Marquee
Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!
tangazo
Monday, March 11, 2013
TASWIRA KATIKA MAONYESHO YA UTALII YA ITB BERLIN UJERUMANI LEO
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki akiwa katika mazungumzo na Rica Rwigamba Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Rwanda wakati alipokutana katika maonyesho ya dunia ya Utalii ITB yanayofanyika kwenye jengo la Messe Berlin jijini Berlin Ujerumani, Monyesho hayo yanahusisha makampuni yenye kutoa huduma mbalimbali za utalii duniani ambao hukutana na kutangaza utalii wa nchi zao huku wakifanya makubaliano na kuingia mikataba mbalimbali ya kuuziana bidhaa za kitalii, Maonyesho hayo yanamalizika rasmi leo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya ndege ya Flightlink Capt. Munawer Dhirani akizungumza na
Ibrahim Mussa Mkurgenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii
katikati ni
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula
akisikiliza kwa makini wakati Balozi huyo alipotembelea katika banda la Tanzania kwenye maonyesho ya ITB yanayomalizika leo jijini Berlin Ujerumani kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki .(PICHA NA FULLSHANGWEBLOG)
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Geofrey Meena kushoto akitembelea Banda la Kampuni ya Pongo Safaris katika maonyesho ya Utalii ya ITB, wengine kutoka kulia ni Marlon Van Hee Meneja Mradi wa kampuni ya ECEAT PROJECTS ya Uholanzi ,Julias Alexander Pundo Mwakilishi wa kampuni ya Ramogi Tours & Travel Limited Jumuiya ya Ulaya na Cynthia Ponera Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Pongo Safaris
Wadau wa Ujerumani hawakukosa kutembelea maonyesho hayo hapa walikuwa wakipata Menyu wakati wa hafla ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Team Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kazi kubwa ya kuuza utalii wa Tanzania kwenye maonyesho hayo.
Nami nikajichanganya kwenye Banda la Pongo Safaris na Ramogi Tours hapa nikipata picha na Julius wa Ramogi Tours pamoja na Cynthia wa Pongo Safaris
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya ndege ya Flightlink Capt. Munawer Dhirani wakati walipokutana katika maonyesho hayo
Huu nao ulikuwa ni utalii wa aina yake katika maonyesho hayo ambapo watu mbalimbali walikuwa wakipiga nao picha kwa ajili ya kumbukumbu zao
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment