Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, February 26, 2013

BLOG YA KAMANDA WA MATUKIO YAPATA TUZO KATIKA KONGAMANO LA NHIF


Mmiliki wa Blog ya Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda akionesha tuzo ya cheti aliyopatiwa na Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kwa kutambua mchango wake katika masuala ya mfuko huo, wakati wa Kongamano la NHIF na Wanahabari la kujadili tafiti zilizofanywa na wanahabari katika halmashauri 26 nchini kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajili ya Afya. Kongamano hilo lililoshirikisha wanahabari 150  lilimalizika mwishoni mwa wiki Mjini Mtwara.
Mkuu wa Wilaya ya Kalmbo, Moshi Chang'a (katikati) akimkabidhi tuzo hiyo Mmiliki wa Blog ya Kamanda wa Matukio, Kamanda Richard Mwaikenda. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba.
Mmiliki wa Blog ya Kamanda wa Matukio, Kamanda Richard Mwaikenda (katikati), akiwa na wanahabari wenzie wakati wa Kongamano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Benjamini Mkapa katika Chuo cya Ualimu Mtwara, mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni; Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile, Mtangazaji wa Televisheni ya ITV Mara, George Marato, Mtangazaji wa ITV, Dar es Salaam, Godfrey Monyo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...