Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 29, 2013

BONDIA IDDY MKWERA AMCHIMBIA MKWALA LUCAS NDULA WA MUHEZA




IDDY MKWERA
BONDIA Iddy Mkwera wa Dar es salaam anatarajia kuzipiga na Lucas Ndula wa Muheza wakati wa kusherekea sikukuu za pasaka jumapili ya march 31 katika viwanja vya wazi vya Jitegemee vilivyopo wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga
Bondia huyo  aliyefika Muheza kwa mbwembwe na kusema atamtwanga
Ndula
K,O ya raundi ya pili ili arudi na ushindi Dar es salaam kwa ushindi mnono unajua mimi nafundishwa na kocha wa kimataifa Rajabu Mhamila 'Super D'  anaejua mbinu zote za masumbwi Duniani na nimefanyia mazoezi miezi miwili hivyo sitarajii kuremba katika mpambano huo kwani kwa sasa nimeamua kucheza mchezo huu na ninawambia mabondia wote walio katika uzito wa kg, 60 kuwa tayali kupambana na mimi

Mchezo huo utakaochezwa katika viwanja vya jitegemee Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga utakuwa na bule hivyo watu mbalimbali wameobwa kujitokeza kuja kuangalia vipaji vya mchezo huo wenye kupendwa na vijana wengi nchini

Nae mmoja wa wadau wa nchezo wa ngumi Muheza Allan Augastino ambaye aliyetoa galama mbalimbali amesema vijana wengi wanapenda ngumi hivyo nimeamua kuwaletea hapa hapa bila kujali chochote na kugalamia kila kitu ikiwemo mabondia kutoka Dar pamoja na ulingo  maalumu kwa ajili ya kuchezea

Mbali na mbambano uho kutakua na mapambano mengine mbali mbali ambapo Omari Kibwana wa dar atapambana na
Bakari Sendekwa

  Nae kocha wa mchezo huo Muheza, Chalres Muhilu ' Spins' alisema mpambano huo wa wazi umeandaliwa kwa ajili ya kutoa burudani wilayani hapo na kuhamasisha mchezo wa masumbwi

mabondia kutoka Dar wakipambana na Muheza pamoja na kutoa rai kujitokeza kwa wafadhili kudhamini mchezo huo unaopendwa na vijana wengi wilayani humo ndio mana tumeamua kuweka katika viwanja vya wazi ili watu wote wajionee wenyewe mchezo wa ngumi unavyo endeshwa katika mazingira magumu

Nae Kocha wa kimataifa wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' aliyepewa jukumu la kwenda na vijana kutoka Dar ili wakalete changamoto na kuleta amasa ya mchezo huo amesema atakwenda na Omary Kibwana  atakayemenyana na Bakari Sendekwa katika uzito wa kilo 52 na Iddy Mkwera atakaepambana na Lucas Ndula mpambano wa raundi 6

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

TIMU YA LIVERPOOL YA WATOTO WAFANYA ZIARA YA PASAKA NA KUTOA ZAWADI


Visiting time: Samed Yesil, Jordan Ibe, Kristoffer Peterson, Craig Roddan, Ryan McLaughlin and Jack Dunn
Katika picha: Samed Yesil, Jordan Ibe, Kristoffer Peterson, Craig Roddan, Ryan McLaughlin na Jack Dunn.

Wachezaji vijana wa Liverpool wameonyesha upendo na kuguswa na watoto walioko mahospitalini katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ya Pasaka.

Kama inavyofanywa na watu mbalimbali nyakati kama hizi za sikukuu ya Pasaka na wao pia wamewatembelea watoto na kuwapa zawadi katika hospitali iliyoko karibu na klabu yao ya Liverpool.

 Jumla ya vijana wa klabu hiyo kumi na moja kutoka katika kituo cha kukuzia vipaji cha klabu hiyo, wametembelea hospitali ya Alder Hey jana na kuzungumza na watoto ambapo wataendelea kuwepo hospitalini hapo kipindi chote za sikukuu ya Pasaka.
 
Mlinzi Conor Coady mwenye umri wa miaka 20, ambaye alikuwepo katika kikosi cha kwanza cha Liverpool katika mchezo dhidi ya Anzhi Makhachkala katika michuano ya Ulaya 'Europa League' naye alikuwa ni miongoni mwa hao waliofanya ziara hiyo.
Amekaririwa akisema kinda huyo akisema, ‘Kufanya ziara kwa watoto hao ilikuwa jambo kubwa'.
Ameendelea kwa kusema, ‘Nina wadogo zangu nyumbani kwa hiyo najua nini maana ya watoto hawa kupata ujio wetu hususani kwa kuwapa faraja katika kipindi hiki.’
 
Wachezaji hao waligawanyika katika makundi ili kutoa nafasi ya kuzungumza watoto wengi zaidi pamoja na familia zao.
Coady aliuungana na kundi lililokuwa likitoa zawadi ya Chocolate akiwa na wachezaji wengine Lloyd Jones, Jordan Ibe, Ryan McLaughlin, Jack Dunn, na Brad Smith.
Easter bonus: The Liverpool youth players dropped into Alder Hey Hospital to visit the children
Pia alikuwepo Samed Yesil, ambaye mpaka sasa ameshaichezea ligi ndogo ya Capital One michezo miwili kama ilivyokuwa Kristoffer Peterson, Danny Ward, Adam Morgan na Craig Roddan.
Regulars: The academy players visit the hospital every month to see the children
Alder Hey Children’s NHS Foundation Trust ni moja kati ya vituo vya afya vinavyokusanya watoto wengi barani Ulaya ambapo watoto zaidi ya laki mbili hupatiwa huduma kila mwaka.

MATUKIO MUHIMU KUTOKA RUVUMA


 Baadhi ya waandishi wa Habari mkoani Ruvuma kulia wakimsikiliza mhandisi wa maji taka na mazingira wa mamlaka ya maji safi na taka manispaa ya Songea9SOUWASA) Eddie Emanuel  jana wakati walipotembelea mabwawa ya maji taka katika eneo la Londoni mjini Songea.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga wakimsikiliza mwenyekiti wa halmashauri hiyo Oddo Mwisho(hayupo pichani0wakati wa kikao chao hivi karibuni mjini Mbinga.

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KUUAGA MWILI WA MBUNGE WA CHAMBANI DAR ES SALAAM LEO


  Kaimu Katibu wa Bunge Mhe John Joel akisoma wasifu wa marehemu
 Rais jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Spika Anne Makinda alipowasili katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Rais jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mbunge wa Monduli Mhe Edward Lowassa na Mbunge wa Mafia Mhe Abdulkarim Shah alipowasili katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Rais jakaya Mrisho Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 na kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Mama Salma Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo  katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 ambapo Rais Kikwete aliongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Wabunge wanawake wakiwa katika maombolezo  katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 ambapo Rais Kikwete aliongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Rais jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongzi wa kitaifa na wabunge katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 ambako aliongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.

UCHAGUZI MIKUU BFT KUFANYIKA JIJINI MWANZA


Viongozi wa sasa BFT, Rasi Joan Minja (kulia) na Katibu Mkuu, Mashaga makore

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Mchezo wa Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) unatarajiwa kufanyika Mei mwaka huu jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa BFT, Mashaga Makore, aliiambia MICHARAZO asubuhi ya leo kuwa, kuwa uchaguzi huo utafanyika mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kimataifa ya Majiji yanayotarajiwa kufanyika jijini humo kati ya Mei 20-25.
Makore alisema mchakato wa kuelekea kwenye kinyang'anyiro hicho ambacho kitatanguliwa na Mkutano Mkuu wa shirikishi hilo utatangazwa mara baada ya shamrashamra za sikukuu ya Pasaka.
"Uchaguzi Mkuu wa BFT utafanyika mwezi Mei jijini Mwanza mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya kimataifa ya ngumi inayoshiriki miji mikuu ya Afrika Mashariki na Kati, ambapo utatanguliwa na Mkutano Mkuu," alisema Makore.
Makore alisema maamuzi hayo yalifikiwa na Kamati yao ya Utendaji iliyokaa hivi karibuni na kutoa wito kwa wadau wa mchezo huo wenye uwezo na sifa za kuongoza shirikisho hilo kujiandaa kuijitosa kuwania uongozi kwenye uchaguzi huo.

JENGO LA GHOROFA 16 LAANGUKA KATIKATI YA JIJI


 Mtoto Maisamali Karim (6) ambaye ameokolewa kutoka katika madrasa ya Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri Jamaat iliyoangukiwa na jengo hilo katika mtaa wa Indira Gandhi. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
 Changamoto ya uokoaji ni ngumu, lakini vikosi mbalimbali vinaendelea na zoezi hilo, ili kunusuru maisha ya waliofukiwa na kifusi.
 Hizi nia aina ya nondo ambazo kimsingi sio imara kuweza kuhimili ujenzi wa ghorofa ndefu kama hili, kuna haja mamlaka husika likatupia macho kampuni za ujenzi ili kuokoa maisha ya wajenzi na watumiaji wa majengo hayo.
 Askari wakiimarisha ulinzi wakati zoezi la uokoaji likiendelea.
  Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea, huku nondo nyembamba zikionekana na kuacha maswali miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.
  Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
 Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
Waokoaji.

 Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP), Suleima Kova kuhusu jengo la ghorofa 16 lililoanguka majira ya saa mbili asubuhi katika makutano ya mtaa wa Indira Ghandi na Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi. Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo hapo. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
 Waokoaji wakiwa kazini.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova akiwa katika eneo la tukio. Kulia ni Mbunge wa viti maalum (NCCR-Mageuzi James Mbatia.

CRDB CHINA DESK YAZINDULIWA


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu na  Balozi wa China hapa nchini, Lü Youqing wakiwasili katika hoteli ya Serena.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.
 Balozi wa China hapa nchini, Lü Youqing akitoa hotuba yake.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa.


DAR ES SALAAM, Tanzania

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei, amewataka wajasiriamali na wawekezaji wanaofanya biashara zao kati ya Tanzania na China, kuchangamkia fursa pana ya ukuzaji mitaji yao na pato kwa kutumia huduma mpya ya CRDB China Desk.

Dk Kimei aliyasema hayo jana wakati wa hafla ya uzinduzi wa China Desk, inayotolewa na CRDB, itakayo wahudumia wafanyabiashara, wajasiriamali na wawekezaji wanaofanyakazi zao baina ya mataifa hayo rafiki.
“China Desk, ni huduma yenye fursa inayoweza sio tu kusaidia kukuza mitaji na kutanua wigo wa maendeleo, bali kudumisha ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo baina ya China na Tanzania, ambao uliasisiwa karibia nusu karne iliyopita,” alisema Dk Kimei katika hafla hiyo.

Aidha, akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, aliiomba CRDB kuboresha utoaji wa mikopo ya riba nafuu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, ili kuharakisha ukuaji wa pato la Mtanzania na Taifa kwa ujumla.

Dk Nagu alibainisha kuwa, taasisi za kipesa nchini zina mchango mkubwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kukuza pato lao, kama zitakuwa tayari kuwapa mikopo yenye masharti nafuu na riba ndogo, ili kusaidia harakati zao za kujikwamua na kukuza uchumi wa taifa.

“CRDB mnastahili pongezi kwa huduma hii, inayokuja wakati ambao Tanzania kama Taifa, lilimpokea rais mpya wa China, Xi Jinping katika ziara ya kikazi. Taasisi nyingine za kifedha zitambue umuhimu wa ushirikiano baina ya mataifa haya na kubuni huduma kama hizi,” alisema Dk Nagu.

Aliongeza kwamba, kwa kuwa harakati za kumkomboa Mtanzania zimeshika kasi, huku China ikijitoa kadri iwezavyo kuisaidia Tanzania, kuna haja huduma kama hizo za China Desk zikaambatana na mikakati endelevu ya kimandeleo, na taasisi nyingine nazo zinastahili kuiga.

Kwa upande wake, Balozi wa China hapa nchini, Lü Youqing, aliipongeza CRDB kwa kufuata nyayo za waasisi wa China na Tanzania, kiasi cha kubuni na kuzindua China Desk – dawati litakalowanufaisha wajasiriamali na wafanyabiara wa kila upande.

“Huduma hii ni harakati chanya inayofuata nyayo za waasisi wa ushirikiano baina ya China, Rais Mao Tse Tung na Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere. Vizazi na vizazi vitabaki kujivunia na kila mmoja atajisikia yu nyumbani anapokuwa katika moja ya nchi hizo,” alisisitiza Youqing.

COSMAS KIBUGA KUZICHAPA NA SWEET KALUU JUMALIPILI HII



Bondia mwenye makeke mengi na asiyekubali kushindwa ulingoni na , Cosmas Kibuga, anatarajia kupanda ulingoni siku ya jumapili wiki hii katika ukumbi wa Texas Manzese, kuzipiga na bondia mkongwe, Sweet Kalulu, katika pambano la kirafiki la kusherehekea  Pasaka. 
Akilizungumzia pambano hilo muandaaji wa mchezo huo, Miraji Msusa, alisema “burudani yetu ni kuangalia ngumi na kushangilia na najua ngumi nzuri zipo katika hawa mabondia wasio na majina na wenye upinzani mkali ,nikaonelea lazima katika sikukuu hii ya pasaka tusiiache ipite hivihivi bila kupata starehe yetu,  kusubiri mpaka tarehe 7 april kwenye pambano kubwa la pale ccm mwinjuma-mwanayamala  ni mbali, Nikaafikiana na cosmas kibuga na sweet kalulu ambao ni wapinzani mitaani wamalizie kiu yao hiyo''. alisema

MICHEZO YA UMISSETA WILAYA YA ILALA YAANZA KUTIMUA VUMBI


Shani Ally wa Benjamin akiwa na mpira

Mchezaji Marysiana Edga akijaribu kumtoka Shani Ally wa Benjamini

Wachezaji waliovaa nyekundu ni timu ya  cluster ya Benjamini na njano ni cluster ya Kinyerezi kabla ya mchezo ambao Benjamini walishind

Mchezaji Nusrat Msuya wa Kinyerezi akiwa na mpira wakati wa mchezo wao dhidi ya Benjamini kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Jangwani Wasichana
Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji kabla ya mchezo kuanza 
Mchezaji wa Benjamin akijaribu kutuliza mpira wakati wa mchezo dhidi ya Kinyerezi uwanja wa Azania
MASHINDANO ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) wilaya ya Ilala yameanza leo kwa michezo ya soka, netbali, kikapu, wavu na riadha kufanyika kwenye viwanja vya sekondari za Azania, Jangwani na Zanaki.

Kwenye viwanja vya Azania walianza kwa kufukuza upepo ambapo wasichana na wanavulana walikimbia  kwenye mbio za mita 100, 200 na 800 na washindi kupatikana.

Baadae ulifika wasaa wa soka ambapo timu za Beenjamin walicheza na Kinyerezi na mpaka Lenzi ya Michezo inatoka uwanjani hapo Kinyerezi ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 huku Cluster ya Upanga na Ilala wao wakiwa bado hawajafungana.

Kwa upande wa netbal Benjamini iliifunga Kinyerezi.

Awali akifungua mashindano hayo Mwenyekiti wa Umuja wa Wakuu wa shule za Sekondari za Ilala aliwataka wachezaji kuwa na nidhamu kwenye michezo kwani kama utashindwa darasani michezo inaweza kukuajiri.

BigRight YAWEKA MIKAKATI YA UBINGWA


Kampuni  changa ya Bigright Promotion inaanzisha mkakati wa kuwapiganisha mabondia  kwa ajili ya kugombania mikanda au kutetea mikanda yao isipotee.Ibrahim kamwe kiongozi wa kampuni hiyo alisema ” Tutaanzia kwa kuandaa ubingwa wa mapambano  ya uzito mdogo kabisa yaani light fly weight,baadae tunawaandalia fly weight na super fly  ,bantam …. .. ..mpaka heavy weight ,hiyo itawasaidia mabondia kupata mapambano ya mara kwa mara na kuwapatia kipato kidogo kwa ajira walioichagua inayoambatana na utambulishaji wa kimataifa kwa nchi yetu,kwani mchezo wa ngumi ni mchezo  mmojawapo unaoutangaza na kuipeperusha vema bendera ya nchi yetu kimataifa,bila ya watanzania wengi kulifahamu hilo ,hivyo kukosa usaidizi mzuri toka serikalini na taasisi binafsi tofauti na baadhi ya nchi za wenzetu zinazopenda na kuithamini michezo, Nchi nyingi zinatangazika  kupitia  michezo hadi sisi tunazifahamu na kuzitembelea  au kuwa na shauku ya kutaka kuzitembelea, wakati uwezo huo wa kufanya vizuri  tunao lakini hatusaidiwi kujinyanyua wala kuwa na sehemu ya kueleweka kwamba hii ni kwa ajili ya ngumi (ulingo wa kisasa na ukumbi wa uhakika),na wakati wadau wa mchezo huu tunanung`unika na kuhaha kutafuta wadhamini  nasi tujikwamue tokakatika hali tuliyonayo, kuna wengine wasio wastaarabu  watataka kuchukua nafasi hii kufanya ubadhilifu dhidi ya wanaosaidia-hii sio njema  na inadumaza michezo.
Kwa mfano mashindano yaliyo andaliwa na bigright tarehe 7 april mwananyamala hayana udhamini wala ufadhili wowote hivyo yanaendeshwa katika hali ya ugumu ili vijana nao wapate kucheza kuliko kufanya mazoezi ya muda mrefu bila mashindano hivyo kuwasababisha baadhi ya mabondia kukata tama na kuacha ngumi au kijiingiza katika vitendo vya ukabaji jambo ambalo sio jema na laweza kuepukika kwa kuwaandalia mashindano kama haya na ili azma yetu ya kuyafanya yaendelee yatubidi tushirikiane kwa kushawishi wafadhili, wadhamini au wapenda mchezo wenye uwezo kidogo wawe wanatuwezesha japo kidogo walichonacho ili nasi tuwe tunaongeza nguvu ya kupigania michezo isidorole,  mipango ikienda kama tulivyopanga tunategemea kila mwezi kuwashindanisha kugombania ubingwa na kila mwezi wa 12 kunakuwa na ligi ya mabingwa na kumzawadia mshindi  kitu ambacho atakuwa anakikumbuka katika maisha yake,hivyo  kwa alie tayari na mwenye mapenzi na maendeleo ya michezo tunaomba mchango wako uwe wa vifaa kama gloves,bandages,ballguard,headguard,gumshield,chakula ,nauli,ulingo na mengineyo mengi tu sijayaorodhesha,msitutenge na uwezo wetu mdogo tusaidiane
IBRAHIM ABBAS KAMWE

Mechi ya Azam yahamisha Bonanza la Wanahabari TCC


BONANZA la vyombo mbalimbali vya habari lililopangwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu viwanja vya Leaders Klabu likiandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), sasa litafanyika viwanja vya Sigara (TCC), Chang’ombe pia Dar es Salaam.

Uamuzi wa kuhamisha bonanza hilo umechukuliwa na sekretarieti ya TASWA kutokana na maombi ya waandishi wengi wa michezo kwa vile siku hiyo kuna mechi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika kati ya timu ya soka ya Azam na Barrack Young Controllers ya Liberia  itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam siku hiyo.

Azam ni timu pekee ya Tanzania iliyobaki kwenye michuano ya Afrika kwa ngazi ya klabu baada ya Simba na Jamhuri ya Pemba kutolewa katika raundi ya awali.
Tunaamini kwa bonanza kufanyika Sigara itakuwa rahisi kwa wadau wetu kushiriki kwenye bonanza na wale wengine watakaohitaji kwenda uwanjani wafanye hivyo wakitokea Sigara kwa hakuna umbali mrefu na kisha warejee kujumuika na wenzao mpaka mwisho.
Tunawaomba radhi kwa mabadiliko hayo, lakini yakiwa na lengo la kujenga na kuwa pamoja na wenzetu wa Azam kuhakikisha tunashirikiana nao kwa namna mbalimbali siku hiyo.
Bonanza hili linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) likiwa na lengo la kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja.
Bonanza hilo ambalo litahusisha wadau 1,500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari litaambatana na michezo mbalimbali itakayohusisha vyombo vyote vitakavyoshiriki na pia kutakuwa na burudani ya muziki kutoka katika moja ya bendi kubwa za muziki wa dansi hapa nchini, ambayo itatangazwa siku zijazo.
Nawasilisha
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA

CAG akabidhi Ripoti Kwa Rais Kikwete


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Bwana Ludovick Utouh akikabidhi Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2011-2012 kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Freddy Maro)
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...