Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, February 23, 2013

BAADA YA SHOW ZA DIAMOND KUBUMA, SASA DIAMOND ATUHUMIWA KUTAPELI WARWANDA MILIONI 9

Hivi karibuni msanii wa nchini Rwanda aitwaye Mico the Best amejikuta akiingia hasara kubwa baada ya kumlipa Diamond aliyemshirikisha kwenye wimbo wake uitwao SINAKWIBAGIWE kwaajili ya show nchini Rwanda lakini hitmaker huyo wa ‘Nataka Kulewa’ alishindwa kwenda. Show hiyo ilikuwa ifanyike kwenye mji uitwayo Remela, nje kidogo ya Kigali.

Baada ya hapo Mico amekuwa akiongea na vyombo mbalimbali vya nchini Rwanda na Tanzania akitaka apewe haki yake.
Anasema alimlipa Diamond dola 6,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 9 pamoja na nauli ya ndege ya watu wanne.


Mico NA DIAMOND

“Diamond amenidharau mimi na amewadharau wanyarwanda wote waliokuja kumuona,” Mico aliiambia website ya Rwanda inyarwanda.com.MATANGAZO YALIYOBANDIKWA SEHEMU MBALIMBALI NCHINI RWANDA KAMA PROMO

Amesema anataka kuzungumza na Diamond ili amrudishie fedha yake baada ya kumsababishia hasara kubwa na ameomba msaada kwenye balozi za Rwanda na Tanzania.

Haya ni maoni ya mashabiki wa Rwanda walioandika kwenye page yetu ya Facebook:

Ibrahim Kg B-raz

Diamond amezalau wa nyarwanda kwa show yenye ingelikuwa jumatano iliyo pita…msani Mico anaumiya sana na machozi ya ma millioni zilizo panwa kwa makubaliano katika hao wasani…sasa leo hii manager Lingo wa DiamonD anajulisha kwamba hakujuwa show hiyo….kilio Kigali kutoka kwa mafans paka leo hata msani Mico muenyewe wanadayi!!!!!!!

Blue Saidoz Akaga

Huku rwanda msanii Diamond amezinguwa kabisa! Ka kula pesa za advance za msanii Mico the best wahapa rwanda sawa na 6000$ wakakubaliana kwamba atakuja katika launch ya msanii huyo Kigali tarehe 16.Feb.2013 then akaenda zake arusha, Sio ungwana kabisa.

Gnl Patrick

Diamond kadanganya wanyarwanda wote ametukoseyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...