Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 25, 2013

MADA MAUGO NA BENSON MWAKEMBE WAKWEA PIPA KUWAKABILI WARUSI


             TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI-MICHEZO
mabondia mada maugo na benson mwakyembe leo saa kumi alasiri wameondoka nchini kuelekea nchni urusi kwa ajili ya mapambano yao yasiyokuwa ya ubingwa.
mada maugo atapambana na MOVSUR YUSUPOV wakati benson mwakyembe atazipiga na PTI USTRAKHANOV .
mabondia hao watazichapa katika uzito wa super middle [kg 75] ni mapambano ya raundi nane [8]

mabondia hao wamejiandaa vyema sana kwani masharti ya mikataba yao ni magumu sana nayo ni;-

bondia atakayepigwa na kushindwa pambano kwa udhaifu wa kiwango chake au  kutojiandaa vyema kwa ajili ya pambano hilo na ikathibitika hivyo ,bondia atalipwa malipo kwa raundi alizozicheza tu.
masharti haya ya mkataba yanawalazimisha mabondia hawa kupigana kwa kiwango cha juu ,kwa sababu moja ya sababu zilizofanya mkataba kuwekewa masharti haya magumu ni tabia ya baadhi ya mabondia kutoka nchi za afrika kujiangusha kwa makusudi ulingoni wakisingizia wamepigwa na kumbe wanawatengenezea rekodi mabondia wa nchi za ASSIA NA ULAYA.

Mada maugo na benson mwakyembe wameondondoka na ndege ya shirika la EMIRATES ,na wanatarajiwa kurejea nchini tanzania tarehe 29-07-2013

TPBO-LIMITED INAWATAKIA SAFARI NJEMA ,NA YENYE MAFANIKIO,NA MUNGU AWAREJESHE NYUMBANI SALAMA.

                              
                                              imeletwa kwenu nami;-
                                                                yassin abdallah mwaipaya-ustaadh

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...