Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 29, 2013

UCHAGUZI MIKUU BFT KUFANYIKA JIJINI MWANZA


Viongozi wa sasa BFT, Rasi Joan Minja (kulia) na Katibu Mkuu, Mashaga makore

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Mchezo wa Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) unatarajiwa kufanyika Mei mwaka huu jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa BFT, Mashaga Makore, aliiambia MICHARAZO asubuhi ya leo kuwa, kuwa uchaguzi huo utafanyika mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kimataifa ya Majiji yanayotarajiwa kufanyika jijini humo kati ya Mei 20-25.
Makore alisema mchakato wa kuelekea kwenye kinyang'anyiro hicho ambacho kitatanguliwa na Mkutano Mkuu wa shirikishi hilo utatangazwa mara baada ya shamrashamra za sikukuu ya Pasaka.
"Uchaguzi Mkuu wa BFT utafanyika mwezi Mei jijini Mwanza mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya kimataifa ya ngumi inayoshiriki miji mikuu ya Afrika Mashariki na Kati, ambapo utatanguliwa na Mkutano Mkuu," alisema Makore.
Makore alisema maamuzi hayo yalifikiwa na Kamati yao ya Utendaji iliyokaa hivi karibuni na kutoa wito kwa wadau wa mchezo huo wenye uwezo na sifa za kuongoza shirikisho hilo kujiandaa kuijitosa kuwania uongozi kwenye uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...