Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 24, 2010

MREMBO MWENYE KIPAJI KINONDONI KUPATIKANA JUMAPILI


Mrembo mwenye kipaji Kinondoni kusakwa Jumapili

Na Mwandishi Wetu

WANYANGE wanaowania taji la Redd's Miss Kinondoni 2010, Jumapili wanatarajia kupanda jukwaani kumsaka mrembo mwenye kipaji 'Miss Talent 2010'.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Kinondoni, Yusuf George alisema kila kitu kuhusu mashindano hayo yamekamilika na kinachosubiriwa ni kumpata mnyange mwenye kipaji.

Mwenyekiti huyo alisema mshindi atakayepatikana katika kinyang'anyiro hicho atatangazwa katika fainali za mashindano ya Redd's Miss Kinondoni 2010.

"Kila kitu kinakwenda vyema kuhusiana na mashindano haya ya kumsaka Miss Talent 2010, kinachosubiriwa sasa ni Jumapili ifike ili kumpata mshindi," alisema Mkurugenzi huyo.

Yusuf alisema mashindano ya kumsaka Miss Talent yatafanyika katika ukumbi wa hoteli ya Geraffe Ocean View iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Akizungumzia mashindano ya Redd's Miss Kinondoni, Yusuf alisema mashindano hayo yatafanyika Julai 2, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City.

Alisema washiriki wote wapo katika hali nzuri na kila mmoja anajitapa kunyakua taji la kanda hiyo, ambayo inaoongoza kwa kutoa Miss Tanzania na pia mwaka 2005, Miss Kinondoni alifanya vizuri Miss world kwa kuweza kutwaa taji la Miss World Afrika.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...