Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 30, 2010

MISS KINONDONI WATEMBELEA GAZETI LA MAJIRA

warembo waripotembelea BTL

Mhariri wa Dar leo Wiliam Shao akiwaonesha gazeti la leo warembo
wakiongea na mhariri wa majira jumapiri Ponsian Rwechungura
Amina Athumani kushoto akiwa na warembo walipotembelea kampuni ya Bussines Time
Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Bussines Time Mwali Ibrahimu kulia akiwaelekeza warembo wa miss Kinondoni jinsi gazeti linavyotoka kabla ya kwenda kiwandani
Mhariri wa michezo wa gazeti hili, Selemani Mbuguni (kulia) akiwaelekeza jambo warembo wanaowania taji la miss Kinondoni walipotembelea Dar es salaam jana.

MBUNGE WA SINGIDA MJINI MOHAMED DEWJI AGAWA VYANDARUA KWA WAKINAMAMA

Katika Hotuba ya Mh.Mohammed Dewji Mbunge wa Singida mjini alikuwa na haya machache ya kusema kwa Wanachi wake “Ndugu Zangu pamoja na mambo mengine leo hii nimekuja katika ziara ya kawaida ya kuhamasisha maendeleo ndani ya jimbo langu.

Lakini kama mtakumbuka niliwaandikia barua maafisa watendaji wa vijiji waniorodheshee majina ya mama wajawazito pamoja na watoto walio na umri chini ya miaka 5 ili nije niwapatie vyandarua vyenye dawa”.MO aliendele kusema “Ikiwa hii ni awamu ya pili kwani kwa awamu ya kwanza nilitoa Vyandarua zaidi ya 6,000 ndani ya vijiji vyetu 19 vya manispaa,mwaka 2007.

Ndugu zangu lakini mnaweza kujiuliza kwa nini nimelenga makundi haya,nimelenga makundi haya kwa sababu ugonjwa wa malaria bado unaongoza kwa kuuwa watu wengi mpaka sasa,tofauti na magonjwa mengine,Na takwimu zinaoonyesha,wanaoathirika zaidi na gonjwa hili la malaria ni mama wajawazito na watoto wenye Umri chini ya miaka 5,Takwimu zinaonyesha kuwa katika kila watoto 100 watoto watano wanapoteza maisha kwa ugonjwa wa malaria”MO alizidi kusisitiza.

Ndugu zangu sasa mimi kwa kutambua hili tatizo,nimeona bora nihamasishe jamii itambue umuhimu wa kutumia vyandarua vyenye dawa ya Kinga,nasisitiza kuwa hii ni hamasa tu,pia nawaomba viongozi wenzangu tushirikiane katika kutoa elimu juu ya matumizi ya Vyandarau”alisema MO.Mbali na MO kutoa vyandarua 6000,Kampuni ya simu za Mkononi Vodacom Tanzania Kitengo cha Vodacom Foundation kimetoa Vyandarua 10,000 jimboni kwa Mh.Mohammed Dewji hii yote ni kupambana na vita dhidi ya Malaria.NA www.fullushangwe.blogspot.com

SEREKALI YAONGEZA WIKI MBILI ZA USAJIRI WA SIM CADYBAADHI YA WANANCHI WAKISUBILI KUSAJIRI SIMU CADY ZAO

SOKO LA PAMOJA KUANZA KESHO

WAZIRI wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC),Dkt. Diodorus Kamala amewahakikishia watanzania kuondoa hofu ya kunyang'anywa ardhi yao kutokana na Tanzania kujiunga na Jumuiya hiyo.

Dkt.Kamala alisema kuwa ardhi ya Tanzania itabaki kuwa mali ya watanzania na haitaguswa na raia kutoka nje ya nchi kwa kisingizio soko la pamoja.

Hayo aliyasema Dar es Salaam juzi wakati akitoa ya utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo na kuongeza kuwa Tanzania inatazamiwa kunufaika na soko la watu milioni 130 kwa kuuza bidhaa zitokanazo na kilimo katika jumuiya baada ya kuboresha mazingira ya uzalishaji.

Dkt. Kamala alisema kuwa Tanzania ndio nchi pekee inayotarajiwa kutoa chakula kwa nchi za EAC kutokana na kuwa na ardhi nzuri ya mazao hivyo hatuna budi kutumia nafasi hiyo kuimarisha uchumi na maendeleo kwa ujumla.

"Jumuiya ya Afrika Mashariki imejaliwa kuwa na vyanzo vya maji, nishati, ardhi na hata mbolea hivyo kupitia jitihada za kikanda;Sekretarieti ya EAC imejipanga kuibua mpango wa kupatikana kwa utaratibu wa kuvuna mbolea itakayosaidia utekelezaji wa mkakati wa maendeleo ya kilimo,"alisema.

Aidha, Dkt. alisema kuwa suala la uuzwaji wa chakula nje ya nchi ambalo limekuwa kikwazo kwa wakulima kutokana na baadhi ya viongozi kuzuia limepitishwa na Mawaziri wa EAC na limewasilishwa kwa wakuu wa nchi hizo kutiliwa saini siku yoyote.

Alisema kuwa kitendo cha kumzuia mkulima kutouza chakula nje ni kumkwamishia maendeleo na malengo kwa kuwa ana uhuru wa kuuza nje kama nchi husika imeshindwa kununua kwa bei ya faida inayolingana na gharama alizotumia.

Vile vile alisema kuwa itifaki ya Umoja wa Forodha ya Afrika Mashariki mwaka 2004 imeridhiwa na nchi zote uanachama na malengo makuu ya itifaki hiyo ni kuondoa ushuru wa forodha kwa biashara ya bidhaa miongoni mwa nchi uanachama.

Pia kuweka wigo wa pamoja wa biashara wa ushuru wa forodha kwa bidhaa zitokazo nje ya jumuiya, kuweka vigezo vya jumuiya vya kutambua uasili wa bidhaa na kuondoa vikwazo visivyo vya kiforodha.

Dkt. Kamala alisema kuwa kila nchi kuorodhesha bidhaa nyeti zinazotozwa ushuru wa forodha kwa viwango vikubwa zaidi ya kiwango cha juu cha asilimia 25.

Alisema kuwa zipo bidhaa nyeti (sensitive Products) kutoka nje ya jumuiya ambazo hutozwa ushuru zaidi ya viwango hivyo vitatu ikiwa madhumuni ni kuzuia ushindani usio wa halina kulinda viwanda na uzalishani wa ndani. ya

Dkt. Kamala aliwataka watanzania kuwa wamoja wakati wa soko la pamoja kwa kusaidiana pale inapopatikana nafasi za ajira na kuachana na uoga ambao ni silaha ya udhaifu katika maendeleo.

Alisema kuwa watanzania wanatakiwa kuonesha uzalendo, nia, kujiamini na kudhubutu kupambana na soko la pamoja kwani wizara hiyo ipo sambamba katika kufanikisha elimu inawafikiwa wote kuhusu faida ya EAC na jinsi ya kukabiliana mabadiliko.

Hata hivyo alisema kuwa shirikisho hilo halitavunjika tena kama ilivyotokea mwaka 1977 kutokana na kutokana na mikataba madhubuti iliyowekwa ikiwemao ya sheria ya kila nchi yoyote iliyo EAC lazime ifuate sera za soko la uchumi na mengineyo.

Dkt. Kamala alisema kitendo cha nchi ya Kenya kupiga vita Tanzania kutouza pembe za ndovu kimetoa picha ya wazi kwa watanzania kutoa maamuzi ya kuridhia au la katika mazungumzo yanayoendelea sasa kuhusu suala hilo.

WAFANYAKAZI WA TBL WASHEREKEA SIKU YA FAMILIA

Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Trevor Gray (kulia) akimzawadia mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo box moja la kilaji cha safari lager Siku ya Familia za wafanyakazi wa kampuni hiyo, iliyofanyika katika Hoteli ya South Beach, Kigamboni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na familia zao, wakishindana kuvuta kamba wakati wa Siku ya Familia iliyofanyika katika Hoteli ya South Beach, Kigamboni, Dar, wikiendi ilopita
Mfanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Sufiani Athuman, akishindana kucheza pool na mfanyakazi mwenzie Rajabu (hayupo pichani) katika pambano lililofanyika Siku ya Familia iliyofanyika katika Hoteli ya South Beach, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Wa pili kushoto ni mwamuzi wa pambano hilo, Skubi Mlapakolo. AKA Skubi duu.picha na www.mtaa kwa mtaa.blogspot.com

KESHO NI KUANZWA RASMI UTEKELEZAJI WA SOKO LA PAMOJA LA AFRIKA MASHARIKI KWA NCHI ZA TANZANIA,KENYA,BURUNDI,RWANDA NA UGANDA

Katibu Mkuu wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki DR. Stergomena
Katibu Mkuu wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki DR. Stergomena Taxkizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanzishwa rasmi utekelezaji wa soko la pamoja Afrika Mashariki kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Uledi Mussa
Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Uledi Mussa kulia akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari iliyofanyika ofisini kwake leo kulia ni Mhasibu wa Wizara hhiyo Bw. Ahadi Msangi

WAKATI utekelezaji wa Soko la pamoja kwa nchi za Jumuia ya Afrika mashariki unaanza Kesho, WIZARA ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini imewatoa hofu Watanzania kwa kusema kuwa hakutokuwa na uingiaji holela wa wageni kutoka nje kwa kuwa ushirikiano utafuata sheria na taratibu zilizopangwa.

Pamoja na ulegezaji wa mashariti ya uingizaji na utoaji bidhaa nchini, pamoja na kuwepo fursa huru katika utafutaji ajira, Wizara imesema uanzishwaji wa soko la pamoja hauta athiri Sheria na taratibu ambazo zilikuwepo kabla ya uanzishwaji wa ushirikiano.
Fulsa zilizofunguliwa na Tanzania ni pamoja na Walimu wa Vyuo Vikuu elimu ya juu kuanzia mwaka 2010, Sekondari katika masomo ya Hisabati na Sayansi-2011, shule za msingi-2010, walimu wa vyuo vya kilimo-2010, Uhandisi Madini, na Ufundi sanifu-2011, Maofisa Ugani 2015,wauguzi na wakunga- 2010 pamoja na waongoza ndege kuanzia mwaka 2012.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki Dkt Stergomena Tax alisema, hakuna haja ya Watanzania kuhofia kupoteza chochote kwa kuwa shirikisho halitaendeshwa kwa misingi ya ubaguzi hama wa rangi au utaifa.
Alisema cha msingi ni kwa watanzania wenyewe kutambua na kuchangamkia fursa zitakazojitokeza, ikiwa ni pamoja na kujitahidi kutoa huduma bora zenye ushindani badala ya kutegemea kubebwa na kupendelewa.

"Watanzania tunapaswa kujiamini katika utendaji kazi, wengi tumezoea masuala ya kubebwa na kupendelewa kwa misingi ya kujuana badala ya kutegemea uwezo utendaji kazi, hii ni dhana potofu na tunapaswa kuachana nayo, tusimame wenyewe" alisema Dkt. TAX.

Alisema utekelezaji wa soko la pamoja utakuwa wa Hatua kwa Hatua kulingana na ratiba na taratibu zilizokubaliwa na kuwekwa ndani ya itifaki na nchi wannachama, na kuwa hatua hiyo itatoa nafasi ya kufanyika marekebisho mahala ambapo yatahitajika.
"Utekelezaji wa soko la pamoja utaongozwa na sheria taratibu na kanuni zilizokubaliwa kwa kuondoa vikwanzo ulegezaji wa masharti katika maeneo ya msingi" alisema.
Dkt Tax alisema kuwa upande wa biashara ya bidhaa zote zinazozalishwa ndani ya jumuiya ya afrika mashariki na kukidhi vigezo vya utambuzi wa asili wa bidhaa zinaweza kusafirishwa kutoka nchi moja hadi nyingine bila kutozwa ushuru wa forodha.
Aidha alisema kuwa kuanzia julai moja Raia wa Afrika mashariki watakuwa huru kuingia na kuishi na kufanya kazi katika nchi yoyote ndani ya Jumuiya na kupata huduma nyingine kama kutembelea ndugu, matibabu, masomo au utalii, alimradi tu wafuate taratibu zilizowekwa na idara za uhamiaji za nchi husika.
"Ili kunufaika na uhuru huu raia mhusika atawajibika kuwa na hati halali ya kusafiria na kupita katika vituo rasmi mipakani ambako baada ya kukamilisha taratibu za uhamiaji atapewa hati ya kuingia na kukaa nchini kwa kipindi cha miezi sita,"alisema.

Alisema kuwa kwa upande wa ajira raia wa Nchi Wanachama anaruhusiwa kutafuta ajira katika meneo yaliyofunguliwa katika nchi yoyote na kutobaguliwa kwa misingi ya utaifa katika ajira na maslahi na haki nyingine za mfanyakazi.
Alisema kuwa mfanyakazi ataruhusiwa kuambatana na mke wake au mume pamoja na watoto ambapoa nao watanufaika na uhuru wa kuariwa au kujiajiri katika nchi husika.

Alisema katika kuanza kwa biashara ya huduma kwa kunazia nchi wanachama zimekubaliana kuondoa vikwazo hatua kwa hatua na vikwanzo vipya kwa watoa huduma kutoka katika nchi wanachama katika sekta kuu saba za huduma zilizoainishwa

Vilevile alisema kuwa katika soko la mitaji nchi wanachama zimekubali kuondoa vikwanzo kwa raia wa Afrika mashariki kuwekeza kwenye soko la mitaji katika Nchi nyingine ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hatua kwa hatua kwa mujibu wa ratiba ya utekelezaji.

Alisema kuwa watakuwa na fursa ya kuanzisha na kuendsesha shughuli za biashara na uchumi katika nchi yoyote mwanachama wa jumuiya ya afrika mashariki bila kubaguliwa kwa misingi ya Utaifa wa kampuni au mjasiriamali.
Aidha nchi wanachama imekubali kuandaa orodha ya vikwazo katika sheria zao na kuviwasilisha katika baraza la mawaziri la jumuiya ya Afrika mashariki ndani ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya soko la pamoja kupata nguvu ya kisheria.

Hata hivyo alisema kuwa raia anayetaka kukaanchini anatakiwa kuomba kwa mamlaka husika kibali cha ukazi ndani ya siku 30 tangu tarehe ya kuingia chini akiambatanisha hati halali ya kusafiria kibali cha kufanya kazi nchini na nyaraka nyingine zitakazo hitajika na ofisi ya uhamiaji.

KIKAPU MUHUNGANO KUFANYIKA MWANZONI MWA MWEZI UJAO ZANZIBARMichael Maluwe katibu mkuu wa TBF akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es salaam kushoto ni katibu mkuu wa TBF Alexander Msofe.

Tuesday, June 29, 2010

TAYSON FURY ATOA UBINGWA WA NGUMI UZITO WA JUU UINGEREZA KWA KUMTWANGA JOHN MCDERMOTT

TYSON Fury ametwaa ubingwa wa ngumi katika uzito wa juu Uingereza baada ya kumtwanga
mpinzani wa John McDermott.
Mpiganaji huyo wa Manchester mwenye urefu wa futi 6 na inchi 7 sasa atapambana na Derek Chisora Oktoba baada ya kumwangusha mara mbili McDermott kabala ya kumaliza pambano katika raundi ya tisa kwenye ukumbi wa Brentwood Leisure Centre.
Fury mwenye umri wa miaka 22, alishinda kwa pointi dhidi ya McDermott mkazi wa Essex Septemba mwaka jana.Alisema: "Nilimpiga McDermott mara ya mwisho na nimefanya tena hivyo, sasa bila ya kuhitaji maamuzi ya majaji.

nyota wa Brazil Maicon kujiunga na Mournho

LONDON, Uingereza
JOSE Mourinho ameipiga bao
Manchester City katika mbio za kumsaini mchezaji wa kibrazili
Maicon.
Beki huyo wa Brazil aliye katika michuano ya Kombe la Dunia amekubali kujiunga na The Special One katika timu ya Real Madrid akitokea Inter Milan kwa ada ya pauni milioni 25 mara baada ya kutoka Afrika Kusini.
City ilitarajia kumweleza mchezaji huyo kuungana na Roberto Mancini katika mapinduzi ya Eastlands.
Lakini Maicon amemwambia kocha wake wa zamani Mourinho kamba anataka kuungana naye
Bernabeu msimu ujao.
Uhamisho huo umekuwa ukileta mashaka kwa Liverpool kuwa huenda kocha Rafa Benitez atatumia fedha hizo kurudi anfiel kumtaka
Javier Mascherano.
Awali nyota wa Brazil Maicon aliiambai klabu ya Manchester City kwamba anataka kuichezea Real Madrid.

UHOLANZI YATINGA 8 BORA

Wachezaji wa Uholanzi wakimpongeza Arjen Robben baada ya kuifungia timu yake bao dhidi ya Slovakia katika mechi ya hatua ya 16 bora iliyochezwa kwenye Uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban, jana. Uholanzi ilishinda bao 1-0.

MISS TEMEKE KUPATIKANA MWEZI UJAO

Baadhi ya warembo wanaowania taji la Miss Temeke wakiwa katika picha ya pamoja taji la Miss Temeke 2010 linalotarajia kufanyika pale TCC Sigara Chang'ombe Julai 9/ 2010,www.jihachie.blogspot.com

WAJASILIAMALI NCHINI KUKUTANISHWA NA ZAIN JULAI 20

Meneja Mauzo wa Zain Tanzania Zedi Selemani (kulia) akiongea wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu siku ya Wajasiliamali yatakayofanyika Julai 20 katika Viwanja Vya Karimjee jijini Dar es Salaam chini ya Udhamini wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania. Kushoto ni Rais wa East Africa Speakers Bureau, Paul Masahuri waandaaji wa maadhimisho hayo.
Rais wa East Africa Speakers Bureau, Paul Mashauri (kushoto) akiongea wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu siku ya Wajasiliamali itakayofanyika Julai 20 katika Viwanja Vya Karimjee jijini Dar es Salaam chini ya Udhamini wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania. Kulia ni Meneja Mauzo wa Zain Zedi Seleman.

WAISLAM WAONDOLEWA HOFU JUU YA MAHAKAMA YA KADHI NCHINI

Baadhi ya wanahabari wakifatilia mkutano
Katibu mkuu wa BAKWATA Bw. Suleiman Lolila akizungumza kwenye mkutano huo leo
Mufti wa Tanzania Shehe Issa Shabani Simba (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya uwanzishwaji wa mahakama ya Kadhi nchini,kushoto ni Shehe wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Alhad Mussa Salumu.
KATIKA KIPINDI HIKI CHA SABA SABA TANGAZA NASI UFAHAMIKE NA WENGI KUPITIA BLOG HII WASILIANA NASI KWA SIMU O713/0754/0774/0787-406938 AU emai mhamila1@gmail.com TEMBELEA www.burudan.blogspot.com burudan mwanzo - mwisho

KINONDONI KUPATA MREMBO WAKE JULAI 2

YUSUPH GEORGE katikati akiwa na mkewe waandaaji wa shindano la miss KINONDONI wakitangaza zawadi za warembo kulia ni mdau Selemani Mbuguni.

Jumla ya warembo kumi na moja wanatarajia kupanda jukwaani kuwania taji la mrembo wa KINONDONI lilopangwa kufanyika JULAI 2 MWAKA HUU.

Mshindi wa pili atapata shilingi milioni moja na mshindi wa tatu laki nane

Monday, June 28, 2010

ZAIN WAKABIDHI ZAWADI ZA WASHIRIKI WA AFRICAN CHALENGE

Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Zain Bw. Muganyizi Mutta, (kulia) AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI
Mwandishi wa habari wa chanal ten akizungumza na Justiu Rwelengera
Baadhi ya wanafunzi wakiesabu dola zao baada ya kukabidhiw kutoka kushoto ni Fredy Mwakalinga Rodriaue Sakaya Deliphinius Karumuna na Justiu Rwelengera
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Zain Bw. Muganyizi Mutta, (kulia) akimkabidhi Mratibu wa Chuo Kikuu ARDHI Dr,Mbura Omari dola 1600 kwa ajili ya kutambua ushiriki wao katika mashindano ya Zain Afrika Challenge Dar es saam, jana.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Zain Bw. Muganyizi Mutta, (kulia) akimkabidhi Mratibu wa Chuo Kikuu Huria Bw. Salim Hamad, dola 1600 kwa ajili ya kutambua ushiriki wao katika mashindano ya Zain Afrika Challenge Dar es saam, jana.Zain yakabidhi zawadi ya pesa taslim kwa Vyuo viliyoshiriki ZAC

Dar es Salaam June 28, 2010.

Zain Tanzania leo imekabidhi zawadi za pesa taslim kwa baadhi ya Vyuo Vikuu na wanafunzi walioshiriki katika mashindano ya Zain Africa Challenge yaliyomalizika hivi karibuni.
Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania Muganyizi Mutta alikabidhi Dola za Marekani 1600 kwa Meneja Masoko wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Omary Mbula pamoja na Salim Hamadi kutoka Chuo Kikuu Huria cha Dar es Salaam kwa ushiriki wa vyuo vyao katika mashindano ya ZAC. Dola 1000 ni za chuo wakati dola 600 ni kwa ajili ya washiriki sita kutoka vyuo hivyo ambapo kila mwanafunzi, kocha na mratibu wanapata dola 100 kila mmjoja
Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi kila mmoja jana alipata dola za Marekani 500. Chuo Kikuu cha Ardhi ni miongoni mwa Vyuo Vikuu vitano vilivyofuzu kuingia fainali nchini Uganda. Chuo cha Ardhi pia kitapewa dola za Marekani 5000 za kukisaidia chuo na pesa hizo zitaingizwa katika akaunti ya chuo kuboresha elimu chuoni hapo..
Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania alitaja Vyuo Vikuu vingine vitakavyopokea pesa za ZAC kama; Chuo Kikuu cha Sokoine University na Chuo Kikuu cha Mzumbe kutoka Morogoro, Saint John na Chuko Kikuu cha Dodoma kutoka Dodoma, pamoja na Teofilo Kisanji University kutoka Mbeya na State University cha Zanzibar. Vyuo hivi kila kimoja kitapata dola za Marekani 1000 fedha za chuo na kila mshiriki kati ya washiriki sita atapata dola.
Aidha alivitaja vyuo vitakavyopokea Dola za Marekani 10,000 kama fedha za chuo na kila mshiriki kuondoka na dola 1000 kuwa ni chuo kikuu cha Arusha University na Chuo Kikuu cha Tumaini ambavyo vilifuzo kuingia fainali zilizorushwa kwenye luninga. Chuo kikuu cha Zanzibar kwa upande wake kitapata dola za Marekani 5000 na kila mshiriki dola 500. Chuo hiki ni miongoni mwa vyuo vikuu vitano vilivyofuzu kushiriki katika mashindano ya Kampala.
Zain iliwekeza zaidi ya dola za Marekani 1000,0000 katika Zain Africa Challenge mwaka huu ikiwa ni sehemu ya programu yake inayolenga kukuza elimu barani Afrika

MWISHO WA KUSAJILI LAIN 30 JUNE 2010

Bahadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wakiwa wamejitokeza kusajili laini za simu zao za mkononi jana baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutangaza faini kwa watakaoshindwa kusajili simu zao.mwisho kusajili simu hizo ni 30.6.2010. watu wengi wamekuwa wakijitokeza siku za mwisho mwanzoni walikuwa wapi kusajili

VIPAJI MISS KINONDONI VYAPATIKANA

Hii ndiyo tano bora ya shindano la kipaji la Redds Miss Kinondoni lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Hoteli ya Giraffe Ocean View iliyoko Mbezi jijini Dar es salaam warembo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya jaji mkuu Gerald Hando kutangaza matokeo, kutoka kulia ni Irene Hezron, Salma Ally, Alice Lushiku, Caroline Mbembo na Tamara Ally.www.fullshangwe.blogspot.com

Sunday, June 27, 2010

TWANGA YATIMIZA MIAKA KUMI KWA MAANDAMANO

maandamano ya mashabiki wa TWANGA PEPETA toka VIJANA hadi LEADERS
ASHA BARAKA na baadhi ya mashabiki wa TWANGA PEPETA akiwa katika viwanja vya LEADERS

DARAJA LA MANZESE LAENDELEA KUWA KIVUTIO KWA WAPITA NJIA

Watu wakivuka kupitia Daraja la Manzese
Daraja la manzese

BANDA LA KAMPUNI YA MAKAI MORINGA (MLONGE) ENTERPRISES KUPAMBWA NA WAREMBO WA MISS UTALII SABASABA MWAKA HUU

Eileen Kasubi Katikati akiwa na warembo wanaowania taji la Miss Utalii Tanzania Kampuni ya Makai Moringa (Mlonge) Enterprises ni moja ya wadhamini wa mashindano hayo

TAARIFA KWA VYOMBO KWA HABARI

Ndugu waandishi wa habari Jina langu ni Eileen Kasubi , Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Makai Moringa (Mlonge) Enterprises ambayo inajushughulisha na ulimaji na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na mti wa mlonge kwa zaidi ya miaka 8 sasa.

Tulishirikiana na kampuni ya kimataifa ya Optima of Africa, tulihamasisha kilimo cha mti wa zao hilo na kununua mazao yake kwa wakulima .

Mlonge ni mti wa maajabu kwani ni lishe,kinga na tiba kwa zaidi ya magonjwa 300 ya binadamu. Bidhaa zote za mlonge zinazotengenezwa na Makai Enterprises ni bora na zimethibitishwa na Mkemia Mkuu wa Serikali na Mamlaka zote za kitaifa na mataifa.

Bidhaa hizo zinatokana na majani, mbegu,mizizi na mti wenyewe wa Mlonge kwa kutengeneza virutubisho asili,vipodozi, na madawa ya mwili wa binadamu.

Awali tulikuwa na bidhaa kuu 8 ambazo ni
1)Unga wa majani ya Mlonge ambao ni lishe, tiba na kinga zaidi ya magonjwa 300 inalinda afya ya binadamu pamoja na kurutubisha mifumo mbalimbali ya mwili.
2)Mbegu za Mlonge hutibu Malaria, Saratani ya tumbo,hupungusa sonona stress, huleta hamu ya kunywa maji,huongeza kinga ya mwili CD4s
3) Mafuta ya Mlonge ya kula huua sumu ndani ya chakula, huua aina nyingi za bacteria kwenye chakula na huondoa cholesterol
4)Mafuta ya kupaka mwilini (Moringa skin care oil) huondoa fangazi kwenye ngozi, chunusi, harara makovu pamoja na mba mwilini
5)Mafuta ya kuchua (Moringa Massage Oil) Huondoa maumivu ya mgongo, kiuno, miguu, hutibu baridi ya-bisi na hupasha misuli joto.
6)Sabuni ya kuogea (Moringa Toilet soap) Hutibu magonjwa mbali mbali ya ya ngozi,fangazi, chunusi ,mba na hulinda ngozi yako
7)Mafuta ya nywele (Moringa Hair food)hung’arisha na kuimarisha nywele huondoa mba na mapunye kichwani na kurefusha nywele.
8)Moringa Sports Ointment (Mafuta ya wana michezo) Huondoa maumivu ya misuli inayokakamaa na hushtua neva na misuli iliyolala kutokana na maumivu au kutokana na kiharusi.

Nafurahi kuwajulisha kuwa leo hii tunazindua bidhaa zetu mpya
ambazo ni:-
1) Moripower - Inaongeza nguvu za kiume
2)Moribites - Inatibu Kisukari
3)Morident - Tiba ya Meno)
4)Moringa Shampoo - Inaondoa mba na miwasho yote kichwani , Inaondoa uchafu kichwani kwa nywele za aina yote
5)Moringa Face & Body Scrub -Huondoa madoa, chunusi usoni, mgonngoni, na sehemu zote za mwili
6)Moringa Body Shower - Sabuni ya Maji ya Kuogea
7)Moringa Hand wash Sabuni Asili ya kunawia mikono
8)Moringa Detergent and Disnfectant - Dawa za kusafishia sakafu,vyoo na masink
9)Sabuni Mwaniki (Ladies Soap) - Sabuni maalum na nyeti kwa kina mama humaliza fangazi katikati ya mapaja na kwapani .

Kutokana na mabadiliko ya kisayansi na teknologia, matumizi ya bidhaa zenye kemikali yamekuwa yakiongezeka kila siku, huku madhara yake yakiadhiri maisha ya kila siku ya binadamu, kuanzia katika vipodozi, tiba na usafishaji. Ndio maana leo hii tunawashuhudia watu wakiishi maisha mafupi kuliko awali, watu kuonekana wazee kuliko umri wao, magonjwa ya ngozi huongezeka na hata wanaume wengi kupoteza ulijari na nguvu asili za kiume, wakati mwingine baadhi ya magonjwa hujenga sugu ya kutotibika.

Tumeamua kuwatumia na tunawashukuru sana warembo wa Miss Utalii Tanzania, kuzindua Bidhaa hizi za mlonge, kutokana na ukweli kuwa wamekuwa msitari wa mbele kuhamasisha utamaduni na utunzaji wa misitu ya nchi, ambako mlonge pia unatoka. Tutawatumia pia warembo hawa katika maonyesho ya kitaifa 7/7 mwaka huu, ambako bidhaa hizi zitapatikana katika banda letu liliopo katika mabanda mapya ya 7/7 , Banda la Maliasili na Utalii na Banda la SIDO .

Mwisho nitoe wito kwa watu wote kutumia bidhaa asili za Mlonge uliotengenezwa na Makai kwa maisha marefu zaidi. Tayari bidhaa hizi zimepata soko katika nchi mbai mbali duniani zikiwemo Ujerumani, Marekani, Denmark, Japan, Africa Kusini, Malawi na nchi nyinginezo.

Ofisi zetu zipo:-
Pamba House G0orofa ya Pili Chumba No. 205
Simu No. + 255 2135531/ 0713 607408/0787 607408
0767 838188
Email: makaimlonge@yahoo.com

HAMISI DAKOTA HAPORA SIMU KWA AJIRI YA KUSOMA MESEJI

Hamisi Dakota huyu noma akifuatilia simu ya jamaa yake kujua undani wake kuna nini ,mkuu huyu ndiye kibosile wa TID.akiwa katika mhemuko na mtu wake wakati wa moja ya shoo za TID jijini Dar es salaam

MISS ILALA HUYU HAPA SI MWINGINE NI BAHATI CHANDO

Miss Ilala 2009,Sylivia Shally akimvisha Taji mrithi wake,Bahati Chande usiku wa kuamkia leo mara baada ya kuibuka mshindi na kulinyakua taji la Miss Ilala 2010, katika ukumbi wa Ubungo Plaza,

Miss Ilala 2010 Bahati Chando akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Consolata Lukosi na Mshindi wa tatu na Salma Mwakalukwa mshindi wa pili mara baada ya kutangazwa kuwa washindi wa shindano la miss Ilala lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam,
WAREMBO wa tano BORA Miss Ilala wakiwa katika picha ya pamoja katikati ni Miss Ilala Bahati Chando Consolata Ulkosi mshindi wa pili kulia na mshindi wa pili Salama Mwakalukwa kushoto wengine kulia ni Neema Alen mshindi wa tano na Ummy Mohamed mshindi wa nne.

KANDA YA KATI YAPATA MERMBO WAO

Mshindi wa Miss Kanda ya kati Beatrice Singh akiwa na wenzake waliomfuatia Wilani Etami (kushoto) na Pili issa baada ya kutangazwa matokeo ya ushindani huo. picha na www.prhabari.blogspot.com

WANAFUNZI WA KIKE WAJENGEWA UWEZO WA MASOMO YA SAYANSIMARIAM MNANGWA MMOJA KATI YA WANAFUNZI 130 WALIOKUWA KATIKA KAMBI MAALUM KWA AJILI YA MASOMO YA SAYANSI KWA WANAFUNZI WA KIKE KUTOKA MIKOA YA PWANI NA MOROGORO AKIWAONESHA WENZAKE MATOKEO YA MAJARIBIO WALIOKUWA WAKIFANYA. LENGO LA KAMBI HIYO NI KUWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI WASICHANA KUPENDA NA KUFANYA VIZURI KATIKA MASOMO YA SAYANSI, KAMBI HIYO ILIFANYIKA KATIKA SHULE YA SEKONDARI KILAKALA MKOANI MOROGORO

MWALIMU PRUDENCIANA NDUMWA AKITOA MAELEKEZO KWA BAADHI YA WANAFUNZI WA KIKE WALIOKUWA KATIKA KAMBI YA MAALUM YA SAYANYASI KWA AJILI YA WANAFUNZI WASICHANA 135 KUTOKA SHULE MBALIMBALI ZA MIKOA YA PWANI NA MOROGORO, LENGO LA KAMBI HIYO NI KUWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI WASICHANA KUPENDA NA KUFANYA VIZURI KATIKA MASOMO YA SAYANSI, KAMBI HIYO ILIFANYIKA KATIKA SHULE YA SEKONDARI KILAKAL MKOANI MOROGORO
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...