Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 22, 2013

WAWILI WAKAMATWA KUFUATIA TUKIO LA KUVAMIWA MBUNGE WA KASULUACP-David Misime
Mnamo tarehe 20/06/2013 majira ya 19.00 hrs maeneo ya Area ‘E’ Manispaa ya Dodoma Mheshimiwa MOSES S/O MACHALI, miaka 31, Muha, Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia NCCR – Mageuzi wakati anaelekea nyumbani kwake anakoishi njiani alikutana na vijana wanne (4) walikouwa amesimama katikati ya barabara akapiga honi lakini hawakupisha. Aliamua kuwauliza “Jamani mnasimama katikati ya barabara si nitawagonga?” 
Nao wakamjibu: “Wewe si unajifanya motto wa Mbunge, tutakupiga sasa”.

Alipojaribu kupita walipiga gari lake. Ilimbidi ashuke ili atazame kama gari hilo limepata uharibifu. Ndipo vijana hao wakaanza kumshambulia kwa ngumi na mateke huku naye akijitahidi kujihami, ndipo wakatokea vijana wawili (2) na kumsaidia. Kijana mmoja kati ya waliokuwa wanamshambulia Mheshimiwa Machali ‘alimng’ata’ mgongoni kijana aliyekuwa anamsaidia Mheshimiwa Mbunge.

Watuhumiwa baada ya kuona wamezidiwa nguvu walitimua mbio. Mheshimiwa Machali aligundua kuwa simu yake ya mkononi wameondoka nayo.
Msako mkali ulifanyika na usiku wa manane watuhumiwa wawili (2) walikamatwa ambao ni:-

1.         JEREMIA S/O LAWRENT MKUDE@ JERRY, Miaka 18, Mkaguru, Mkulima, Mkazi wa Chaduru, Manispaa ya Dodoma. Huyu amekutwa akiwa na jeraha usoni alilopata wakati anapambana na Mheshimiwa Mbunge na vijana waliokuwa wanamsaidia.
2.         CHARLES S/O CHIKUMBILI, Miaka 22, Mkulima, Mkazi wa Swaswa, Manispaa ya Dodoma.
Watuhumiwa walipokamatwa usiku huo wa manane wamekutwa na misokoto miwili (2) ya bhangi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...