Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, September 27, 2019

BONDIA MAKUBI ATAMBA KUMPIGA ABDALLAH MA MOROGORO OKTOBA 4 KATIKA UKUMBI WA 361 MWENGE


Na Mwandishi wetu 

Bondia Ibrahim Makubi yupo kambini kwa ajili ya mazoezi yake ya kumkabili bondia abdallah kingolwira  wa ( morogoro ) katika pambano lake litakalo fanyika Oktoba 4 katika ukumbi wa 361 uliopo mwenge jeshini mpambano huo ambao umewekwa kwa ajili ya kupandisha viwango mabondia mbalimbali litakuwa ni sehumu moja ya kuwapongeza mabondia

waliofanya vizuri nje ya nchi na kurudi na mikanda mikubwa nchini miongoni mwa mabingwa hao ni Abdalah Pazi ,Tonny Rashidi ,Bruno Vifua Viwili mabondia hawo wameleta mikanda hiyo nchini ndani ya mwezi mmoja tu

Makubi ametamba kumsambalatisha bila huruma yoyote ile Abdalah wa morogoro kwani ushindi wake ndio utakao msafishia njia ya kwenda juu zaidi katika mapambano ya ngumi anajua kuwa ngumi sio mchezo raisi kama ilivyo kwa michezo mingine

nae kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' anaemnowa na kumtafutia mambambano kwa ajili ya kumpandisha Daraja bondia huyo amesema kwa sasa makubi kila pambano lake kwake ni fainal kwani hapa kazi tu No Pain No Gain tutaakikisha tunashinda kila pambano na mpaka atakuwa bingwa wa mabingwa nchini na Duniani alisema Kocha  Super d

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...