Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, September 27, 2019

BONDIA MAKUBI ATAMBA KUMPIGA ABDALLAH MA MOROGORO OKTOBA 4 KATIKA UKUMBI WA 361 MWENGE


Na Mwandishi wetu 

Bondia Ibrahim Makubi yupo kambini kwa ajili ya mazoezi yake ya kumkabili bondia abdallah kingolwira  wa ( morogoro ) katika pambano lake litakalo fanyika Oktoba 4 katika ukumbi wa 361 uliopo mwenge jeshini mpambano huo ambao umewekwa kwa ajili ya kupandisha viwango mabondia mbalimbali litakuwa ni sehumu moja ya kuwapongeza mabondia

waliofanya vizuri nje ya nchi na kurudi na mikanda mikubwa nchini miongoni mwa mabingwa hao ni Abdalah Pazi ,Tonny Rashidi ,Bruno Vifua Viwili mabondia hawo wameleta mikanda hiyo nchini ndani ya mwezi mmoja tu

Makubi ametamba kumsambalatisha bila huruma yoyote ile Abdalah wa morogoro kwani ushindi wake ndio utakao msafishia njia ya kwenda juu zaidi katika mapambano ya ngumi anajua kuwa ngumi sio mchezo raisi kama ilivyo kwa michezo mingine

nae kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' anaemnowa na kumtafutia mambambano kwa ajili ya kumpandisha Daraja bondia huyo amesema kwa sasa makubi kila pambano lake kwake ni fainal kwani hapa kazi tu No Pain No Gain tutaakikisha tunashinda kila pambano na mpaka atakuwa bingwa wa mabingwa nchini na Duniani alisema Kocha  Super d

BONDIA JUMA CHOKI SASA AWAZIA UBINGWA WA TAIFA BAADA YA KUWA KING OF THE RING


NA MWANDISHI WETU

BONDIA Juma Choki Baada ya kumgalagaza bila ya huruma Emanuel Mwakyembe na kuchukua ubingwa wa King Of The Ring 2019 katika uzito wa KG 58 amesema ato bweteka kwa kuwachua ubingwa huo 

ambapo alipewa zawadi ya pikipiki pamoja na kitita cha shilingi laki tano amesisitiza ato bweteka kwa kuwa bingwa wa mashindano hayo ata hivyo ameomba kuwa andaliwe ubingwa wa taifa ndio matarajio yake kwa sasa akichukuwa ubingwa wa taifa kisha ataenda juu kuchukuwa ubingwa wa Afrika arafu ubingwa wa Dunia

Bondia huyo mwenye ndoto ya kuwa bingwa wa Dunia kupitia mchezo wa masumbwi nchini Tanzania kwa kuchukuwa mikanda nje ya nchi na kuletea sifa Tanzania 

Akizungumza kocha wake ambaye ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa choki ni bondia mzuri na malengo yake ni kufika mbali na kweli atafika anapo pataka kwani kwenye nia pana njia

ikumbukwe kuwa mimi ndio nimewatoa mabondia mabingwa wa dunia ambao wamepita katika mikono yangu kama vile Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Idd Mkwela Vicent Mbilinyi Sunday Kiwale Ibrahimu makubi ambaye kwa sasa yupo mazoezini akijiandaa na mpambano wake na abdallah kingolwira wa morogoro pambano litakalofanyika Oktoba 4 katika ukumbi wa 361 mwenge pale jeshini

hivyo nina uwakika na mabondia wangu wote ninaowafundisha na siku zoto sinaga kazi mbovu

NGUMI KUPIGWA IJUMAA OKTOBA 4 UKUMBI 361 MWENGE

NGUMI KUPIGWA IJUMAA OKTOBA 4 UKUMBI 361 MWENGE

Mabondia wa mgumi za kulipwa nchini walioibuka na ushindi wanatarajia kushiriki katika sherehe za kupongezwa na mashabiki wao Oktoba Nne Club 361Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Mratibu mkuu wa Pambano la kuwapongeza mabondia hao Selemani Semunyu alisema mipango imekamilika ikiwemo mabondia watakaocheza ingawa maombi ni mengi ya mabondia wengi kutaka kushiriki kuonyesha furaha yao na kuwaunga mkono mabondia wenzao .
Aliwataja miongoni mwa mabingwa hao ni Abdalah Pazi ,Tonny Rashidi ,Bruno Vifua Viwili na Nassib Ramadhani kwa pamoja na bondia yeyote bingwa na wameletea taifa heshima kubwa wadau na mashabiki hakuna budi kuwapongeza.

" Serikali na Wabunge wamewapongeza lakini wadau na mashabiki sasa huu ndio wasaa wa kuwapongeza hata kama kuna zawadi ya kuwapa hii ndio sehemu moja lakini sie tunawapongeza kwa pambano" Alisema Semunyu.
Aliongeza kuwa pambano hili pia litatumika kupata mabondia watakaowania mikanda mwezi Desemba ambapo litafanyika pambano la funga mwaka.
" Watakaofanya vizuri katika pambano hili wataweza kupata nafasi katika pambano la mwezi wa 12 ambapo historia ya Ngumi nchini kwa kipindi cha hivi karibuni itawekwa " Alisema Semunyu.
Pia amewashukuru kamisheni ya ngumi za kulipwa kutoa kibali kwa wadhamini Smart Gin na kuomba wadhamini wengine kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha kurejesha hadhi ya mchezo wa ngumi nchini.
Kwa upande wake mratibu wa kiufundi wa mapambano hayo Yassin Abdalah Ustaadh aliwataja mabondia watakaosindikiza sherehe hiyo kuwa ni issa nampechehe (Dsm) vs alli hamisi (morogoro )
Ibrahim Makubi (Dsm)vs abdallah kingolwira ( morogoro )Maganga kulwa (mbagala) vs Said Sudi (M'nyamala) )Hashimu msungo vs Epson john Lewis Salumu omari vs ramadhani chicho
Aliongeza kuwa mapambano yanaweza kuongezeka kutokana na mabondia wengine kutafuta nafasi ya kutaka kushiriki Desemba lakini wengine nao wanataka kushiriki kuonesha furaha ya ushindi huo

Saturday, September 14, 2019

MABONDIA JUMA CHOKI NA EMANUEL MWAKYEMBE WAPIMA UZITO KUPIGANA KESHO SEPTEMBA 15 MASAKI


Bondia Juma Choki akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Emanuel Mwakyembe utakaofanyika katika ukumbi wa Backet Lounger Septemba 15 kushoto ni katibu wa Kamisheni ya ngumi Tanzania TPBRC Yahya Pori

Bondia Juma Choki akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na mpinzani wake Emanuel Mwakyembe kulia mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Backet Lounger Septemba 15 Jumapili 

Bondia Juma Choki na Emanuel Mwakyembe wakitunisha misuli mbelew ya kamera mabondia hawo wamepima uzito na Afya kwa ajili ya mpambano wao wa Septemba 15 katika ukumbi wa Bucket uliopo Masaki jumapili hii

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila Super D kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Jumachoka na kocha Edward Lwiyakwipya na bondia Emanuel Mwakyembe


NA Mwandishi wetu

MABONDIA Juma Choki na Emanuel Mwakyembe wamepima uzito kwa aqjili ya mpambano wao kwa ajili ya mpambano wa King Of The Ring utakaofanyika Septemba 15  katika ukumbi wa Backet Lounger uliopo Masaki Dar ES salaam

Mabondia hawo wamefanikiwa kufika Fainal baada ya kuwashinda wapinzani wao katika hatua za awali mshindi katika mpambano huo atanyakuwa pikipiki pamoja na kitita cha shilingi laki tano na atakaepigwa atachukuwa flat TV kubwa pamoja na kitita cha shilingi laki tano

Promota wa Mpambano huo Crisiani Kisinini amesema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ambapo bondia Issa Nampepeche atazipiga na Emanuel Timtimu na mabondia wengine wengi


Aliongeza kwa kusema kuwa mapambano ya ngumi yataanza saa moja kamili usiku  uki kila likipigwa pambano moja kunakuwa na burudani na mpambano wa mwisho kabisa utafanyika saa tano na saa sita itakuwa mwisho na atajulikana nani ni champion wa mashindano ya King Of The Ring ambapo Mshindi wa kwanza mpaka wa tatu watajinyakulia zawadi kubwa

Mshindi wa kwanza ataondoka na Pikipiki pamoja na laki tano pesa taslim na wa pili atajinyakulia flat TV kubwa pamoja na Laki tano wa tatu atachukuwa kiasi cha pesa Taslim shiling Laki Tano

Hivyo amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi waje waangalie nani bingwa katika uzito wa KG 58 kwa hapa nchini Tanzania

Tuesday, September 10, 2019

JUMA CHOKI AJIFUA KUMKABIRI MWAKYEMBE SEPTEMBA 15


Bondia Juma Choki kushoto akioneshana umwamba na bondia wa Kimataifa ambaye alishawai kuishi nchini Marekani miezi takribani 8 kwa ajili ya mchezo wa masumbwi nchini humu Ibrahimu Class 'KING CLASS MAWE' Choki anajiandaa na mpambano wake wa fainal dhidi ya Emanuel Mwakyembe septemba 15 katika ukumbi wa bucket club uliopo Masaki Dar es salaam

Bondia Juma Choki kushoto akioneshana umwamba na Ibrahimu Makubi wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Super D Coach iliyopo kariakoo

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana umwamba na Juma Choki wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kamba ya Super D coach Shule ya Uhuru Dar es salaam Jana


Bondia Alex Kachelewa kushoto akitupiana makonde na Juma Choki wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Super D coach shule ya Uhuru 


Bondia wa Kimataifa nchini Tanzania ambaye alishawai kuka nchini Marekani kwa Takribani ya miezi nane kwa ajili ya mcheszo wa masumbwi Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto' akioneshana umwamba na Juma Choki anayejiandaa na mpambano wake dhidi ya Emanuel Mwakyembe utakaofanyika septemba 15 katika ukumbi wa Backet club ulipo masaki


Bondia wa Kimataifa nchini Tanzania ambaye alishawai kuka nchini Marekani kwa Takribani ya miezi nane kwa ajili ya mcheszo wa masumbwi Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto' akioneshana umwamba na Juma Choki anayejiandaa na mpambano wake dhidi ya Emanuel Mwakyembe utakaofanyika septemba 15 katika ukumbi wa Backet club ulipo masaki


Na Mwandishi Wetu

Bondia Juma Choki anaye jiandaa na mbambano wake dhidi ya Emanuela Mwakyembe septemba 15 katika ukumbi wa bucket Clab uliopo Masaki jijini Dar es es salaam amejinasibu kumtwanga bondia huyo na kuchukuwa ubingwa wa king of The Ring 

akijinasibu bondia huyo alivyotembelewa kambini kwake kwa Super D Coach iliyopo shule ya Uhuru Jijini Dar es salaam 

Amesema kuwa mwakembe ana uwezo wa kukanyaga moto wake ata siku moja huko alikutana na viande sasa kaja kwenye kazi kazi hapo  ndipo pa kuoneshana uwezo kama anavyosemaga kocha Super D Kazi Kazi No Pain No Gain yani siku hiyo patachimbika hivyo mwakyembe ajipange sana kwana mazoezi ninayofanya na mbinu ninazofundishwa sio za kitoto hatari tupu

Nae kocha wa bondia huyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema hii ni vita kubwa sana kwa kuwa kocha wa mwakyembe  Edward Lwiyakwipya wamesoma nae pamoja katika ngazi kubwa ya kozi ya kimataifa hata hivyo mimi nina mbinu nyingi zaidi yake ata hivyo nita akikisha napata ushindi usiokuwa wa kuwachosha majaji hivyo matumaini yangu ni kumpiga k,o mbaya zaidi

ikumbukwe kuwa mabondia wote wenye viwango vya juu nchini wanatoka kwangu ukiangalia mabondia wote wakubwa wanatoka kwangu na wana viwango vya kimataifa hivyo najivunia kwa hilo ukiangalia mabondia wanaotoka kwangu akuna ata mchovyu mmoja alijinasibu Super D

Aliongeza kwa kusema mikono yake wamepita mabondia wengi sana akiwemo Sanday Kiwale, Idd Mkwera Vicent Mbilinyi Ibrahimu Class' King Class Mawe' Shomali Milundi  Shabani Kaoneka na mabondia mbalimbali nchini wote wamepita katika mikono yangu kwa njia moja au nyingine hapa ndio No Pain No Gain kazi kazi hivyo wapenzi wa ngumi muje kwa wingi kuangalia kazi hii ambayo aita muacha mtu salam
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...