaro Ambassador Jacqueline Chuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchuano huo utakaofanyika katika ukumb wa Kili Home Resort

Tuesday, June 23, 2015

WASAMBAZAJI WA FILAMU KUGOMA KULIPA KODI IFIKAPO JULAY MOSI

Mwenyekiti wa chama cha wasambazaji wa Filam TAnzania 'TAFDA' Moses Mwanyilu kushoto akionesho moja ya filamu  kwa wahandishi wa habari katika ukumbi wa Idara Habari Maelezo Dar es salaa  awapo pichana juu ya filamu ambazo zinauzwa kiolela bila ya kulipa kodi tena kwa galam nafuu kulinganisha na zao ambao wanalipa kodi kupitia mamlaka ya Mapato TRA  ambapo julay mosi wameazimia kuto peleka filamu zao bodi ya filamu na kutonunua stemp kwa ajili ya ulipaji wa kodi wa pili kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa chama hico Suleiman Ling'ande
 
 Mjumbe wa chama cha usambazaji wa Filamu nchini Saleh Abdallah kushoto akizungumza na wahandishi wa habari awapo pichani juu ya filamu zilizojaa mtaani ambazo azijalipiwa kodi uku zikiachwa bila kuchukuliwa hatua yoyote ile wakati wao filamu zao zinakaguliwa na Bodi pamoja na kulipa kodi katika mamlaka ya mapato TRA kulia ni Mwenyekiti wa chama cha wasambazaji wa Filam TAnzania 'TAFDA' Moses Mwanyilu
 Mwenyekiti wa kikosi kazi kutoka chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania,Bw Moses Mwanyilu akionyesha baadhi ya filamu ambazo zinauzwa nchini bila kupata kibali kutoka bodi ya filamu Tanzania na kutokuwa na stika za ushuru za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakielezea changamoto zao kuhusiana na filamu za kitanzania kulazimishwa kukaguliwa na bodi ya filamu na kuwekwa stika za TRA ilhali filamu za nje hazifanyiwi hivyo na kupelekea filamu za kitanzania kutokuwa na ushindani sokoni.


Mwenyekiti wa kikosi kazi kutoka chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania,Bw Moses Mwanyilu akionyesha filamu kutoka nje ambayo inasemekana kuwa na maadili yasiofahaa kutazamwa na watoto chini ya miaka 18 ambayo inaendelea kuuzwa nchini huku ikiwa haijakaguliwa na bodi ya filamu wala haina stika za TRa kitu ambacho kimekuwa kikiwaumiza watayarishaji na wauzaji wa filamu za kitanzania ambazo zimekuwa na mlolongo mrefu hadi kuingia sokoni.


 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kuandika kile kinachozungumzwa 

Mjumbe wa chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania, Bw Saleh Abdallah akizungumzia kauli moja waliyokubaliana kama wasambazaji kuwa Kuanzia tarehe 1 Julai 2015 wao kama watayarishaji na wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania wamesitisha swala la kupeleka filamu zao bodi ya filamu kwaajili ya kukaguliwa wala kununua stika za TRA mpaka pale mamlaka husika zitakapokaa chini na kujadiliana kuhusu swala hili

Chama cha wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania leo wamekutana na waandishi wa habari kuelezea nia yao ya kusitisha kupeleka filamu zao bodi ya filamu Tanzania kwaajili ya kukaguliwa huku wakielezea sababu kuwa Bodi ya filamu imekua ikikagua filamu za Tanzania tu huku zile za nje zikiwa hazikaguliwi na kupelekea kuwaumiza wao katika soko la filamu 

Vilevile wamesitisha zoezi la kununua stika za TRA kutokana na sababu kuwa kazi nyingi za nje hazina stika na pia maafisa wa TRA wakipita kukagua filamu wanachukua za Tanzania tu ambazo hazina stika huku wakiziacha zile zinazotoka nje na zile zinaharamiwa huku sheria ya filamu ya mwaka 2012 ikisema kuwa filamu zote ziwe za nje au za ndani zinatakiwa kukaguliwa na kupewa daraja.

Kutokana na sababu ambazo chama cha wasambazaji wamezieleza kuwa Pamoja na kuwaandikia barua Mamalaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Filamu kuhusiana na swala hilo hawakuweza kupatiwa majibu ya barua yao na ndipo walipoamua kusitisha kununua stika na kupeleka filamu zao bodi kwaajili ya kukaguliwa mpaka watakapokaa meza moja huku wakiendelea kupeleka filamu sokoni.

Saturday, June 20, 2015

BONDIA WA MOROGORO AOMBA PAMBANO LA NGUMI KWA MAPROMOTA


Na Mwandishi Wetu 

PIUS KAZAULA
BONDIA Pius Kazaula wa Morogoro KG 66 amejitokeza hadharani na kuwaomba wadau wa mchezo wa masumbwi pamoja na mapromota kumwandalia mpambano kwa ajili ya kupima kiwango chake kwa kuwa mapromota wengi wapo Dar es salaam wao wa mikoani wanasahaulika

akizungumza na mwandishi wa habari kwa njia ya simu amesema mabondia wa uzito wake wapo wengi ingawa kila siku wanapangiwa wao kwa wao mana unaweza kukuta bondia mmoja kacheza na mtu mmoja mara nne wakati mabondia wengine tupo mokoani tunafanya mazoezi tu bili kujipima viwango vyetu

hivyo napenda kutoa wito kwa mapromota kujitokeza kutusapoti sisi mabondia wa mkoani ili nasi tujipime na mabondia mnao waamini

najiamini kuwa naweza kazi hivyo nami wasinikwepe kwa kuwa nawataka mabondia wao nasikia Bagamoyo Mkoa wa Pwani nao wanandaa ngumi mara kwa mara wajaribu kutuita na sisi si Dar peke yake mabondia wapo nchi nzima hivyo mapromota kama wana nia kweli ya kukuza mchezo na kuendeleza ngumi chini wawe wanachanganya mikoa mbalimbali 

bondia huyo mwenye makazi yake Morogoro akusita kumpongeza kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa sapoti anayotoa kwa mabondia mbalimbali na kuwapatia vifaa vya masumbwi  kwa galama nafuu na DVD zenye mbinu mbalimbali za mafunzo ya ngumi anazotoa kuelekeza mabondia chipkiz ambao wana kiu ya kuwa mabingwa wa Dunia kupitia mchezo wa masumbwi nchini

Airtel yazindua michuano ya ARS 2015


Mkurugenzi wa Idara Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na michezo Leonard Thadeo akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa  Airtel Rising Star msimu wa tano. Hafla ya uzinduzi ilifanyika jijini  Dar es Salaam leo 17th June,2015.

Mkurugenzi wa Idara Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na michezo Leonard Thadeo akiwa alama ya uzinduzi wa kampeni ya " Its Now" yenye kuwawezesha vijana  kutimiza ndoto zao katika Nyanjambalimbali kama technologia, michezo na muziki. Wakishuhudia ni Raisi wa TFF Jamali Malinzi( kushoto) Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Malya (kulia) akifatiwa na mwenyekiti wa soka la vijana Bwana Ayoub Nyenzi

XXXXXXXXXXXXX

DAR ES SALAAM
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua rasmi msimu wa tano wa mashindano ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ambayo yataanza kutimua vumbi Agosti 8 katika ngazi ya awali na kuhitimishwa kwa fainali za Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia
Septemba 11 - 21 mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano amesema kampuni ya Airtel Tanzania  ina nia thabiti ya kusaidia maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini na kujivunia mafanikio yaliyotokana na michuano hiyo kwa miaka minne iliyopita.

"Tunaona fahari kwamba michuano ya Airtel Rising Stars imeweza kuibua vipaji vya wachezaji ambao baadhi yao wamechaguliwa kujiunga na timu za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 20", alisema Singano.

Kumbukumbu za TFF zinaonyesha kwamba timu ya taifa ya wanawake imeundwa na wachezaji wengi kutoka Airtel Rising Stars ambayo madhumuni yake makubwa ni kuibua na kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17.

Singano pia ametangaza kampuni ya Airtel kuingia mkataba na nahodha wa Ivory Coast na kiungo wa Manchester City Yaya Toure katika kampeni mpya iitwayo  "It's Now" yenye lengo la kulea na kukuza vipaji barani Afrika kupitia Nyanja mbalimbali kama vile michezo, ikijumuisha mashindano ya Airtel Rising Stars kwa vijana chini ya umri wa miaka 17.

Sehemu nyingine ambazo kampeni hii itazigusa ni mtindo wa maisha na muziki, ambapo wateja watapata ufumbuzi wa masuala mbalimbali ya kiteknolojia ili kuona fursa zinazowazunguka.

Huu ni mwaka wa tano mfululizo kwa michuano ya Airtel Rising Stars kufanyika hapa nchini Tanzania ambayo huanzia ngazi ya chini hadi Taifa. Singano alilipongeza Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) pamoja na serikali kupitia Wizara ya Michezo kwa kuiunga mkono kwa dhati michuano ya Airtel Rising Stars tangu ilipoanzishwa nchini mwaka 2011.

Mkurugenzi wa Idara ya michezo katika wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema serikali inatambua mchango wa Airtel katika kuibua vipaji vya wanasoka chipukizi.

 "Inatuwia vigumu kuwekeza kikamilifu katika bmichezo kwa sababu ya kulemewa na majukumu mengine muhimu ya kijamii ndio maana tunahamasisha sekata binafsi kujitokeza kusaidia na Airtel wanafanya kazi nzuri" alisema Thadeo.

Mwaka huu michuano ya ARS itajumuisha mikoa ya Ilala, Kinondoni,Temeke Mbeya, Mwanza na Morogoro kwa upande wa wavulana na huku upande wa wasichana ukiwakilishwa na mikoa ya Ilala,Kinondoni, Temeke, Mbeya na Arusha.

Kwa upande wake, Rais wa TFF Jamal Malinzi aliipongeza Airtel Tanzania kwa kuwekeza kwenye soka la vijana. "Nawapongeza sana kampuni ya Airtel Tanzania kwa mpango wake huu wa kuwekeza kwenye soka la vijana ambao kwa kweli ndio msingi wa maendeleo wa mpira wa miguu hapa Tanzania na duniani kote", alisema.

Airtel ni kampuni ya simu za mkononi yenye matawi barani Afrika katika nchi za Burkina Fasso, Chad, Congo, Brazzaville, DRC, Gabon, Ghana, Kenye, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Rwanda, Selisheli, Sierra-Leone, Tanzania, Uganda na Zambia.

BENKI YA CRDB YAKABIDHI PASSO KWA MSHINDI WA SHINDANO LA 'Tuma Pesa na Simbanking Shinda Passo'


Mshindi wa Promosheni ya 'Tuma Pesa na Simbanking Shinda Passo' Mwinyi Khamis Juma mkazi wa Mbalali mkoani Mbeya, akipunga mkono baada ya kukabidhiwa zawadi yake katika hafla iliyofanyika mkoani Mbeya juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Mkoa wa Mbeya, Benson Mwakyusa na Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa. (Na Mpiga Picha Wetu) 
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (aliyeshika mfano wa ufunguo) akizungumza neno muda mfupi kabla ya makabidhiano wa zawadi ya Passo kwa mshindi wa Mkoa wa Mbeya, Mwinyi Khamis Juma. Kushoto ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Mwanjelwa, Ephraim Lwila na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Sumbawanga, Colnerius Msigwa (kulia) 
 Mshindi wa Shindano la "Tuma Pesa na Simbanking Shinda Passo" Mwinyi Khamis Juma mkazi wa Mbalali mkoani Mbeya, kiushukuru uongozi wa Benki ya CRDB baada ya kuibuka mshindi wa Promosheni ya Shindano la 'Tuma Pesa na Simbanking Shinda Passo' inayoendeshwa na benki ya CRDB. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Mwanjelwa, Ephraim Lwila. 

Friday, June 12, 2015

NGUMI ZA VUNJA JUNGU KUPIGWA BAGAMOYO JUMAPILI UKUMBI WA TASUBADVD ZA SUPER D BOXING COACH ZILIZOPO SOKONI
Na Mwandishi Wetu
 Bondia Shabani Kaoneka sasa atapanda ulingoni juni 14 jumapili hii kukabiliana na Cosmas Kibuga  uzito wa kg 72 baada ya mpinzani wake wa mwanzo Said Mbelwa kuingia mitini akizungumzia mpambano uho mwandaji Muhsin Shaliff amesema kuwa maandalizi ya mpambano uho yamekamilika kwa asilimia 98 kufikia 100

mbali na mpambano uho wenye upinzani mkali kutakuwa na michezo mingine itakayo wakutanisha Adam Ngange wa Chanika na Mfaume Mfaume wa Manzese mpambano wa kg 61 mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa TASUBA uliopo Bagamoyo mjini

siku hiyo pia kutakuwa na bondia Abdallah Pazi 'Mfalme wa wazalamu' atakaepambana na Mrisho Rajabu 'Dame' wakati bondia kutoka Kiwangwa Bagamoyo Iddi Pialali 'Simba aliyejeruiwa' atakumbana na Sweet Kalulu mpambano wa kg 63 raund sita

ngumi zingine zitawakutanisha Raymond Mbwago atapambana na Halidi Honga

siku hiyo pia kutapambwa nja burudani kutoka kwa Jumanne Iddi pamoja na Sam wa Ukweli watakaopamba jukwaa hilo kwa ajili ya burudani za muziki wa kizazi kipyaa 

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Monday, June 8, 2015

NGUMI KUFANYIKA TENA BAGAMOYO JUMAPILI JUNI 14


Na Mwandishi Wetu

MPAMBANO mkali wa masumbwi unatarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii juni 144 katika ukumbi wa TASUBA Bagamoyo mjini mpambano uho utakaowakutanisha mabondia Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo na Sweet Kalulu wa Dar es salaam

akizungumzia mpambano uho mratibu Muhsini Sharif amesema pambano hili litakuwa la raundi sita uzito wa kg 63 mbali na mpambano uho kutakuwa na mipambano mingine ya kumaliza ubisha kati ya Adam Ngange wa Chanika na Mfaume Mfaume kg 61 pamoja na Abdallah Pazi 'Mfalme wa wazalamu' na Mrisho Rajabu 'Dame' kg 74 wa kawe mpambano mwingine ni kati ya Raymond Mbwago na Halidi Hongo kg 63

aliongeza kwa kusema kuwa pia siku hiyo kutakuwa na burudani za nguvu kutoka kwa wasanii Sam Wa Ukweli na Jumanne Iddi ndio watakaotoa burudani kwa siku hiyo

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

MPAMBANO WA VICENT MBILINYI NA SAID MUNDI ULIVYOPIGWA UWANJA WA NDANI WA TAIFA


Bondia Said Mundi kulia akimtupia konde Vicent Mbilinyi wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliopita Mundi alishinda kwa point mpmbano uho wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Vicent Mbilinyi kushoto na Said Mundi wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika wishoni mwa wiki iliyopita katika uwanja wa ndani wa taifa Mundi alishinda kwa point  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Vicent Mbilinyi kushoto na Said Mundi wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika wishoni mwa wiki iliyopita katika uwanja wa ndani wa taifa Mundi alishinda kwa point  Picha na SUPER D BOXING NEWS

MBILINYI KUSHOTO NA MUNDI KULIA WAKISUBILI MATOKEO

Bondia Abdallah Pazi kushoto akipambana na Ibrahimu Tamba wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita  SUPER D BOXING NEWS

Friday, June 5, 2015

MABONDIA VICENT MBILINYI NA SAID MUNDI WA TANGA KUPIGANA KESHO UWANJA WA NDANI WA TAIFA
Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akitunishiana misuli na Said Mundi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpaqmbano wao wa kesho jumamosi utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akipozi kigagwe na Said Mundi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumamosi ya juni 6 katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
 Bondia Vicent Mbilinyi akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Said Mundi wa Tanga kushoto ni mratibu wa mpambano uho Antony Rutta Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Said Mundi wa Tanga akipima uzito kwa ajili ya mpambano weake na Vicent Mbilinyi kushoto ni Anton Rutta Picha na SUPER D BOXING NEWS

Thursday, June 4, 2015

BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO KUPANDA ULINGONI KUMKABILI MGANDA JUNE 13


 

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Fransic Miyeyusho  'Chichi Mawe' atapanda tena ulingoni june 13 katika ukumbi wa Fruends Corner manzese kuzidunda na Mbaraka Seguye wa Uganda katika mpambano wa raund nane uzito wa Frather Weight

bondia huyo mkongwe alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa sasa yupo fiti na matalajio yake kumpiga kwa K,O mbaya sana mgnda uyo ya raundi ya sita aliwashukuru baadhi ya wadau mbalimbali waliompatia sapoti ya kmbi yake akiwemo Evans Shayo ambaye ni mfanya biashara maarufu wilaya ya Kinondoni kwa kumudumia kambi yake ya maandalizi na Group Agent pamoja wadau wa Ze Bonga waliopo Kinondoni

bondia huo anaingia ulingoni akiwa na kumbukumbu ya kupigwa kwa point na Fadhili majia katika mpambano uliofanyika feb 28

ata hivyo aliwapa uwakika zaidi wa kushinda mpambano uho wa raundi nane katika mpambano uho kuta kuwa na mpambano mwingine wa kimataifa utakaowakutanisha bondia Haji Juma wa Tanga atakae pambana na  Remmy Igga wa Uganda mpambano wa raundi sita Bantam Weight na mpambano mwingine utawakutanisha 

bondia Mada Maugo na Jacobo Maganga katika uzito wa KG 76 mpambano wa raundi kumi Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

BONDIA MRISHO RAJABU 'DAME' ATAMBA KUMCHAKAZA ABDALLAH PAZI JUNE 14 BAGAMOYO

BONDIA MRISHO RAJABU 'DAME' ATAMBA KUMCHAKAZA ABDALLAH PAZI JUNE 14 BAGAMOYO

Na Mwandishi wetu
Bondia Mrisho Rajabu 'Dame' amempania kumchakaza katika raundi za awali bondia Abdalla Pazi 'Mfalme wa Wazalamu' katika mpambano wao wa raundi sita utakaofanyika katika ukumbi wa TASUBA uliopo Bagamoyo mjini juni 14

Rajabu amesema atahakikisha awapi tabu majaji kwa kumsambalatisha kwa K,O ya raundi za awali wakati wa mpambano wao ambao umevuta isia za watu wengi wa Dar es salaam na mkoa wa Pwani

siku hiyo pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo Iddi Pialali 'Simba aliyejeruiwa' atapambana na Sweet Kalulu

wakati Raymond Mbwago atavaana na Halidi Honga na mchezo mwingine mkali zaidi utawakutanisha Mfaume Mfaume wa Manzese na Adam Ngane wa Chanika  pamoja na mipambano mingine mbalimbali 

siku hiyo pia kutapambwa nja burudani kutoka kwa Jumanne Iddi pamoja na Sam wa Ukweli watakaopamba jukwaa hilo kwa ajili ya burudani za muziki wa kizazi kipyaa 

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Monday, June 1, 2015

NGUMI KUFANYIKA TENA BAGAMOYO JUNE 14 UKUMBI WA TASUBA


Na Mwandishi Wetu

NGUMI kupigwa tena Bagamoyo mpambano mkali wa masumbwi utakao wakutanisha Mfaume Mfaume wa Manzese pamoja na Adam Ngange wa Chanika utafanyika Bagamoyo katika ukumbi wa TASUBA siku ya june 14 ambapo watasindikizwa na mipambano mingine mikali siku hiyo

bondia Iddi Pialali 'Simba Aliyejeluiwa' atapambana na Sweet Kalulu wakati Raymond Mbwago atapambana na Haridi Hongo na Ramadhani Sebe atakabiliana na Said Kassim mpambano mwingine utakuwa ni kati ya bondia Abdalla Pazi' Mfalme wa wazalamu' atakae pambana na Haridi Van Dame' wa Kawe

siku hiyo pia kutakuwa na burudani za mziki wa kizazi kipya ambapo msanii Jumanne Iddi na Sam wa ukweli ambao watapamba burudani za mchezo uho wa masumbwi

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

BONDIA FRANCIS CHEKA ALIVYO MSAMBALATISHA MTHAILAND KWA T.K.O YA RAUNDI YA NANE Bondia Francis Cheka kulia akipambana na Kiatchai Singwancha wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Cheka alishinda kwa T.K.O ya raundi ya nane Picha na SUPER D BOXING NEWS
 Bondia Francis Cheka kulia akioneshana umwamba wa kutupiana makonde  na Kiatchai Singwancha wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba Cheka alishinda kwa T.K.O ya raundi ya nane Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Shabani Kaoneka kulia akimtupia konde la nguvu Zumba kukwe wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Kaoneka alishinda mpambano uho kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Seleman Zugo kushoto akipambana na Twaha Kiduku wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila akiwa na wadau wa masumbwi
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo0 wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akiwa na wadau mbalimbali akiwemo kaka yake wa pili kushoto Shabani Mhamila 'Star Boy' wakishudia mpambano wa cheka
Bondia Francis Cheka kulia akioneshana umwamba wa kutupiana makonde  na Kiatchai Singwancha wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba Cheka alishinda kwa T.K.O ya raundi ya nane Picha na SUPER D BOXING NEWS
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...