Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 25, 2013

BONDIA MTANZANIA OMARI KIMWERI 'LION BOY' KUPAMBANA TENA AUSTRALIAOmari Kimweri
BONDIA Mtanzania Omari Kimweri  'Lion Boy' anaefanya shughuli zake nchini  Australia anatarajia kupanda ulingoni mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya kuchezo mpambano wake mwingine baada ya kuwatwanga mabondia kadhaa nchini humo bondia huyo anaechezea uzito wa light flyweight
Amesema kuwa ataendeleza wimbi la ushindi kwa kutoa vipigo kama alivyotoa kwa bondia   Yodpichai Sithsaithong pamoja na  Lookrak Kiatmungmee ambazo ndio mechi zake za mwisho kucheza kabla ya hii inayomkabili punde

Aliongeza kwa kusema kuwa unajua mimi ni Bingwa hivyo sito kubali kupoteza mpambano huo utakaofanyika katika ukumbi wa  The Melbourne Pavilion nchini  Australia mpambano huo utakaosimamiwa na kamisheni ya nchi hiyo umekuwa gumzo kila kona kwa kuwa bondia Mtanzania  Kimweri amejizolea umaarufu mkubwa nchini humo

Bondia huyo aliyeanza kujishulisha na mchezo wa ngumi za kulipwa nchini    Australia mwaka 
2007  


Mpaka sasa akiendelea na shughuli zake hizo amesema lengo lake kubwa ni kuchukuwa mikanda inayotambulika kimataifa ingwa yeye kwa sasa ni bingwa wa WBO ambapo aliupata kwa kumtwanga bondia  Panmongkol Ekarin  wa Thailand bondia huyo amewaomba watanzania kumuombea duwa kwani ana kibarua kizito cha kuitanganza nchi yake kimataifa bondia huyo mwenye uraia wa nchi mbili Tanzania na Austalia amesema ana mpango wa kuja Tanzania na kuzamini mchezo uho kama mfadhili endapo marengo yake yatatimia alisema 'mimi nataka nije kupigana Tanzania nikiwa mchezaji na promota vile vile hivyo nafanya mpango huo mambo yakiwa mazuri nitakuja bongo ili nifanye uwekezaji katika Boxing '


Bondia huyo mpaka sasa amekwisha cheza mapambano   15 akishinda 12  na kupoteza mapambano matatu bondia huyo anayefananishwa na Simba muwindaji amekuwa tishio kwa mabondia wenye uzito wake kwa niaba ya watanzania wote tunaungana kumsapoti bondia Omari Kimweri anayefanya kazi zake nchini Austalia aweze kushinda mpambano waku huo Mungu Ibariki Africa,Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Bondia Omari Kimweri, AMIN
Bondia Mtanzania Omari Kimweri akinyooshwa mkono juu kuashiria ushindi wake

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...