Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, March 18, 2013

JEFFREY MATHEBULA NA TAKALANI NDLOVU KUAWANIA UBINGWA WA DUNIA
Mabondia wa Afrika ya Kusini, Jeffrey Mathebula na Takalani Ndlovu, wanatarajia kukutana ulingoni katika ukumbi wa Carnival City Casino jijini Johannesburg jimbo la Gauteng nchini Afrika ya Kusini katika pambano la mchujo (Elimination Title) la ubingwa wa dunia uzito wa unyoya (Featherweight).
 
Jeffrey Mathebula pichani (kushoto) na Takalani Ndlovu katika moja ya mapambano yao.
Wawili hao ni mahasimu wakubwa wanaojulikana nchini Afrika ya Kusini na walishakutana mara mbili ambapo Ndlovu alishhinda pambano la awali huku Mathebula akishinda pambano la mwisho.

Wakati huo huo mabondia, Vusi Malinga wa Afrika ya Kusini na Diarh Gabutan wa Phillipines watakutana katika mpambano mwingine wa mchujo kuwania tiketi ya kukutana na bingwa wa dunia katika uzito wa Bantam.

Promota maarufu wa Afrika ya Kusini Branco Milenkovic, wa kampuni ya Branco Boxing Promitions atakuwa ndiye mwandaaji wa mpambano huo unaotarajia kufanyika machi 23, mwaka huu.

Huu ni mwendelezo wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa IBF katika programu yake ua “Utalii wa Michezo” barani Afrika ambapo imejiwekea lengo la mapambano 100 ya ubingwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...