Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 21, 2013

KIBA KUACHIA VIDEO MPYA
Na Elizabeth John

BAADA ya kutamba na kibao chake cha ‘Kidela’, mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdukarim Kiba ‘Abdukiba’ anatarajia kuachia video ya kibao hicho hivi karibuni.
Mbali na ‘Kidela’ Abdukiba alishawahi kutamba na vibao vyake kama, Kizunguzungu, Demu sio na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Abdukiba alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho ambacho anatarajia kukisambaza wiki ijayo.
“Namshukuru mungu kazi hii imepokelewa vizuri na mashabiki wangu nab ado inaendelea kufanya vizuri, naomba tu wapenzi wangu wasichoke kunipa sapoti bado kuna vitu vizuri ambavyo nimewaandalia,” alisema.
Abdukiba alisema, video hiyo amefanya na mtayarishaji maarufu nchini Adamu Juma, ambapo yeye ndio ameandaa mazingira ambayo wamefanyia kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...