Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, June 8, 2015

NGUMI KUFANYIKA TENA BAGAMOYO JUMAPILI JUNI 14


Na Mwandishi Wetu

MPAMBANO mkali wa masumbwi unatarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii juni 144 katika ukumbi wa TASUBA Bagamoyo mjini mpambano uho utakaowakutanisha mabondia Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo na Sweet Kalulu wa Dar es salaam

akizungumzia mpambano uho mratibu Muhsini Sharif amesema pambano hili litakuwa la raundi sita uzito wa kg 63 mbali na mpambano uho kutakuwa na mipambano mingine ya kumaliza ubisha kati ya Adam Ngange wa Chanika na Mfaume Mfaume kg 61 pamoja na Abdallah Pazi 'Mfalme wa wazalamu' na Mrisho Rajabu 'Dame' kg 74 wa kawe mpambano mwingine ni kati ya Raymond Mbwago na Halidi Hongo kg 63

aliongeza kwa kusema kuwa pia siku hiyo kutakuwa na burudani za nguvu kutoka kwa wasanii Sam Wa Ukweli na Jumanne Iddi ndio watakaotoa burudani kwa siku hiyo

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...