Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, November 30, 2010

TBS WAWAPA SOMO WAUZA MIKATE NA BIDHAA ZA MAINDI


Baadhi ya washiliki wa Kongamano la watu wanaotengeneza mikate,mafuta,na bidhaa za maindi wakiwa katika kongamano hilo lililoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dar es salaam

TANGAZO LA DAWA YENYE NGUVU


DAWA YA NGUVU ZA KIUME NA MSIMKO KWA WANAWAKE WASIO NA HAMU YA TENDO LA NDOA AMBAYO HULETA MSISIMKO KWA WANAUME NA WAKE WAKUTANAPO.KWA SASA INAPATIKANA KWA BEI NAFUU HAPA JIJINI DAR ES SALAAM MAKUTANO YA MTAA WA KIPATA NA BARABARA YA MSIMBAZI

KWA MAELEZO ZAIDI TEMBELEA http://enzoy.org/index.php?lang=EN

PIGA NO O713827689, 0755074505 , au 0719 541366

KARIAKOO SOKONI LANGO KUU ULIZA LUKINDO 0755686929

BUGURUNI LOZANA STENDI YA TAX ULIZIA ADAMU KIBANDANI 0755875884


KARIAKOO SHULE YA UHURU STENDI YA MABASI YA TANDIKA ULIZIA ZUNGU MUHUZA TIKETI 0712743870


GONGOLAMBOTO GRAD'S BAR ULIZA MAPUNJA 0713388956

ULIZIA FUNDI MITAMBO ALLI MOMBA POPOTE ALIPO 0715260220

NA UKIWA ILALA SHARIF SHAMBA FIKA DSJ BANDA NAMBA 14 SIMU 0718718671

NA UKIWA KOTA ZA BANDARI KARIAKOO FIKA MKUNGUNI KIBANDANI KWA HUSEIN 0753893295

MWANANYAMALA FIKA JABA KLABU ULIZA MACHELLAH 0713470492

Monday, November 29, 2010

ngumi mawe masumbwi yanaendelea

bondia Mohamedi Matumla kulia akitwangana na Edward Luanda katika mpambano wao matumla alishinda kwa pointi
mohamed matumla vs edwrd luanda
mashabiki
mabondia Shabani Madilu kushoto akipambana na Alfa George madilu alishinda pambano hilo kwa point
Kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti ya Ilala Dar es salaam Rajabu Mhamila Super D akifatilia mpambano katika kusaka vipaji vipya vya mchezo huo
Alfa George vs Shabani Madilu

SEND OFF PARTY YA Rehema Mkongo

bibi akitoa nasaha kwa mjukuu wake
Rehema Mkongo akimnywesha kinywaji mume wake Abas Mbonga
Mariamu Kimaya akiwa na mpambe wake Rehema Mkongo
Rehema Mkongo akimlisha mume wake Abas Mbonga
maarus wakingia ukumbini kwa mbwembwe
maarusi wakiwa salon
kamati ya maandalizi
Fatuma Likwata shoga wa bi arusi alikuwepo kumpa kampani

mzee makasy amtembelea kamanda gurumo muhimbili leo

mwanamziki wa siku nyingi mzee makasy akimjulia hali mwenzie muhidini gurumo (KAMANDA) alielazwa hospital ya taifa muhimbili gurumo yupo mwaisera wodi namba moja baada ya kutoka katika chumba cha wagojwa wenye uangalizi maalumu (ICU)


Saturday, November 27, 2010

KOCHA WA NGUMI AKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO


MDAU WA MICHEZO AMKABIDHI VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI KOCHA RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KWA AJILI YA KUENDELEZA MCHEZO HUO KWA VIJANA WASIO NA VILABU NCHINI.


Kampuni ya IRO & STEEL LTD, ALTAF& CO.PK inayojishughurisha na utengenezaji wa vyuma leo imemkabidhi kocha na mdau maarufu wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' vifaa michezo vyenye thamani ya laki tatu na hushee kwa ajili ya kuuendeleza mchezo wa ngumi.

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam leo wakati wa hafla hiyo, Mdau binafsi na Engeneer wa kampuni hiyo, Zulfiqal Ali alisema wameamua kutoa vifaa hivyo ili kuuendeleza mchezo wa ngumi kwa vijana hasa wa kujitegemea na kuunga mkono jitihada za Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza michezo. .

Vifaa hivyo ni Groves pea nane, fulana mia sita za kufanyia mazoezi , pamoja na kamba nne za kuruka wakati wa kufanya mazoezi

Alisema kutokana na idadi kubwa ya vijana kupenda mchezo huo na kukabiliwa na tatizo la vifaa, mdau huyo ameona aweze kumsaidia kwa kumpatia vifaa kocha huyo ambaye anatoa mafunzo kwa mabondia wa kujitegemea katika ufukwe wa Coco Beach siku za Jumamosi na Jumapili.


"Baada ya kuwa nimeona juhudi za Mhamila 'Super D' ambaye siku za nyuma alikuwa bondia hapa nchini na alizichezea timu mbalimbali nimeamua kumwongezea nguvu ili aweze kufanya kazi hii kwa mafanikio lakini pia hapa tunaunga mkono juhudi za Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete katika kuthamini na kuendeleza mchezo hapa nchini,." alisema Zulfiqal.

MDAU WA MICHEZO AMKABIDHI VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI KOCHA RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KWA AJILI YA KUENDELEZA MCHEZO HUO KWA VIJANA WASIO NA VILABU

Kocha wa Ashanti Boxing Rajabu Mhamila Super D (kulia) akikabidhiwa vifaa vya mchezo huo na Mkurugenzi wa Kampuni ya IRO&STEEL LTD Zulfiqar Ally wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo kwa ajili ya vijana wasio na vilabu nchini. wanaoshuhudia kushoto ni Bakari Gobe,Ally Raza na Kashif Ally kutoka

Kocha wa Ashanti Boxing Rajabu Mhamila Super D (kulia) akijaribu kuzichapa na Mfadhili aliyemfadhili vifaa vya mchezo huo Zulfiqar Ally wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo kwa ajili ya vijana wasio na vilabu nchini. wanaoshuhudia kushoto ni Bakari Gobe,Ally Raza na Kashif Ally kutoka Kampuni ya IRO&STEEL LTD ambayo Mkurugenzi wake ni Zulfiqar


Super D,Bakari Gobe,Zulfiqar Ally,Ally Raza na Kashif Ally wakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano



MAAFALI YA 10 YA CHUO CHA ROYAL COLLEGE

Rajabu Mhamila Super d akiwapa sapoti waitimu Innocent Melleck na Joyce Macha
Innocent Melleck akitunikiwa shaada yake na Henry Muhanika ambaye alikuwa mgeni rasmi
Innocent Melleck akipeana mkono na Henry Muhanika ambaye alikuwa mgeni rasmi

Msanii Boaz Zile alikuwa akitumbuiza katika mahafali hayo

Innocent Melleck
Innocent Melleck akitafakali kabla ya kutunukiwa cheti

Innocent Melleck akisoma lisala mbele ya mgeni rasni

Friday, November 26, 2010

MZEE GURUMO ALAZWA MUHIMBILI

Mzee Gurumo aka Kamanda kiongozi wa bendi ya msondo ngoma amelazwa ktk hospitali ya taifa ya muhimbili MNH wodi ya Mwaisela no 5 akisumbuliwa na ugonjwa wa Mapafu kujaa maji, nyepesi zilizopatikana zinasema kwa sasa anapumua kwa msaada wa mashine ya gesi

Wadau na wapenzi wa burudan na watu wote kwa ujumla naomba tumuombee kheri mzee wetu apone haraka!

MAONESHO YA BADHAA ZA MIKONO YAZINDULIWA COCO BEACH LEO


Sisi wanachama wa TanCraft na NASME/WEEC tunayofuraha sana kwa siku hii ya leo kwa kuitikia mwaliko wetu kujumuika nasi ili kufanikisha tukio la leo la ufunguzi wa maonyesho ya 5 ya kazi za mikono. Mheshimiwa Katibu Mkuu

Katika maonyesho haya tunao wanaonyeshaji toka Tanzania ----Malawi --- na Kenya ---- katika sekta zifuatazo:







1. Vikapu

2. Ufinyazi

3.Bidhaa za Ngozi

4. Uchongaji wa Vinyago

5. Nguo na Ushonaji

6. Uchoraji na Picha

7. Usindikaji wa Vyakula

8. Watoa huduma mbalimali


Kauli mbiu yetu ni

NJOO, ANGALIA NA NUNUA BIDHAA ZA ZILIZOTENGENEZWA TANZANIA NA MALAWI.


  1. UTANGULIZI:

Trade Facilitation Office (TFOC) ya Canada wakishirikiana na Bodi ya Biashara ya Nje (BET) pamoja na Shirikia la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) waliandaa na kuratibu tukio la uendelezaji wa masoko ya kazi za mikono hapa Tanzania. Bidhaa ziliandaliwa na maonyesho ya kazi za mikono yalifanyika katika viwanja vya maonyesho vya Sabasaba mwezi April 2006 na yalifunguliwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa wakati huo

Wakati huo ndipo (TanCraft) ikaanzishwa mwezi April 2006. Shughuli za usajili rasmi kisheria zilifanyika mnamo Mwezi August 2006 chama kilipata Cheti cha usajili no.SO. 14470 kilichotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  1. KAZI ILIYOFANYIKA:

Mheshimiwa Katibu Mkuu


Katika majukumu ambayo tuliyapa kipaumbele ni:

  1. Kuandaa Kitabu cha orodha ya wazalishaji wa kazi za mikono hapa Tanzania kwa kusaidiana Trade Facilitation Office of Canada 2007

  2. Kuandaa maonyesho ya Kwanza ya TanCraft ambayo yalifanyika katika Viwanja vya Karimjee 2007

  3. Kuandaa Maonyesho ya Pili yaliofanyika nchini Malawi mwaka 2008 kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi

  4. Kuandaa maonyesho ya Tatu yaliofanyika tena nchini Malawi kwa kushirikiana na NASME chama ambacho kinashughulika na wajasiriamali wadogo nchini pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi 2009

  5. Kuanda semina mbalimbali zinazohusu ujasiriamali 2009, 2010

  6. Kuandaa maonyesho mengine makubwa nchini Malawi kwa kushirikiana na wenzetu NASME/WEEC ya Malawi mjini Lilongwe kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi enzi za Mh. Balozi Mstaafu Rashid Makame.

  7. Kuandaa semina mbalimbali za kuimarisha wanachama kwenye biashara zao ili waweze kuongeza tija na pia kiwango cha uzalishaji bidhaa bora.

  8. Kuandaa semina za Ukimwi mahali biashara na kazi.


1.1 MALENGO YA CHAMA:

1.1.1 Kuendeleza sekta ya kazi za mikono kwa kuhamasisha miradi mbalimbali yenye lengo la kuunganisha sekta nzima na kutumia raslimali, ujuzi na utaalamu mbali mbali uliopo katika sekta ya kazi za mikono na sekta zinazohusiana;


1.1.2 Kutambua matatizo yaliyomo katika sekta ya kazi za mikono ambayo yanazuia kukua kwa sekta na kushiriki katika kutatua.


      1. Kuwasaidia wanachama wake ili waweze kupata misaada inayohitajiwa kwa ajili ya masoko ya nje ya nchi pamoja na upatikanaji wa mali ghafi


      1. Kuandaa mazingira na kujenga uwezo wa kubadilishana taarifa na uzoefu kati ya wazalishaji wa kazi za mikono pamoja na wafanyabiashara wa sekta ya kazi za mikono kwa upande mmoja na kushirikiana na mashiriki ya serikali ili kupata matokeo mazuri katika matumizi ya rasilimali zilizopo pasipo kusababisha uharibifu wa mazingira;


      1. Kushirikiana na mashirika ya hapa nchini na ya kimataifa katika kuhamasisha biashara kati ya nchi zinazoendelea na zilizoendelea ili kupata msaada na ushirikiano ambao utaleta manufaa kwa chama na wanachama wake.


  1. CHANGAMOTO, MAHITAJI NA MAPENDEKEZO:

  1. Eneo/sehemu ya pamoja ya kuendeshea shughuli zetu za kila siku ; Kwa vile TanCraft ni asasi inayounganisha Watanzania wote; imethibitika kuwa na wasanii ni wengi kiasi cha kulazimika kuwa na eneo maalum la kuuzia na hata kuzalishia

TANCRAFT inaomba ipewe jengo au sehemu katika mikoa inayotembelewa na watalii wengi kama vile Arusha,na DSM kule TRIDO. Hili ltaisaidia sana Tancraft kwani tukiwa na eneo moja la uzalishaji tutakuwa na ubora wa hali ya juu na unaofanana kwa ajili ya soko kubwa na hilo litaongeza kipato kwa wasanii na kuongeza ajira.


  1. Mhe. Katibu Mkuu

TanCraft kwa kuona kuwa kuna haja ya kushirikiana na nchi za Jirani kama Malawi tuliamua kwenye Maonyesho yaliopita kule Lilongwe kwamba kila mwaka mara moja maonyesho yatafanyika katika nchi ya Tanzania naMalawi, ndio maana leo hii tuko na wajasiriamali kutoka Malawi kutimiza makubaliano yetu.

Tumealika wenzetu kutoka Kenya ili tuweze kuwa nao pamoja katika soko hili la Kusini mwa Afrika ambapo baadae tunataka kuwashirikisha Zambia, Botswana na Zimbambwe tuwe pamoja katika kuondoa umaskini katika jamii yetu.


  1. MIPANGO YA BAADAYE:

  • Kuziwezesha na kuziboresha bidhaa za sanaa za mikono Tanzania

  • Kufanya kazi kwa karibu zaidi na serikali yetu ili kuhakikisha nchi yetu inakuwa na chuo maalumu cha ufundishaji na udumishaji wa sanaa za mikono .


  1. Kujenga nafasi kati ya wazalishaji wa kazi za mikono ili wajue umuhimu na nguvu ya kuwa na huduma za masoko ambazo ni endelevu.


8. Wenye kutoa huduma mablimbali


  1. SHUKURANI:

Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wafuatao ambao wamesaidia mno kuifikisha TanCraft hapa ilipo leo.

  1. Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko,

Wizara imekuwa ikiwateua maofisa wao kutusaidia katika maandalizi na pia hata kufuatana nasi katika maonyesho huko Malawi ili kuhakikisha kazi inafanyika kwa kiwango cha Juu.


  1. Ubalozi wa Tanzania kule Malawi, Ubalozi wetu umekuwa ukituunganisha na serikali ya Malawi na Wajasiriamali kila tunapohitaji msaada wao ingekuwa ni vigumu sana kama wasingeonyesha juhudi hii kuanzia mwanzo hasa mwaka 2008 hadi leo 2010

  2. Ubalozi wa Malawi nchini Tanzania kwa kushirikiana nasi katika maandalizi ya aina zote na pia kuwa kiungo kikubwa cha mawasiliano kati yetu na wenzetu wa Malawi.

  3. Wafadhili wetu hapa Tanzania Matching Grant Program chini ya ( TPSF) kwa kuwawezesha wajasiriamali kushiriki maonyeshomabalimbali semina,utafit wabidhaa hapa ndani ya nchi na nje wa masoko,kujiendeleza katika somo la kiingereza nk.

  4. Mmiliki wa CoCo Beach kwa kutupa eneo la kuonyeshea biashara zetu kwa na pia kushirikiana nasi katika maandalizi yote bila kuchoka.

  5. Jeshi la Polisi Mkoa wa DSMi kwa kushirikiana nasi katika kuhakikisha Usalama wa Raia na mali zao

  1. Tunapenda kuwashukuru wote waliotusaidia kwa namna moja au nyingine ili kufanikisha kazi hii na kukiweka chama hapa kilipo hasa wajasiriamali wenyewe kwa kujitoa kuonyesha bidhaa zao kila wanapohitajika, kuhudhuria semina zote zilizoandaliwa na chama na pia

kuchangia gharama zilizotakiwa, na viongozi wenzangu wote kwa kujitoa muda wao na kushiriki katika mikutano yote bila kuchoka.

Mheshimiwa Katibu Mkuu

Tunakukaribisha uweze kusema na Wajasiriamali

KARIBU MHESHIMIWA KATIBU MKUU

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...