Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 19, 2013

BAKWATA v/s ISTIQAAMA ZATOKA SARE, SHEIKH MKUU WA MKOA WA DAR, AL-HAD MUSSA, NYOTA WA MCHEZO


 Mshambuliaji na Nahodha wa timu ya Bakwata, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al-had Mussa Salum (kulia) akimtoka beki wa timu pinzani ya Istiqaama ya Dar es Salaam, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Dar es Salaam Zuu, Kigamboni jijini mwishoni mwa wiki iliyopita. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
 Kamanda kwa Polisi wa Kanda maalum, Suleiman Kova, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa mchezo huo mwishoni mwa wiki.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, akimkabidhi Jezi, Nahodha wa timu ya Bakwata, Sheikh Al-had Mussa, wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Katikati ni Nahodha wa timu ya Istiqaama, Saleh Omar Saleh.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, akimkabidhi Jezi, Nahodha wa timu ya Istiqaama, Saleh Omar Saleh, wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Kushoto ni Nahodha wa timu ya Bakwata,  Sheikh Al-had Mussa,
 Sheikh Al-had Mussa, akionyesha umahiri wake wa kuchezea soka.
 Kikoso cha timu ya Bakwata

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...