Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 19, 2010

WANAMICHEZO BORA WA TASWA WAKABIDHIWA TUZO ZAO


Wadau wakiwa wamepozi kufatilia matukio mbalimbali kutoka New Habari kutoka kulia ni Rachel, Zaituni na Winniefrida.
Washindi Mwanaidi Hassani (Netiboli), Juma Kaseja (Mpirawa miguu) na David Nyombo (vitu vizito) wakisubri kutangazwa kwa mwanamichezo bora wa mwaka 2009.Hata hivyo Mwanaidi aliibuka mshindi na kuwa katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi usiku.(Picha na Zuberi Mussa)Mwenyekiti wa baraza la michezo la Taifa Idd Kipingu akimkabidhi tuzo mwanamichezo Bora wa mwaka 2009 Mwanaid Hassani baada ya kuwashinda wachezaji Juma Kaseja na David Nyombo kwenye hafla ya kukabidhi tuzo hizo
Mhariri wa Gazeti sports starehe Masoud Sanane (kushoto) akimkabidhi tuzo mwanamichezo Bora wa mwezi Sept. John Boko wakati wa hafla ya kuwapa zawadi washindi wa mwaka 2009 Dar es Salaam
Wasanii wa kikundi cha hakuna matata kutoka Kinondoni Seleman Msuwa juu na Alli Mohamed wakitoa Burudani kwa mashabiki waliofika kwenye Hotel ya New Africa kushuhudia tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka 2009
Wanamuziki wa Kalunde Band wakiongozwa na meneja wa bendi hiyo Debora Nyangi kushoto wakifanya vitu vyao katika hafla ya tuzo za mwanamichezo bora wa mwaka wa chama cha waandishi wa habari za michezo nchini TASWA jana kwenye hoteli ya New Africa jijiniu Dar es salaam.
Duh wadau wakipozi kwa madaha mbele ya Camera ya FULLSHANGWE kutoka kushoto ni Dina Ismail Mahmoud a.k.a Mama Pipiro Tanzania Daima, Cesilia Radio Uhuru, baba mkubwa Masoud Sanani Busness Time, Teddy Mapunda Meneja Mkuu Uhusiano na Jamii Serengeti Breweriers ambao ndiyo wadhamini wa tuzo hizo, Angela Msangi TBC1 na mdau Suleiman Mbuguni a.k.a Mzee wa Harua
Waddhamini wakuu wa tuzo hizo Serengeti Breweriers, mgeni wa heshima pamoja na viongozi wa chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA wakipiga picha ya pamoja na wanamichezo wote walioshinda tunzo mwaka jana 2009.www.fullshangwe.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...