Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, February 28, 2013

MICHUANO YA MPINGA CUP YAANZA RASMI LEO


 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akidaka mpira ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup inayowahusisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodabado inayoanza rasmi leo kwa muda wa wiki moja. Mpinga cup imedhaminiwa na  Airtel , Rotary Club, Mr price na Shoprite  ikiwa na lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki na kupunguza ajali barabarani . akishuhudia kushoto ni  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akikagua timu wakati wa uzinduzi wa  michuano ya Mpinga Cup inayowahusisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodabado inayoanza rasmi leo kwa muda wa wiki moja. Michuano hii imeanza rasmi kwa mechi kati ya Kawe Tiptop na Manzese anayefata pichani ni Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga
 kikosi cha timu ya Manzese  katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mpinga Cup yaliyofanyika leo katika viwanja vya polisi oyesterbay , katikati pichani ni Kanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Saalam Suleiman Kova akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga
 kikosi cha timu ya Kawe Tiptop katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mpinga Cup yaliyofanyika leo katika viwanja vya polisi oyesterbay , katikati pichani ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga
 Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akikagua timu kabla ya mechi kati ya  Kawe Tiptop na Manzese leo wakati wa uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup, anayefata pichani ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando
Kanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Saalam Suleiman Kova akijiandaa kudaka mpira ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup inayowahusisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodabado inayoanza rasmi leo kwa muda wa wiki moja. Mpinga cup imedhaminiwa na  Airtel , Rotary Club, Mr price na Shoprite  ikiwa na lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki na kupunguza ajali barabarani . akishuhudia kushoto ni  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga

WATANZANIA WATAKIWA KUWEKA TOFAUTI ZAO MBALI NA KUISHANGILIA SIMBA WAKATI WA MECHI YA MARUDIANO NA LIBOLO YA ANGOLA


 
Watanzania wametakiwa kuweka tofauti zao mbali na kuishangilia timu ya Simba inapocheza mechi yake ya marudiano na Libolo ya Angola Jumapili hii kuwania kufuzu katika Ligi ya Mabingwa wa Afrika.

Wito huo umetolewa na wadhamini wa Timu ya Simba, Kilimanjaro Premium Lager, kupitia Meneja Masoko Fimbo Butallah wakati wa kutoa vifaa kwa timu ya Simba tayari kwa mechi hiyo kama sehemu ya udhamini.

“Wanapokwenda kwenye mechi hii hawandi tu kama Simba bali wanaenda kuiwakilisha Tanzania kwa hivy0 ni muhimu kwa watanzania wote kuungana na Kilimanjaro Premium Lager kuleta hamasa ili timu yetu iibuke na ushindi na kusogea mbele katika mashindano haya,” alisema.

Alisema wao kama wadhamini wana imani kuwa Simba imejiandaa vizuri na watafanya maajabu na kuibuka na ushindi ugenini.
“Mechi hii ni ngumu lakini tuna imani watafanya vizuri na kuwafurahisha watanzania,” alisema Bw Butallah.

Akipokea vifaa hivyo Msemaji wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga aliishukuru Kilimanjaro Premium Lager kwa udhamini wake mnono ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa klabu yao.

“Zawadi ambayo tunaweza kuwapa wadhamini wetu ni kushinda Jumapili,” alisema Kamwaga.

Alisema watanzania wasiwe na wasiwasi kwani Simba ina uwezo wa kufanya ilichofanya kwa Zamalek miaka kumi iliyopia kwani Zamalek ilishinda Tanzania lakini katika mechi ya marudiano Simba ikashinda.

“Kuna wakati pia Zambia ilitufunga mabao manne nyumbani lakini tulivyoenda kwa tukawafunga matano,” alisema Kamwaga.
Simba inatarajiwa kuondoka Ijumaa alfajiri kuelekea Angola tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa Jumapili.

Kilimanjaro Premium Lager ni mdhamini wa timu za Simba na Yanga na Timu ya Taifa (Taifa Stars).

NADHIPA WA ISIDINGO AANZA SAFARI YA KUELEKEA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO LEO 
 
 
 
 
 
 
 
 
Mwigiizaji maarufu Nadhipa ameanza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro leo asubuhi akiwa na wanawake wengine 10 kwa ajili ya kuhamasisha ukatili dhidi ya wanawake.
 
Katika msafara huo wapo Watanzania Wawili, Ashura Kayupayupa, ambaye ni mwanaharakati dhidi ya ndoa za mapema na Mwalimu Anna Philipo ambaye ni Mwanaharakati dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia kutoka katika jamii ya Wahadzabe.

Kutoka Nepal ni Shailee Basnet, Pujan Acharya, Nimdoma Sherpa, Pema Diki Sherpa, Chunu Shretha, Asha Kumari Singh na Maya Gurang, pamoja na wapiga picha wawili James Gimbrone na Russ Paraseau

MAPACHA WATATU KUZINDUA YARABI NAFSI MARCH 2


Waimbaji wa bendi ya Mapacha watatu Khalidi Chokolaa (kushoto) na Jose Mara wakiwa wameshika CD ya albam yao mpya  Dar es salaam jana watakayoizindua March 2 katika ukumbi wa bussines park.(Picha na www.burudan.blogspot.com
Meneja wa bendi ya Mapacha Watatu akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wao (Picha na www.burudan.blogspot.com
Msanii wa bendi ya mapacha watatu Catherine Fidelic ' Cindy' akiimba mbele ya wana habari

Wednesday, February 27, 2013

WANA CCM KATA YA JANGWANI WAFANYA MKUTANO WA KWANZA

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Jangwani Mohamed Bawaziri (kulia) akipiga makofi  ya furaha na Mjumbe wa alimashahuli kuu ya CCM, Rameshi Patel wakati wa kumkaribisha kufungua mkutano wao wa kwanza wa kata hiyo Dar es salaam  tangia wachaguliwe kushoto ni mwanachama Said Side

Mjumbe wa alimashahuli kuu ya CCM, Rameshi Patel katikati naMwenyekiti wa CCM Kata ya Jangwani Mohamed Bawaziri

Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa kata ya Jangwani wakipiga vigeregere, Dar es salaam jana  wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza tangia wachaguliwe viongozi wa kata hiyo.

MFALME WA SAUDI ARABIA ATEMBELEA BENKI YA EXIM


 Mtoto wa Mfalme wa Saudi Arabia Amr Al Faisal (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Dinesh Arora (kushoto) wakati alipotembelea makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam Jana. Kati kati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant . (Na Mpiga Picha Wetu)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant (kushoto) akijadiliana jambo na Mtoto wa Mfalme wa Saudi Arabia Amr Al Faisal (kulia) alietembelea makao makuu ya benki hiyo jana. Kati kati ni Balozi wa Sudan nchini Tanzania Dr. Yassir Ali.

MILIONI 105 ZATUMIKA KUKARABATI JENGO LA HOSPITALIMkuu wa Wilaya ya Iringa akizundua Jengo la Utoaji wa Huduma ya Macho katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (Picha zote na Denis Mlowe)
 Mkuu wa wilaya akiwa katika picha ya pamoja na madaktari na wahudumu wa hospitali ya rufaa |wa mkoa wa Iringa.
Na Denis Mlowe, Iringa
JUMLA ya shilingi Milioni 105 zatumika katika ukarabati wa Jengo la Huduma ya upasuaji wa Macho na kati ya hizo milioni 35 zitatumika kwa gharama ya kununulia vifaa vya tiba ya macho katika hospitali ya rufaa ya Iringa.
Mkuu wa Wilaya kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk. Leticia Warioba alisema hayo wakati akizungumza na wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa uzinduzi wa Jengo la Huduma ya Upasuaji wa Macho na pamoja na Kituo cha Huduma ya Upimaji na kutengeneza miwani katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa  kwa udhamini wa mashirika ya Sightsaver na Brien Holder Vision kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Walioba alisema kwamba watumishi wa idara ya afya hususani upande wa macho kuzingatia kwamba wanatumia msaada huo kwa malengo yaliyokusudiwa kwa manufaa ya wananchi na kuwataka wasimamizi wa huduma za afya hospitalini hapo kuhakikisha kuwa vifaa vyote vilivyotolewa na wadau kuingizwa katika leja ya Hosptali ya Mkoa.
“Vile vile vifaa hivi vitunzwe kwa kufanyiwa matengenezo na kinga kama inavyotakiwa ili viweze kutoa huduma kwa muda mrefu” alisema dk. Warioba na kuongeza kwamba “Ushirikiano ambao mashirika haya yameonyesha katika kuboresha huduma za afya ya macho ni mfano wa kuigwa na wadau wengine wa sekta za huduma za jamii”
Awali mratibu wa huduma ya macho katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa Dk. George Kabona alisema kwamba lengo la mradi huo ni kuhakikisha watu wote wenye upofu unaozuilika wanapata huduma na wale wenye upofu usiozuilika hasa watoto wanapata elimu bora kuhusu huduma za macho.
Alisema kwamba jumla ya watu 725 waliokumbwa na mtoto wa jicho walifanikiwa kufanyiwa operesheni toka mwaka 2009 hadi 2011 na opereshi  zote walifanyiwa watu 1265 kati ya wagonjwa 22,169 waliojitokeza ndani ya miaka mitatu ya 2009/2010/2011 aliongeza kusema kuwa mradi huo umewezesha kuwajengea uwezo watoa huduma wa macho mbalimbali ndani ya mkoa ikiwemo madaktari watatu wa upasuaji wa mtoto wa jicho ambao wawili wanatoa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
“Mradi umeweza kutoa elimu kwa wahudumu wengi wa afya ya msingi katika zahanati zetu ili waweze kutoa hudma nzuri za macho hasa maeneo ya vijijini ambako wataalam wa macho hawapatikaniki” alisema Dk. Kabona 
Mradi Jumuishi wa Huduma za macho mkoani Iringa ulianzishwa mwaka 1998 kwa kushirikiana kati ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa chini ya Katibu Tawala wa Mkoa na Shirika lisilo la kiserikali la Sightsaver.

Tamasha la Pasaka kuvuruga Dar hadi Musoma kwa siku 10 Na Elizabeth John
TAMASHA la Pasaka mwaka huu linatarajiwa kufanyika kwa siku nane mfululizo kuanzia Machi 31 hadi Aprili 7 katika mkoa saba, ikiwa ni mara ya kwanza tamasha hilo kufanyika mikoa zaidi ya mitatu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha hilo la kimataifa, Alex Msama, wamefanya hivyo kwa kuheshimu maoni ya wapenzi, mashabiki na wadau wa muziki wa injili, ambao kwa kuguswa na tamasha hilo, wameomba kufikiwa ili kuzoa baraka za Mungu ambazo huambatana na ujumbe wa nyimbo mbalimbali kutoka kwa waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania.

Msama alisema kuwa, maadamu kamati yake imeridhia maombi ya kuongeza idadi ya mikoa, wanawasihi wapenzi, mashabiki na wadau wa muziki wa injili katika mikoa ambayo Tamsha litafika, kujitokeza kwa wingi kujionea na kuchota baraka za Mungu kupitia ujumbe wa nyimbo na hakuna atakayejutia muda wake wa kwenda kulishuhudia.

Mikoa rasmi iliyoshinda katika kivumbi cha uwenyeji wa tamasha hilo ni Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Mbeya, Mwanza na Mara, ambayo imepatikana baada ya wapenzi, mashabiki na wadau kupiga kura kwa njia ya simu na kilichobaki sasa ni Kamati ya maandalizi kutimiza ahadi yake ya kuwapelekea uhondo huo wa muziki wa injili.

Msama alifafanua kuwa, baada ya Tamasha hilo kuzinduliwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Machi 31, siku itakayofuata litakuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya kabla ya kutua Uwanja wa Samora, Iringa Aprili 3 na Aprili 6, itakuwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma na siku itakayofuata kishindo cha tamasha hilo kitatua CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Alisema baada ya kuvuruka kwenye mikoa hiyo, tamasha hilo litaelekea Musoma na Tarime kwa ajili ya kuhitimisha tamasha hilo ambalo limezidi kupata umaarufu mkubwa kutokana na maudhui yake, ambako safari hii limebeba ujumbe wa kuhamasisha suala la Amani na Upendo kwa watu wote bila kujali kabila, dini wala itikadi

RAIS KIKWETE AKAGUA UKUMBI WA KISASA WA MIKUTANO WA KIMATAIFA JIJINI DAR ES SALAAMRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi  mkubwa wa mikutano multi-purpose conference Hall' uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam. Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi. Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali (picha na Freddy Maro)

ANNA BAYI ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA CHANETAMwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Anna Bayi ametangaza rasmi kuwa hatagombea tena ili kutetea nafasi yake wakati wa uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika Machi 23 mjini Dodoma.

Bayi amesema kuwa ameamua kung’atuka ili kutoa nafasi kwa Watanzania wengine wenye sifa kujitokeza na kuongoza chama hicho kwa matarajio ya kuleta mawazo mapya na kuendeleza mchezo huo nchini.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa muda aliotumia kukaa madarakani unatosha kwake na kwamba, anaamini kuwa akishirikiana na wenzake, amesaidia kuipa Chaneta mafanikio makubwa, yakiwamo ya kuipeleka timu ya taifa kushiriki michuano kadhaa ya kimataifa.

"Nimeamua kutogombea tena ili kutoa nafasi kwa wadau wengine kuendeleza gurudumu la netiboli nchini," Bayi.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chaneta, Rose Mkisi, aliwasihi watu wenye sifa kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania uongozi katika chama chao.

Mkisi amesema kuwa tangu watangaze tarehe ya kutoa fomu hizo, hakuna mgombea yeyote aliyejitokeza kuchukua fomu hadi sasa, isipokuwa wamepokea taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa baadhi ya wanamichezo kutoka mikoani kuwa wanahitaji fomu za kuwania ujumbe.

"Tunaomba wanamichezo wenye sifa wachangamkie fursa hii ya kuchukua fomu za kuwania uongozi," Mkisi, akiongeza kuwa tarehe ya mwisho ya kurejesha fomu hizo ni Machi 15 na usaili utafanyika Dodoma Machi 21.

Nafasi zitakazowaniwa katika uchaguzi huo ni pamoja na za mwenyekiti, katibu mkuu, mweka hazina na wajumbe.

Katika hatua nyingine, Chaneta imetaka mikoa kulipa ada ya uanachama kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu kufika

Mkisi amesema mikoa itakayoshindwa kulipia ada ya uanachama haitaruhusiwa kutoa wawakilishi wa kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu.

Awali, uchaguzi wa Chaneta ulikuwa ukipigwa kalenda mara kadhaa kutokana na baadhi ya mikoa kusuasua kuitisha chaguzi zake na pia, baadhi yao kushindwa kulipia ada za uanachama

BOHARI YA DAWA (MSD) YATINGA NA VIFAA TIBA MAONESHO YA WADAU WA AFYA KUSINI MWA AFRIKA


 Ofisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD),Florida Sianga (kulia)) akiwaelekeza Monica Gofrey (kushoto) na Geofrey Kandi kifaa tiba aina ya sterilizer inayotumia gesi katika maonesho ya Shirikisho la Wadau wa Huduma za Afya Kusini Mwa Afrika, leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. (PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
                                              Wageni hao wakiendelea kupata maelezo
 Kitanda cha wagonjwa ambacho ni baadhi ya vifaa tiba vinavouzwa na MSD
                                              Kifaa Tiba aina ya kitasishaji 'Starilizer' inayotumia gesi
                                                                 Kitanda cha kujifungulia
 Kabati la kusambazia dawa wodini 'Dispensing Trolley'
                                           Banda la MSD linavyoonekana kwenye maonesho hayo


JK ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JKT MLALAKUWA Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na  uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na kada mbalimbali za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea leo February 27, 2013

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye uwanja wa sherehe
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia wapo. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya saa toka kwa  Mkuu  wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga huku  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia makamanda wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...