Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 31, 2013

VIJANA WACHANGAMKIA MCHEZO WA BAO
Baadhi ya vijana wanaofanya shughuli zao kando kando ya barabara ya Uhuru Dar es salaam eneo la Malapa  wakicheza mchezo wa bao mchezo huo uliopata umaarufu mkubwa miaka ya nyuma ulikuwa ukuchezwa na wazee pekee rakini kwa sasa vijana wamekuwa wakiufatilia na kuucheza kwa ustad mkubwa kushoto ni Jagani Ndizi na Omari Kijungujiko PICHA NA BLOG YA SUPER D

Aibu! Njemba lafungwa miaka 30 kwa kumlawiti, kumzalisha bintie


Yusufu Amani (39) aliyembaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe Afungwa miaka 30
Hapa akijifunika sipigwe picha baada ya hukumu
Kulia ni mtoto aliyebakwa na baba yake kisha kuzalishwa akiwa na mtoto wake wakitoka mahakamani kulia ni mama mzazi wa binti aliyebakwa na kuzalishwa


MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa akiwa na miaka 15( jina linahifadhiwa).Mwendesha mashitaka wa serikali  Archiles Mulisa  aliiambia mahakamani hiyo Mbele ya Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa Mshtakiwa huyo ni Yusufu Amani (39) anayedaiwa kumbaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe.Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a na 155 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho  mwaka 2002, pamoja na kifungu cha 158(a) cha makosa ya kuzini.


akisoma Hukumu hiyo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mtuhumiwa alianza kujihusisha kimapenzi na mwanaye Mwaka 2008 baada ya kutengana na mkewe ambapo Mtuhumiwa aliachiwa watoto wote.
Aliongeza kuwa wakati huo binti huyo alikuwa na umri wa miaka 12 na alikuwa akisoma shule ya msingi darasa la Tano jambo ambalo wamedumu nalo kwa Miaka mine hadi ilipogundulika kuwa binti alikuwa mjamzito Mei, 2012.
Alisema mbinu aliyokuwa akiitumia ni kumtishia binti asitoe taarifa kwa mtu yoyote na kwamba baada ya kugundulika kuwa na ujauzito alimwambia amsingizie kijana yoyote mtaani kwao.
Hakimu Ndeuruo alisema Mahakama ilimtia hatiani Mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa Mhanga wa tukio hilo ambaye ni binti pamoja na ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa Mkemia mkuu wa Serikali.
Alisema ushahidi wa Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kupima Vinasaba kutoka Mtuhumiwa, Mhanga na Mtoto aliyezaliwa ulidai kuwa  Mshtakiwa ndiye baba halali wa Mtoto kutokana na Maeneo 15 ya vipimo vya Vinasaba kati ya Baba na Mtoto aliyezaliwa kufungana kwa asilimia 99.9.
Aidha kabla ya kutoa hukumu Hakimu alimpa nafasi mtuhumiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu au asiweze kuhukumiwa kabisa lakini hali ikawa tofauti baada ya Mtuhumiwa kujibu kuwa hana la kujitetea vyovyote itakavyokuwa anachotaka ni nakala ya hukumu.
Kutokana na kushindwa kujitetea Hakimu Ndeuruo alimhukumu kwenda jela miaka 30 na kwamba ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu endapo hakuridhika na hukumu hiyo.
Awali katika ushahidi wake Mahakamani hapo Mtuhumiwa huyo alidai kuwa hakutenda kosa hilo bali alitengenezewa na Mkewe ambaye aliapa kumkomesha baada ya kukosana na kumpata mume mwingine jambo ambalo lilipingwa vikali na hakimu na kudai kuwa “ mfa maji haachi kutapatapa”

Na Mbeya yetu

Mabondia wa Tanzania huuza mechi zao Ulaya?


http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2011/11/Rashid-matumla.png
Rashid Matumla 'Snake Man'

Benson Mwakyembe
 

http://www.ibn-tv.com/wp-content/uploads/2012/02/Nyilawila.jpg
Karama Nyilawila aliyetwaa ubingwa wa WBF Ulaya

MABONDIA Mada Maugo na Benson Mwakyembe Jumamosi walipokea vipigo nchini Russia katika mapambano yao ya kimataifa, huku kukiwa na tuhuma kwamba mabondia wengi wa Kitanzania wanaoenda kupigana nje ya nchi 'huuza' mechi zao.
Maugo alipokea kichapo cha TKO ya raundi ya 5 katika pambano la raundi 8 dhidi ya bondia asiye na uzoefu Movsur Yusupov aliyecheza mapambano manne tu kulinganisha na Mtanzania huyo aliyepigana michezo 25.
Mtanzania mwingine, Mwakyembe alidundwa kwa KO ya raundi ya 7 ya pambano lake la raundi 8 dhidi ya bondia mwingine asiye na uzoefu Apti Ustarkhanov, ambaye hilo lilikuwa ni pambano lake la tatu na la pili kushinda tangu aingie kwenye ngumi za kulipwa.
Kina Maugo walipambana dhidi ya wenyeji wao katika mapambano ya uzito wa Super Middle ya raundi nane yaliyofanyika katika ukumbi wa Trade & Entertainment Centre 'Moskva', Kaspiysk chini ya wakala Mkenya Thomas Mutua.
Vipigo vya mabondia hao vimekuja wakati wadau wa ngumi za kulipwa wakihoji sababu zinazofanya mabondia wa Kitanzania kushindwa kutamba kila waendapo nje huku ripoti mbalimbali zikiwatuhumu mabondia wa majuu kuwatumia mabondia kutoka Afrika kupandisha chati zao katika viwango vya ubora kwa kuwanunua wawaachie washinde.
Ripoti za kuuzwa mechi au kuwapo kwa mchezo mchafu ziliwahi kutolewa na baadhi ya mabondia akiwamo Pascal Ndomba na Francis Cheka aliyepokea kichapo cha kushangaza mapema mwaka huu nchini Ujerumani.

Ndomba anayepigana uzito wa juu wa (Cruiserweight), alisema baadhi ya mawakala wa nje hutaka mabondia dhaifu wa kwenda kupigana na mabondia wao ili kupata ushindi kirahisi na kuboresha rekodi zao.
"Hili ndilo linalofanyika, bondia mkali mara chache sana kupelekwa nje na hata akienda basi atahujumiwa ili apoteze mchezo kwa manufaa ya mabondia wanaoenda kupigana nao," Ndomba alisema hivi karibuni.
Naye Cheka alitoa maelezo ya kufanyiwa 'hila' katika pambano lake dhidi ya Uensal Arik aliloongoza kwa raundi sita za mwanzo kabla ya kurushiwa kitaulo katika raundi ya saba na kupoteza mchezo kwa TKO.

Pascal Ndomba
"Sikupoteza pambano lile, ila mwenyeji alibebwa na mwamuzi aliyemaliza pambano kana kwamba nimesalimu amri, ni vigumu mabondia wa Tanzania kushinda nje," alisema Cheka mara alipotua nchini.
Cheka alisema kambi ya mpinzani wake walimfuata hadi hotelini alipofikia kuelekea pambano lao kumshawishi awaachie pambano hilo kwa ahadi ya pesa lakini alipokataa ndipo alipokuja kuhujumiwa ulingoni kwa mtu aliyekuwa upande wa kona yake kurusha taulo ulingoni ilhali alikuwa akiongoza kwa pointi.
Bondia huyo anayeaminika kuwa bora zaidi nchini kwa sasa katika uzito wake, alisema hakuambatana na kocha wake wakati akienda katika pambano hilo hivyo hata kwenye kona yake walikuwa wenyeji wake na ndiyo waliorusha taulo ulingoni.
Hata hivyo, wapo waliomtuhumu kwamba huenda Cheka alicheza 'dili' na wakala wa pambano hilo ili kutotibua rekodi ya mpinzani wake ambaye alikuwa amepoteza pambano moja tu ya 18 aliyokuwa amecheza.
NIPASHE ilizungumza na Marais wa Mashirikisho ya Ngumi za Kulipwa Tanzania, Emmanuel Mlundwa wa PST na Yasin Abdallah 'Ustaadh' wa TPBO kutaka kujua ukweli kuhusu tuhuma hizo, ambapo walikuwa na maoni tofauti .
Mlundwa alisema kinachowaponza mabondia wa Tanzania siyo hujuma wala nini ila maandalizi duni wanayofanya kabla ya mapambano yao pia kuwa na viwango duni kulinganisha na wapinzani wao wanaoenda kucheza nao.

"Ngumi za kulipwa ni biashara, mabondia wa ngumi hizo wanapotafutiwa mechi wanapaswa kujiandaa, lakini hilo halifanyiki na hivyo kwenda kulitia aibu taifa na kujiharibia soko wao wenyewe bila kujua," alisema Mlundwa.
Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa ngumi, alisema siyo kweli kama kuna rushwa zinazofanyika bali Watanzania wanaopewa nafasi kulingana na rekodi zao nchini huenda kupigana kichovu kwa kukosa maandalizi mazuri.
Ustaadh yeye alisema
Francis Cheka
linalowaangusha mabondia wa Tanzania nje ya nchi ni maisha wanayoishi kuwa kinyume na nidhamu ya ngumi za kulipwa na kwamba kutokuwa na mameneja ni tatizo jingine linalowakwaza.
"Mabondia wengi hawafanyi mazoezi mpaka wakati wa pambano, hapo unatarajia afanye vizuri? Pia hawaishi kwa kuzingatia miiko ya ngumi na hivyo wanapoenda nje ni rahisi kupigwa na kuhisiwa labda wanauza," anasema.

Alisema ni vyema mabondia wakafanya kazi chini ya mameneja kama ilivyokuwa kwa Rashid Matumla kwani itafanya ajikite kwenye mazoezi tu na mambo mengine kuwaachia meneja zao.
Ustaadh alisema majukumu wanayobeba mabondia ya kufanya kila kitu wakati mwingine huwafanya washindwe kujikita kwenye mazoezi na hivyo kujikuta muda wa pambano ukifika hawajajiandaa vizuri.
Rais huyo wa TPBO-Limited, alisema pia mabondia wengi hutoa visingizio kila wanapopigwa nje ya nchi bila kuangalia kama sheria za ngumi zinasemaje wanapokuwa kwenye ulingo na kutolea mfano pigano la Cheka na Arik.
"Cheka alipolalamika nilimuuliza vipi katika pambano lake na Arik, hakutupa ngumi yoyote katika raundi ya 7 na kupigwa makonde mfululizo na kunieleza mkono wa kulia ulimzingua, sheria zinasema bondia asipojibu mapigo kwa zaidi ya ngumi 10 alizorushiwa refa anaweza kuvunja pambano au wasaidizi wa bondia kuingilia kati kwa kurusha kitaulo na ndivyo ilivyotokea," alisema.
Mada Maugo

JACK WOLPER AMJIBU MBAYA WAKE ALIYETANGAZA KUWA YEYE NI KAHABAMsanii nyota wa filamu bongo, Jacqueline Wolper amewataka wasanii wa bongo movie kuacha tabia ya kupigana majungu ya kinafiki ambayo huchangia kujenga bifu za kijinga....

Akiongea na mpekuzi wetu, wolper alidai kuwa kuna mipaka ya watu kuishi lakini kuna baadhi ya wasanii wanaamini kwamba majungu ndo mshahara wao kiasi kwamba wasipomsengenya mtu basi hawawezi kuishi...

Wolper anadai kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii wanaosemwa sana kwa mabaya hasa kuhusu maisha yake ya kila siku.Hali hiyo inatokana na umaarufu alionao ambao huwafanya wasanii wenzake wamchukie hasa wasanii wa kike...

Hii ni kauli ya Wolper alipoongea na ripota wetu:

"Wasanii tungekuwa na ushirikiano kama nisha tungefika mbali sana.

"Mimi simuogopi mtu katika maisha yangu, lakini ninachohitaji katika maisha yangu ni Heshima.

"Ukiona nimekukwaza, basi njoo nyumbani au nambie nikufuate ili tuyamalize kibinadamu na si kudhalilishana mitandaoni...


"Kuna msanii mmoja wa kike amekuwa akinichafua sana mitandaoni kwa kuniita kahaba, najuza na matusi mengine kibao.

"Huyo ni mtu anayetafuta pakutokea, anatafuta kujulikana kupitia Wolper na pengine kafulia na sasa anatafuta mtaji.

"Tangu anitukane sikuona haja ya kumjibu kutokana na heshima niliyo nayo katika kazi yangu na heshima yangu kwa wazazi , ndugu na jamaa.


"Niliamua kumwachia mungu.Kama ni kahaba au najiuza, mungu anajua.Alisema Wolper

KESI YA LADY JAYDEE YAPIGWA KALENDAMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi wake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.
Kwa mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia mitandao ya kijamii.

Tuesday, July 30, 2013

SUPER D SUPER COACH ALIPO JUMUHIKA NA NDUGU NA JAMAA ZAKE WA KARIBU KUFUTURU NYUMBANI KWAKE

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na jamaa na ndugu zake baada ya kupata futali ya pamoja  nyumbani kwake wakati wa chungu 20 Ramadhani
SUPER D AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA NDUGU ZAKE NA MARAFIKI

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D'  Katikati akiwa katika picha ya pamoja na jamaa na ndugu zake baada ya kupata futali ya pamoja  nyumbani kwake wakati wa chungu 20 Ramadhani

Super D akipata futari na Ibrahimu Kamwe
Super D akipata futari na Ibrahimu Kamwe

Super D akipata futari na Ibrahimu Kamwe

SUPER D

SUPER D KATIKA POZI

DAR ES SALAAM KUWA MWENYEJI WA MAONYESHO YA VODACOM ELIMU EXPO 2013 VIWANJA VYA CHUO CHA POSTA KIJITONYAMA AGOSTI 30
 Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Kivukoni, Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa maonyesho ya siku tatu ya Vodacom Elimu Expo, yanayotarajia kuanza Agosti 30, mwaka huu katika Viwanja vya Michezo vya Chuo cha Posta, Kijitonyama jijini. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa. 

 Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo (katikati) Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kulia) na  Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, wakigonganisha glasi, kama ishara ya uzinduzi wa maonyesho hayo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo leo, Katikati ni   Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo leo, Katikati ni   Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, na Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

 Sehemu ya waandishi wa habari, waliohudhuria mkutano huo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza Naibu Waziri wa Elimu.
 Naibu Waziri, wakati akizungumza na wanahabari hao leo.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
**********************************************************
Mji wa Dar es salaam umeandaliwa kuwa mwenyeji wa maonyesho ya elimu ya kwanza ya aina yake mwaka huu, katika uwanja utakaoruhusu muingiliano na majadiliano kati yawatengenezaji wa sera, wapenda maendeleo, watunzi mbalimbali, wazazi, wanafunzi, na jamii kwa ujumla.

Maonyesho hayo yaliyopewa jina la Vodacom Elimu Expo, yanalenga kuwahusisha wadau wote wa elimu katika kuangalia mianya iliyopo, kugundua changamoto na kutafutia suluhisho ili kupelekea elimu bora kwa Watanzania kwa ujumla.

Ni tukio litakalochukua siku tatu kuanzia tarehe 30 mwezi wa nane mwaka 2013 na litafanyikia viwanja vya michezo vya Posta Kijitonyama, Dar es salaam.

Wasemaji mbalimbali kutoka mashirika na viwanda tofauti wataongelea kuhusu viwanda vyao na vilevile kukutana na watu ambao wanapenda makampuni yao na bidhaa zao.

“Maonyesho haya ya kujivunia yamepewa maudhui yasemayo ‘Elimu Bora ndio Tegemeo la Watoto wetu, Tuijenge kwa Pamoja.’ Tunawasihi wadau wa elimu kujitokeza kwa wingi katika maonyesho haya. 

Elimu ndiyo ufunguo wa maendeleo katika taifa hili kubwa, na kusaidia elimu katika nyanja tofauti ndio kubwa tunaloweza kufanya”, alisema Njama, Mkurugenzi Mkuu wa maonyesho haya.

Pia aliongezea kuwa wageni zaidi ya 150,000 wanatarajiwa kuhudhuria katika maonyesho haya, wakiwepo pia wasanii na waburudishaji mbalimbali katika umati huo wa watu.

Akiongea wakati akitangaza udhamini wa maonyesho hayo Dar es salaam, Kelvin Twissa, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, alielezea matumaini yake kuwa Vodacom Elimu Expo itasaidia kusuluhisha changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya elimu hapa nchini.

Moja ya changamoto hizo kubwa ni ile ya kulipa ada ya shule, ambalo limeonekana ni jambo la kuchosha sana na kupoteza muda katika mistari mirefu ya benki.

“Ni jambo la kusikitisha kabisa kuchelewa kulipa ada ya shule kwa sababu ya foleni zilizopo katika benki zetu. 

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imekuja na njia ya kuitatua changamoto hii. Sasa hivi kuna uwezekano wa kulipa ada ya shule kupitia M-Pesa. Tunawasihi wadau wa elimu wanaomiliki shule kuanza kutumia huduma hii,” alisema Twissa.

Maneno hayo pia yalisisitizwa na Mheshimiwa Philip Mulugo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ambaye pia alisema serikali ina jukumu la kuhakikishia elimu bora wananchi wake na katika hali ambayo kila mtu anaweza kugharamia. 

“Hii ni fursa kwa wale wote ambao wanajadili na kuja na suluhisho ambalo litapelekea elimu Tanzania kuendelea katika njia iliyo bora. Serikali itatoa kila kinachohitajika ili kufanikisha
jambo hili,” alisema Mulugo.

Vodacom Elimu Expo, tukio lililoandaliwa na Masoko Agencies Tanzania Limited, ni tukio linalokusudia kushawishi ubora na mabadilishano ya habari na majadiliano ya kielimu ambayo yanalenga katika uboreshaji wa ngazi za kielimu Tanzania.

Baadhi ya wadhamini wa maonyesho haya ni, Clouds FM, DTV, Entertainment Masters, Mwananchi Communications Ltd, Times FM, Primebiz Solutions Ltd, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
*************************************
Kuhusu Vodacom Tanzania
Vodacom Tanzania ni kampuni inayoongoza kwa mawasiliano ikiwapa ubunifu wa mawasiliano ya GSM nchini kote.

Kampuni ya Vodacom Tanzania ni ni kampuni shiriki ya Vodacom (Pty) ltd. South Africa ambayo pia ni kampuni shiriki ya Vodafone Group UK. Vodacom Group ( Pty) wanamiliki hisa asilimia 65, na zingine 35 zikimilikiwa na Mirambo Ltd. 

Vodacom Tanzania imepewa heshima ya kuwa kampuni bora kuliko zote katika miaka iliyofuatana kuanzia 2009 -2012.

Vodacom Tanzania ina matawi makuu 6 Dar es salaam na maduka tegemezi 66 nchini kote.

Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya wananchi na ipo kusaidia jamii kwa kupitia Vodacom foundation.

Vodacom foundation ina nguzo kuu tatu ambazo ni, afya, elimu na mambo ya jamii. Mfuko wa Vodacom foundation umesaidia zaidi ya miradi 120 ndani ya nchi na imeshinda tuzo za kitaifa na kimataifa kwenye tuzo za usaidiaji wa jamii ambazo ni East African CSR Awards na Diversion na Inclusion Awards ambayo hutolewa na Vodafone group iliyopo Milan.

Wasiliana na: Georgia Mutagahywa, Mkuu: Idara ya Mawasiliano, 0754 711 215
Kuhusu Muandaaji Vodacom Elimu Expo, tukio lililoandaliwa na Masoko Agencies Tanzania Limited, ni tukio linalokusudia kuwashawishi ubora wa mabadilishano ya habari na majadiliano ya kielimu ambayo yanalenga katika uboreshaji wa ngazi za kielimu Tanzania.

Kuunganisha malighafi za kielimu zilizopo nchini na ukuaji wa teknologia ilikuwa chanzo kikubwa cha waandaaji kwa kuwa walitarajia kutumia nyenzo zillizopo katika huduma za mawasiliano katika kukuza jamii yenye uelewa wa mambo.

Masoko Agencies Tanzania Limited wanalenga katika kuwafi kishia watu elimu na kuwafanya watu wajishirikishe katika nyanja za elimu. 

Tunalenga katika kuendeleza ajenda ambazo watunzi mbali mbali na wasomaji, wawekezaji na wadhamini, pia wazazi na watengeneza sera mbalimbali watakaa pamoja na
kujenga jamii yenye uelewa.

Kufanya kazi na taasisi zote za elimu zikiwepo shule, vyuo, na vyuo vikuu Tanzania, tunalenga kukuza ufaulu kwa kuzijua changamoto wanazokumbana nazo na pia kikubwa zaidi kuziletea suluhisho changamoto hizo.

MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA KUPITIA MDAU AKABIDHI VIFAA KWA AL - MADRASSATUL MUNAUWARATUL ISLAMIYA CHA MSASANI BONDE LA MPUNGA.


IMG_1336

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya iliyopo Msasani Bonde la Mpunga Ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Spika mbili, Vipaza sauti viwili (Microphones) pamoja na Amplifaya ambavyo vitatumika kuendeshea shughuli mbalimbali za kueneza mafunzo ya dini kwa jamii na watoto wanaosoma chuoni hapo. Vifaa hivyo vimetolewa na mdau mpenda maendeleo kupitia kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
IMG_1345
Pichani juu na chini ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pamoja na Bw. Abdulmalik Ibrahim (kulia) aliyemwakilishi mdau aliyetoa vifaa hivyo (jina kapuni) wakikabidhi Spika tatu, vipaza sauti viwili na Mixer kwa Katibu wa Madrasa hiyo Bw. Salim Amri (wa pili kushoto) aliyeambatana na Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah (katikati). Kushoto ni mmoja wa walimu wa madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la Mpunga Ustaadh Mohamed Kassim.
IMG_1339
IMG_1344
Mstahiki Meya Jerry Silaa akikagua moja vifaa hivyo alivyokabidhi leo ofisini kwake .
IMG_1360
Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya ya Msasani Bonde la Mpunga akitoa shukrani kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa pamoja na mdau alijitolea baada ya kupokea vifaa hivyo ambavyo amesema vitawasaidia katika kazi zao za kueneza neno la Mungu hasa kipindi hichi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo kuhubiri Amani nchini.
IMG_1372
Uongozi wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la Mpunga wakiomba dua za baraka kwa msaada waliopokea leo ofisini kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa.

MPAMBANO MWINGINE WA MASUMBWI KUFANYIKA IDI MOSIkocha kwame mkuluma kulia akimwelekeza Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' jinsi ya kutupa makonde mazito mazito Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na SUPER D Bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' yupo kambini kwa ajili ya kupambana na bondia Bahati Mwafyela mpambano utakaofanyika siku ya sikukuu ya Idi Mosi jijini Dar es salaam katika ukumbi wa friends Corner Manzese akizungumzia maandalizi ya mpambano huo mtaalishaji Waziri Rosta amesema mpambano huo wa uzito wa juu umekuwa gumzo katika jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kwani mabondia hawo wanatafutana kwa mda mrefu sana na sasa wamekutana kwa ajili ya mchezo huo Mpambano huo wa raundi 8 siwakukosa kwani ndio mpambano pekee kwa mwaka huu kukutanisha uzito wa juu kwani mabondia wa uzito huu  wanaotamba viwango vyao ni vidogo ukizingatia kuwa wapo wachache nchini aliongeza kuwa mbali na mpambano huo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia chipkizi na wanaotamba hapa nchini Na kwa upande wa kocha anaemnoa bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' amesema kuwa bondia wake alikuwa na manyama nyama mengi lakini kwa sasa akuna kutokana na mazoezi anayompatia kwani kwa sasa dozi yake ni kutwa mara tatu na mpaka siku ya mchezo naisi mambo yatakuwa safi Mpambano huo utakao sindikizwa na mabondia Hassani Mandula atakae pambana na Twalib Mchanjo na Fadhili Majia atakae menyana na Ally Mahiyo na Mustapha Doto atapambana na Hashimu Mjeshi mapambano yote ya utangulizi itakuwa ni ya raundi sita
Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zitakazokuwa zikisabazwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
 
DVD hizo mpya ni kati ya  
mike tyson vs evander holyfield na felix trinidad vs roy jones jr

Felix 'Tito' Trinidad vs Pernell Whitaker

ambapo dvd hizo zilizo rekodiwa kwa ubora wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mchezo wa masumbwi nchin


--
Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
           mhamila1@gmail.com
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Airtel yakabidhi milioni 14 kwa washindi wa promosheni ya Airtel yatosha. Mteja wa Airtel mkoani arusha bw, Robert Justin akihesabu pesa zake alizojishindia wakati wa promosheni ya Airtel yatosha mara baada ya kuzitoa kupitia njia ya Airtel Money katika ofisi za Airtel mkoani
Arusha.

 Meneja wa airte Mauzo wa kanda ya kaskazini Stephen Akyooo akikabidhi shilingi milioni 1 kwa Bw, Robert Justine wa jijini Arusha fedha alizojishindia katika promosheni  ya Airtel Yatosha inayoendeshwa na Airtel maalum kwa wateja  wake wote wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha kwa wiki, siku au mwezi mbapo pia mteja anaweza kujishindia moja kati ya Nyumba 3 za kisasa zilizopo dar es salaam.
Meneja wa airtel kanda ya kaskazini Stephen Akyoo akiwa na washindi wawili wa shilingi milion moja wa shindano la airtel yatosha kutoka  mkoani Arusha bw, Robert Justine and Balistus Mambo. Washindi wote walikabidhiwa shilingi milioni moja kila mmoja walizojishindia katika promosheni ya Airtel yatosha na kuzitoa kwa Airtel Money.


=======  =======  =====

Airtel yakabidhi milioni 14 kwa washindi wa promosheni ya  Airtel yatosha.
•         Ni washindi wa shilingi milioni moja wa wiki ya kwanza na ya
pili ya promosheni

Jumapili 28 julai 2013, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaa na kuwazawadia washindi 14 wa kila siku wa promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba  kila mmoja shilingi milioni moja pesa taslimu kupitia huduma ya Airtel Money.

Washindi hawa wamepatikana kupitia droo ya wiki ya kwanza na ya wiki ya pili ambapo jumla ya washindi 14 kutoka katika mikoa mbalimbali ya nchi walipatikana na hatimaye kukabithiwa pesa zao

Akiongea wakati wa kukabithi zawadi kwa washindi hao Meneja Mauzo wa
Kanda Mkoani Arusha  bwana Stephen Akyoo  alisema” leo tunayofuraha

kupata washindi wa promosheni ya Airtel yatosha na kuwakabithi zawadi zao. Washindi hawa wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali na kujishindia kila mmoja shilingi milioni moja pesa taslimu kwa kutumia
huduma za Airtel yatosha  na kujiunga na vifurushi vyetu mbalimbali. nae Meneja Uhusiano wa Airtel Akitangaza majina ya washindi hao bwana
Jackson Mmbando alisema "washindi wetu wa wiki ya kwanza na ya pili ni
pamoja na  Hawa Said Mkazi wa Mtwara, John Masawe mkazi wa singida,

Joseph Emmanuel Nchimbi Songea,  Rosemary Michael na John Masanja kutoka Tabora , Zuhura Sabuni kutoka Lindi, Balistus mambo kutoka Moshi, Robert Faustine kutoka Arusha ,  Frank Ladislaus na Paulina Michael kutoka Sengerema Mwanza, Flavian Adamson Malilo kutoka Katavi,

Jacob Muhole kutoka Dodoma,  Singodi Severin kutoka Kagera  na Ephrasia Thadeo kutoka Ngara.

Ili kushiriki mteja anatakiwa kupiga  kupiga *149*99#  na kununua kifurushi cha huduma ya Airtel yatosha cha siku, wiki au mwezi na kuunganishwa mojakwamoja kushiriki kwenye promosheni na kupata nafasi ya kushinda nyumba au pesa taslimu shilingi milioni moja kila siku.

Akiongea mara baada ya kukabithiwa zawadi hiyo Bwana Robert Justine moja kati ya washindi anayetokea mkoani Arusha alisema” nimefurahi

sana kuwa mshindi wa promosheni na ntaendelea kutumia huduma ya Airtel
yatosha ili kuendelea kufaidika na huduma hii na kupata nafasi ya
kushinda nyumba. Natoa wito kwa watanzania kutumia huduma hii na
kuhakikishia   hata wao wananafasi ya kushinda kama mimi nilivyoweza

leo kukabithiwa shilingi milioni moja kwa kutumia tu huduma ya Airtel
yatosha. Promosheni ya Airtel yatosha bado inaendelea kwa mienzi mitatu hadi hapo mwishoni mwa mwenzi wa tisa ambapo mbali na zawadi za pesa taslimu wateja pia wanapata nafasi ya kujishindia nyumba 3 zilizopo kigamboni jijini Dar es saalam

DR. ALI MOHAMED SHEIN ALA FURATI NA WANANCHINI WA MKOA WA KUSINI UNGUJA


IMG_2627Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) pamoja na Viongozi na wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kusini Unguja, wakijumuika katika chakula cha futari aliyoiandaa katika viwanja vya Jengo la Ofisi ya Uhamiaji Tunguu jana. IMG_2638Baadhi ya Wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wakifurahi katika Viwanja vya Ofisi ya Uhamiaji Tunguu,katika mualiko wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, kwa Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja jana. IMG_2649Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akipeana mkono wa shukurani na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Alhaj Dk.Mohamed Gharib Bilal,baada ya futari aliyomualika jana huko katika viwanja vya Ofisi ya Uhamiaji Tunguu,Mkoa wa Kusini Unguja.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

LHRC YATOA TAARIFA YA NUSU MWAKA YA MATUKIO MBALIMBALI NCHINI KUANZIA JANUARY-JUNE 2013


1 Mtafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu  (LHRC), Pasience Mlowe (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Julai 29, 2013, wakati akitoa taarifa ya nusu mwaka ya kuanzia  Januari hadi Juni 2013 ya kituo hicho kuhusu mambo  mbalimbali yaliyotokea nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji wa Kituo hicho Imelda Urio. 2 Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji wa Kituo  hicho Imelda Urio, akizungumza katika mkutano huo.
3 Mtafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Pasience Mlowe (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Wengine ni watafiti wa kituo hicho
4Baadhi ya waandishi wa habari waliodhuria mkutano  jana.PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE.

Sunday, July 28, 2013

MADA MAUGO NA BENSON MWAKYEMBE WACHEZEA VICHAPO TOKA KWA WARUSSIA


MAUGO
BONDIA mada maugo  mwishoni mwa wiki iliyopita alichezea kichapo kutoka kwa  Movsur Yusupov wa Russia  katika mpambano uliopagwa kupigwa kwa raundi nane hata hivyo Maugo alipigwa kwa TKO ya raundi ya tano

ambapo Maugo alisalim amri kwa kupoteza mchezo huo ulifanyika katika viwanja vya Trade And Entertainment Centre "Moskva", Kaspiysk, Russia mwishoni mwa wiki iliyopita

Baada ya kupoteza mchezo uho August 30 atapanda tena uringoni kukabiliana na Thomasi Mashali mpambano wa ubingwa wa WBF Africa uzito wa kati mpambano utakaokuwa wa raundi 12
mwakyembe

Nae bondia benson mwakyembe alikuwa na kibarua kizito siku hiyo hiyo nae alikubali kichapo cha K,O ya raundi ya 7 katika mpambano wa raundi 8

Mabondia wote wawili walionesha kuwa na viwango vya kutosha ila walizidiwa ufundi na maarifa ya mchezo wa masumbwi uringoni
Mchezo wa masumbwi umekuwa ukipanda umaarufu siku adi siku baada ya mabondia wengi kutoka nje ya nchi kwenda kushiriki michezo mbalimbali katika nchi nyingine ambapo imeleta muhamko wa mchezo huo kupendwa na watu wengi zaidi ingawa wadhamini wanaukwepa kwa ajili ya kuwekeza katika mchezo huo

Hata hivyo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini   Rajabu Mhamila 'Super D' amekuwa akitoa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi akitumia mabondia kutoka mataifa yanayofanya vizuri katika mchezo huo ili kujua mbinu mbalimbali wanazotumia
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...