Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, March 18, 2013

SUPER D KUMPIKA KING CLASS MAWE KWA AJILI YA MEI MOSI

Na MWANDISHI WETU
BONDIA Ibrahimu  Class 'King Class Mawe' ameingia kambini kujiandaa 
kumkabili Amosi Mwamakula katika pambano la utangulizi wakati wa
mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.
Pambono la raundi nane linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA
Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu, linatarajiwa kuwa la vuta
nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.
Kocha wa King Class Mawe, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa
bondia wake ameingia kambini juzi kujiandaa kumchakaza Mwamakula ili
kuendelea kujiwekea rekodi nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya
vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na  Mashali" alisema
Super D.
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa
katika mchezo huo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mjapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe.
   

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...