Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 26, 2013

WABUNGE ZITTO KABWE, IDD AZAN NA WENZAO WAHITIMU MAFUNZO YA AWALI YA JKT KAMBI YA MGAMBO 835KJ


Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe pamoja na Wabunge wenzake kadhaa vijana leo wamemaliza rasmi mafunzo yao ya awali ya JKT katika kambi ya Mgambo 835 KJ iliyopo Mkoani Tanga.

Pichani juu ni Zitto Kabwe akijiandaa kwenda katika gwaride la mwisho na picha chini akiwa shambani pamoja na Mbunge mwenzake  Iddi Azan, Abdallah haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa wakiwa katika kambi ya Mgambo 835KJ.

 Zitto Kabwe, amesema amefurahishwa na mazoezi na mafunzo yatolewayo ya kambi hiyo na kuwapongeza wale wote waliyowahi kupia mafunzo hayo ambapo leo anahitimisha  mafunzo hayo na kujiwekea historia ya kubwa katika maisha yake.
Baadhi ya Wabunge waliohitimu mafunzo hayoleohii, Zitto Kabwe, Iddi Azan, Abdallah haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa, wakiwa katika moja ya shamba darasa la kambi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...