Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 19, 2013

TWIGA STARS FULL DISPLINE, HAKUNA KUVAA MILEGEZO AU STAILI ZA NYWELE ZA KIHUNI, WENYEWE WAMKUBALI KOCHA KAIJAGE


WACHEZAJI wa timu Taifa ya wanawake “Twiga Stars” wamemgaya kocha Rogasian Kaijage, waanza kutii masharti yake.
Wachezaji hao ambao walikuwa wanakata nywele kwa staili za ajabu na uvaaji wa surulia na pensi kwa staili ya mlegezo wameonekana kubadilika baada ya kuwa na kocha mpya kwenye kikosi chao.
Kaijage ambaye amerithi mikoba ya Boniface Mkwasa baada ya kubwaga manyanga mwaka jana alipoita timu hiyo alikaa nao kikao na kuwaeleza kuwa hatapenda kuona wachezaji hao wakivaa staili ambazo zinaleta picha mbaya kwa jamii.
“Niliwaambia mpira unahitaji uwe na adabu ili ufanikiwe hivyo niwaambia wabadilike kuanzia muonekana hadi uwanjani na ndio maana unawaoneka wamesuka vizuri na kubana nywele vizuri na kuvaa nguo sawasawa”, alisema Kaijage
LENZI YA MICHEZO ilishuhudia wachezaji wakiwa nadhifu kuanzia kwenye mavazi hadi kichwani na wakifanya mazoezi kwa ari na kocha anapoita timu kila mtu anakimbia kuwahi kufika siyo kutembea wala utani ambao hauna tija.
Naye meneja wa timu hiyo Furaha Francis amefurahishwa na kitendo cha kocha kuwaeleza ukweli wachezaji kuwa nidhamu inaanzia kwenye muonekano kwa jamii.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...