Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 29, 2013

VIPAJI VYA MCHEZO WA SOKA MKOA WA TANGA HIVI HAPA


Mchezaji wa timu ya Watukutu kulia Idrisa Bakari akijaribu kumtoka mchezaji wa timu ya Sepras ya jijini Tanga wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika katika viwanja vya walewale Makolola jijini Tanga leo picha na blog ya SUPER D

Mchezaji wa jimu ya Sepras Hassani Abdallah akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Watukutu wakati wa mchezo wao wa kirafiki picha na blog ya SUPER D

TIMU YA Sepras picha na blog ya SUPER D

Wachezaji wa Watukutu


GAPCO TANZANIA YAINGIA MKOA WA TANGA KUFANYA PROMOSHENI YAKE YA GAPCO RELSTAR


Mwakilishi wa Kampuni ya Gapco T LTD Bw. Atanas Jumbe kulia akimkabizi zawadi kwa Mwakilisha wa Ofisa utamaduni wa Mkoa wa Tanga Bi,Tima Koja wakati wa promosheni ya Gapco Relstar inayoendelea katika jiji laTanga jana eneo
picha na BLOG YA SUPER D
Mwakilishi wa Kampuni ya Gapco T LTD Bw. Atanas Jumbe kushoto akimkabizi zawadi kutoka Kampuni ya Gapco Tanzania Bw,Amoody Amiri Koja wakati wa promosheni ya Gapco Relstar inayoendelea katika jiji laTanga jana eneo
picha na
BLOG YA SUPER D

Wasanii wa  JCB Dominion wakitoa burudani wakati wa promosheni ya Gapco Relstar Oil inanayotengenezwa na Kampuni ya Gapco T LTD Eneo la Makolola  Tanga kutoka kushoto ni Omar Salimu na Jafari Halawi picha na Blog ya  Super D

Wasanii wa  JCB Dominion wakitoa burudani wakati wa promosheni ya Gapco Relstar Oil inanayotengenezwa na Kampuni ya Gapco T LTD Eneo laMkwakwani Tanga  kutoka kushoto ni Omar Salimu Halima Masoud na Jafari Halawi picha na BLOG YA SUPER D

Mwakilishi wa Kampuni ya Gapco T LTD Bw. Atanas Jumbe kushoto akimkabizi zawadi kutoka Kampuni ya Gapco Tanzania Bw, Keya Juma wakati wa promosheni ya Gapco Relstar inayoendelea katika jiji laTanga jana eneo kwa minji
picha na Blog ya Super D
Mwakilishi wa Kampuni ya Gapco T LTD Bw. Atanas Jumbe kulia akimkabizi zawadi kwa Mwakilisha wa Ofisa utamaduni wa Mkoa wa Tanga Bi,Tima Koja wakati wa promosheni ya Gapco Relstar inayoendelea katika jiji laTanga jana eneo
picha na
TANGA

Wawakilishi  wa Kampuni ya Gapco wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuingia Tanga kwa ajili ya promosheni ya Gapco relstar Oil

WALTER AISAMBAZA 'DORODORO'







Na Elizabeth John
BAADA ya kutamba na ngoma yake ya ‘Siachi’, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Walter Chilambo ameachia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Dorodoro’.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Walter alisema kazi hiyo kaisambaza hivi karibuni na anaomba mashabiki wake waipokee kwa mikono miwili.

“Naimani kazi hii itafanya vizuri katika tasnia hiyo kwani mashairi yaliyopo ndani yake yamesimama na yanaujumbe kwa jamii,” alisema msanii huyo ambaye ni mshindi wa Bongo Star Search mwaka jana.

Akizungumzia uandaaji wa video ya kazi hiyo pamoja na ile ya ‘Siachi’ kwamb ayupo katika hatua za mwisho na anawaomba mashabiki wake wasichoke kumsubiri.


“Nitatangulia kutoa video ya ‘Siachi’ naimani itakua nzuri kutokan ana maandalizi ya muda mrefu, najua mashabiki wanaisubiri kwa hamu ila nawahaidi ipo karibuni wataiona,” alisema

RECHO ANAAMINI






Na Elizabeth John


MWANADADA anayetamba katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini, Rachel Haule ‘Recho’, ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Niamini’ ambayo imeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Recho alisema, anamshukuru Mungu nyimbo zake zinapokewa vizuri na mashabiki wake, hivyo anajitahidi kukamilisha video ya wimbo huo mwezi ujao ili kuwapa raha mashabiki wake.

“Muziki ni sehemu yangu ya kazi na sipendi mtu aidharau kazi yangu na sipendi kuwaudhi mashabiki wangu, ili kuepukana na hili nimeamua niwe natoa nyimbo ambazo zimeenda shule ili nisiwachoshe wapenzi wangu,” alisema Recho.

Recho, aliwaomba mashabiki wake wasikae mbali na yeye, kwani kuna vitu vingi amewaandalia ambavyo anaamini vitakuwa ni burudani kwao.

MBASPO MABINGWA AIRTEL RISING STARS MBEYA






 Mshambuliaji wa  Msimamo Youth Educator’s,Saimon Kizito (kulia) akipiga mpira huku beki wa Buguruni Youth Center,Mzee Bazil akijaribu kumzuiya katika mashindano ya vijana  U-17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam juzi.
  Mshambuliaji wa  Msimamo Youth Educator’s,Adeus Kizito akijaribu kumpiga chenga  beki wa Buguruni Youth Center,Husein Hamza  katika mashindano ya vijana  U- 17  ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam juz
 Kiungo wa timu ya Buguruni Youth Center,Razak  Abdalah (wapili kulia) akiwania mpira na beki wa Msimamo Youth  Educator’s, Adam Zogombwa (kulia)  katika mashindano ya vijana  U- 17  ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala, kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam, jezi namba tatu ni Mzee Bazil akijiandaa kutoa msaada kwa mwenzake
Kiungo wa  Msimamo Youth Educator’s,Rajabu Mohamed (katikati) akiwania mpira na wachezaji wa Buguruni Youth Center,Karim Matola  (kushoto) na Razak  Abdalah  katika mashindano ya vijana  U- 17  ya Airtel Rising Stars mkoa wa Ilala,kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam,jezi namba tatu ni Mzee Bazil akijiandaa kutoa msaada kwa mwenzake

UFUNGUZI WA MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP DIALOGUE 2013






Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na vijana wa umri wa CPTM 29ers waliohudhuria mkutano wa Smart Partneship Dialogue 2013 wakati wa ufunguzi rasmi wa mkuatno huo unaoshirikisha watu zaidi ya 800 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre jijini Dar es salaam Ijumaa Juni 28, 2013
Rais Kikwete na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakishiriki katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers 
Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakishiriki katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers 
Mjadala ukiendelea
Rais wa Sri Lanka akishiriki mjadala na vijana wa CPTM 29ers
Rais Omar Bongo katika mjadala huo
Kijana akichangia
Vijana wakichangia mjadala

Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano katika mjadala

Kijana akichangia katika mjadala
Rais wa Sri Lanka na Dkt Mihaela Smith wakifuatilia mjadala



Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana
Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana
Rais Kikwete akisalimiana na vijana hao
Wanahabari wa ndani na nje ya nchi wakirekodi tukio hilo la kihistoria
Wageni mbalimbali katika mkutano huo
Ujumbe wa Swaziland
Ujumbe wa Tanzania
Meza kuu
Meza kuu
Vijana nwa THT wakitumbuiza


Viongozi mbalimbali
THT wakitumbuiza
Meza kuu wakifurahia onesho la THT
Wanafunzi wakiimba kwa furaha

Meza kuu wakishangilia
Sehemu ya wageni
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...