Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 21, 2013

Z. ANTO KUTOA KAZI MPYA SIKU YA PASAKA

Na Elizabeth John

BAADA ya kuwa kimya kwa muda mrefu, mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ally Mohamed ‘Z. Anto’ usiku wa Pasaka anatarajia kutambulisha kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Tanzania’.
Akizungumza Dar es Salaam, Z.Anto alisema kazi hiyo ataitambulisha katika ukumbi wa Mnyaru nite club uliopo jijini Arusha.
“Nashukuru mungu kwa kupata shoo hii ambayo itanipa nafasi ya kuitambulisha ngoma yangu mpya, tukiwa na kundi zima la Solid Ground Famili kutoka Mabimbo jijini Dar es Salaam,” anasema.
Z.Anto anawaomba wakazi wa Arusha wajitokeze kwa wingi siku hiyo ili waweze kupata burudani iliyoenda shule kutoka kwake na kundi hilo ambalo lililiteka soko la muziki huo kipindi cha nyuma.
Mkali huyo alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Kisiwa cha Malavidavi’ licha ya kuwa na vibao vingi ambavyo vilivyofanya vizuri katika soko la muziki huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...