Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 14, 2019

MABONDIA JUMA CHOKI NA EMANUEL MWAKYEMBE WAPIMA UZITO KUPIGANA KESHO SEPTEMBA 15 MASAKI


Bondia Juma Choki akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Emanuel Mwakyembe utakaofanyika katika ukumbi wa Backet Lounger Septemba 15 kushoto ni katibu wa Kamisheni ya ngumi Tanzania TPBRC Yahya Pori

Bondia Juma Choki akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na mpinzani wake Emanuel Mwakyembe kulia mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Backet Lounger Septemba 15 Jumapili 

Bondia Juma Choki na Emanuel Mwakyembe wakitunisha misuli mbelew ya kamera mabondia hawo wamepima uzito na Afya kwa ajili ya mpambano wao wa Septemba 15 katika ukumbi wa Bucket uliopo Masaki jumapili hii

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila Super D kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Jumachoka na kocha Edward Lwiyakwipya na bondia Emanuel Mwakyembe


NA Mwandishi wetu

MABONDIA Juma Choki na Emanuel Mwakyembe wamepima uzito kwa aqjili ya mpambano wao kwa ajili ya mpambano wa King Of The Ring utakaofanyika Septemba 15  katika ukumbi wa Backet Lounger uliopo Masaki Dar ES salaam

Mabondia hawo wamefanikiwa kufika Fainal baada ya kuwashinda wapinzani wao katika hatua za awali mshindi katika mpambano huo atanyakuwa pikipiki pamoja na kitita cha shilingi laki tano na atakaepigwa atachukuwa flat TV kubwa pamoja na kitita cha shilingi laki tano

Promota wa Mpambano huo Crisiani Kisinini amesema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ambapo bondia Issa Nampepeche atazipiga na Emanuel Timtimu na mabondia wengine wengi


Aliongeza kwa kusema kuwa mapambano ya ngumi yataanza saa moja kamili usiku  uki kila likipigwa pambano moja kunakuwa na burudani na mpambano wa mwisho kabisa utafanyika saa tano na saa sita itakuwa mwisho na atajulikana nani ni champion wa mashindano ya King Of The Ring ambapo Mshindi wa kwanza mpaka wa tatu watajinyakulia zawadi kubwa

Mshindi wa kwanza ataondoka na Pikipiki pamoja na laki tano pesa taslim na wa pili atajinyakulia flat TV kubwa pamoja na Laki tano wa tatu atachukuwa kiasi cha pesa Taslim shiling Laki Tano

Hivyo amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi waje waangalie nani bingwa katika uzito wa KG 58 kwa hapa nchini Tanzania

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...