Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, March 24, 2013

POULSEN " Bado sijajua kama wataniongezea muda mwingine," http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2012/05/Kim-Poulsen1.jpg

Zikiwa zimebaki siku 59 kumalizika kwa mkataba wa kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen, Mdenmark huyo amesema hana uhakika wa kuendelea kuinoa timu hiyo ya taifa kwavile waajiri wake, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), hawajamueleza chochote kuhusu suala la kuongezwa muda.

Akizungumza katika mahojiano maalum na jijini Dar es Salaam jana, Poulsen amesema mkataba wake na TFF unamalizika Mei 15 na kwamba hana uhakika kama atapewa mkataba mpya wa kuinoa Stars.

"Ni takriban miezi miwili imebaki mkataba wangu umalizike. Bado sijajua kama wataniongezea muda mwingine," .

"Naweza kuzungumza na timu nyingine lakini napenda niendelee kuifundisha Taifa Stars," alisema zaidi Poulsen akijibu swali kama ameshafanya mazungumzo na timu nyingine kwa ajili ya kuzinoa.

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah amesema  kuwa uongozi unatambua kwamba mkataba wa Poulsen unaelekea ukingoni na kwamba wanatarajia kuzungumza naye baada ya kupokea ripoti ya kamati ya ufundi ya shirikisho hilo kuhusu utendaji wa kocha huyo.

Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni amesema ripoti ya utendaji wa kocha huyo ipo tayari na wanatarajia kuiwasilisha muda wowote ili ijadiliwe kabla ya kutoa maamuzi ya kuendelea ama kutoendelea naye.

Poulsen alisaini mkataba wa mwaka mmoja Mei 11 mwaka jana kuinoa Stars akirithi mikoba ya kocha Jan Poulsen ambaye pia ni raia wa Denmark.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...