Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 4, 2010

TALENT BAND KUZINDUA ALBAM YA KWANZA


BENDI ya muziki wa dansi nchini Talent Band imeanza mazoeziyake kwaaajili ya uzinduzi wa Album yao ya kwanza ijulikanayo kwa jina la Mtoto kutambaa inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi Novemba 25 mwaka huu ukumbi wa Dar West Park Tabata.

Akizungumza jana MKurugenzi wa Bendi hiyo Husein Jumbe amesema vijana wake wamejipanga vema kupagawisha mashabiki wao siku hiyo.

"Nimejiapnga vilivyo ili kuwahakikishia watanzania kuwa uzinduzi huu utakuwa na histolia ya kipekee ambapo hakutotokea mwanamuziki mwingine mwenye uwezo kama nitakao onyesha siku hiyo" alisema Jumbe.

Alisema kuwa Albamu hiyo itajumuisha jumla ya nyimbo sita ambazo zimetungwa na yeye mwenyewe akiwemo na Lyon Simba ambazo ni Subiri kidogo,Ulevi,Dilema,Nyuma ya Pazia,Songo Mbingo,pamoja na Nimeamua kunyamaza.

Hata hivyo Jumbe amewataka wazazi wawahamasishe watoto wao wajitokeze kujiunga na bendi ya Talent badala yake ya kujiunga na makundi yasiyofaa.

Aidha kwa upande mwingine amemshukuru aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Kibaso kwa kununua nyimbo yao moja kwa
Gharama ya Sh 50,000 sambamba na kuwataka wananchi wa Temeke
kuipa ushirikiano wa hali na mali wa kiuchumi ili kuiwezesha
bendi kuboresha shughuli zake za kimuziki.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...