Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 18, 2021

BONDIA RAMADHANI MIGWENE AMUWEKEA MIKWALA ALBANO CLEMENT BAADA YA KUKIMBIWA NA HABIBU PENGO

BONDIA RAMADHANI MIGWEDE baada ya kukimbiwa na mpinzani wake Habibu Pengo aliesaini nae kuzipiga mara ya kwanza sasa amebadilishiwa mpinzani na atacheza na bondia machachali kutoka mlandizi Albano Clement Desema 3 mpambano wa raundi nae utakaofanyika katika uwanja wa Kinesi uliopo Shekilango jijini Dsar es salaam akiongea wakati wa kutambulisha mpambano wa rasmi Migwede amesema kuwa yeye ni bondia hivyo uwezo wake una mruhusu kucheza na mtu yoyote atakaekuwa mbele yake ili mradi walingane uzito tu aliongeza kwa kusema unajua mimi ni bondia hivyo kazi yangu mimi ni kupigana hivyo siwezi kuacha kupigana kwa sababu Pengo kanikimbia hii ni kazi kama kazi nyingine nimepewa kazi na Albano hivyo ajipange kwa kuwa kipigo nitakachompa ni cha mbwa mwizi mimi ni mtu mwingine kabisa niwapo ulingoni hivyo ajitahalishe sasa sijui mwenzie kaona nini mpaka kakimbia na mimi naishi huyu kadandia treni kwa mbele sasa kipigo nitakachompatia atashindwa kuhadithia nae Clement amesema kuwa yeye ni bondia na ngumi ni kazi yake hivyo kazi kazi watakutana ulingoni sdiku hiyo mimi nimewapiga mabondia wakubwa kuliko yeye nimempiga Saidi Mundi kutoka Tanga bondia ambaye ni hatari sana kwa tanzania lakini nimemkalisha na cha moto kakiona nimemtwanga bila huruma bondia Seba Temba kutoka Morogoro na yeye alikuwepo katika mpambano huo sasa sidhani katika raundi nane hizo hatamaliza yote kwa yote mikono yangu ndio itakayo amua mpambano uho mbali na mpambano uho unaosubiliwa kwa hamu siku hiyo pambano ilingine kali litawakutanisha mabondia machachali Muksin Swalehe ;Alkasusu; na Cosmas cheka mabondia ambao walikuwa wakitafutana kwa mda mrefu sasa kumaliza ubishi Desemba 3 katika uwanja wa kinesi

Monday, October 11, 2021

BONDIA RAMADHANI MIGWEDE ASAINI KUZIPIGA NA HABIBU PENGO OKTOBA 12 AWAITA MASHABIKI WA CHANIKA KUJITOKEZA SIKU HIYO

NA MWANDISHI WETU BONDIA RAMADHANI MIGWEDE amesaini mkataba wa kuzipiga na Habibu Pengo Novemba 12 mpambnano wa raundi kumi utakaofanyika jijini Dar es salaam akizungumza na wahandishi wa habari kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa Migede kasaini mkataba uho mbele ya katibu wa kamisheni ya ngumi za kulipwa Yahya Poli mpambano utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao bondia huyo mwenye maskani yake chanika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam atapambana na Pengo mpambano ambao utakuwa autabiliki kwani mabondia wote hawo wana uzoefu mkubwa katika mchezo wa masumbwi mbali na uzoefu waliokuwa nao pia wamekuwa wakiwapa vipondo wapinzani wao kadri wakutanapo nao ulingoni ambapo bondia migwede hivi karibuni alimchakaza vibaya tena bila huruma bondia keis ally kwa k,o ya raundi za awali nae Pengo amekuwa tishio katika kipindi cha hivi karibuni kwani alikuwa akicheza mapambano makubwa na yenye msisimko zaidi na kufurahisha mashabiki awapo ulingoni Pengo mwenye mashabiki luluki katika kitongoji cha mabibo na viunga vyake vya jirani amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuja kuangalia mchezo uho bila ya kukosa nae Migwede amesema alikuwa anamtafuta sana Pengo kwa udi na uvumba hivyo kwa sasa kaingia katika choo cha watoto hivyo kaingia katika 18 zangu hivyo nawaomba mashabiki wake wote wajitokeze kwani siku hiyo atafanya atakachotumwa na mashabiki zake wa chanika pamoja na vitongoji vya jirani hivyo wasikose kuja

Monday, October 4, 2021

DULA MBABE ULINGONI TENA OKTOBA 9 P.T.A SABASABA CHEKA NDANI NAE SIKU HIYO

DULA MBABE ULINGONI TENA OKTOBA 9 P.T.A SABASABA CHEKA NDANI NAE SIKU HIYO NA MWANDISHI BONDIA ABDALLAH PAZI 'DULLA MBABE' atapanda ulingoni kwa ajili ya mpambano wake mwingine zidi ya Alex Kabangu kutoka DRC YA kONGo katika mpambano wa Raundi kumi akizungumza jijini Dar es salaam promota wa mpambano uho Kaike Siraju amesema kuwa pambano hilo la kimataifa litafanyika katika ukumbi wa P.T.A Saba saba siku ya kumamosi hivyo wapenzi na mashabiki wa mchezo wa masumbwi wanapaswa kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwani wameandaa ngumi zitakazoleta burudani ya kutosha siku ya Oktoba 9 Kaike aliongeza kwa kusema kuwa siku ya jumatano bondia kutoka Kongo Alex Kabangu atapokelewa na kufanya mahojiano na wahandishi wa habari za michezo siku hiyo hiyo katika uwanja wa ndege wa kimataifa hivyo amewaomba mashabiki kujitokeza katika mpambano uho aliongeza kwa kusema kuwa siku ya ijumaa itakuwa ni kwa ajili ya kupima uzito na afya kwa mabondia hawo ambapo eneo la kupimia uzito ni katika viwanja vya Las Vegas vilivyopo mabibo sokoni hivyo mashabiki wotenaopmbwa kuja kushudia tukio hilo la upimaji uzito pamoja na Afya kwa mabondia ambapo tutaanza saa nne kamili asubui mpaka saa sita na nusu tutakuwa tumesha maliza mbali na mpambano uho kutakuwa na pambano lingine machachali litakalo wakutanisha bondia Cosmas Cheka kutoka Morogoro na Issa Nampepeche kutoka Dar es salaam wakizungu8mza kuhusu mpambano wake uho bondia Nampepeche amesema yeye ni bondi hivyo amejiandaa vizuri na matarajio yake ni ukushinda kwa .K.O ambayo aita wapa tabu majaji nae cheka amesema kuwa yeye ana wasiwasi kwani mazoezi kwake kama dawa kutwa mara tatu hivyo mpinzani wake ajipange

Monday, August 30, 2021

BONDIA IBRAHIMU CLASS AMTAMBIA NASSIBU RAMADHANI KUWA SEPTEMBA 24 ATAMPIGA KWA K,O

 


 

NA MWANDISHI WETU

 

BONDIA Ibrahimu Class ‘king Class Mawe’ amesema kuelekea katika mpambano wake na Nasibu Ramadhani Septemba 24 atokuwa na msalie mtume kutokana na Nasibu kuwa na maneno sana hivyo baasi anataka akate ngebe kwa kumpiga K.O mbaya sana ambayo aijawai kutokea

 

Katika maisha ya ngumi kwani ndio itakuwa mwisho wake wa kucheza mchezo wa masumbwi nchini hivyo basi naomba wapenzi wa mchezo wa masumbwi waje kuangalia mpambano wa kihistoria nitakaopambana na nasibu mana nimepania kucheza mchezo mzuri ambao utawafurahisha na kuwaburudisha wapenzi wa mchezo wa masumbwi nchini

 

Alijimwambafai Class ata hivyo mpambano uho wa raindi kumi unaosubiliwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa ngumi nchini umekuwa ukoingelewa kila kukicha na wapenzi mbalimbali wa mchezo huo wa masumbwi

Nae bondia Nassibu Ramadhani alijibumapigo kwa kusema kuwa kwa sasa Class atoboi kwani mpambano wa mara ya kwanza alibebwa na majaji hivyo kwa sasa nimemuandalia kipigo kitakatifu ambacho ato kisaau maishani mwake

 

Na mimi uwaga kwangu ni vitendo tu sinaga mambo mengi katika mchezo wa  ngumi mimi ndio sinaga mda wa kuongea ongea kumaliza maneno na kubwabwaja hovyo

 

Nae promota wa mpambano huo Rajabu Mhamila ‘Super D’ kutoka katika kampuni Tanzu ya Kizalendo ya Super D Boxing Promotion wamejipanga kuwaletea mapambano yenye tija kwa mabondia na yenye upinzani mkubwa ili wapenzi wa mchezo wa masumbwi wapate burudani

 

Aliongeza kwa kusema kuwa siku hiyo wameandaa mapambano saba yatakayopigwa siku hiyo uku tukiwa tumesha wasainisha mabondia Juma Choki atakaezipiga na Issa Nampepecvh mpambano wa raundi nane

 

Na tatali wamesha wasainisha mabondia vicent mbalinyi atakaezipiga na Shedrack Ignas wakati Waziri Rosta atakuwa akizipiga na Anuary Mlawa na Albano Clement atazipiga na Ramadhani Migwede na kwa upande wa kina dada bondia Agnes Kayange atazichapa na Lulu Kayage mpambano wa raundi siti na bondia Daudi Mwita atakuwa akizipiga na Saidi Ndilimo

Tuesday, August 3, 2021

MABONDIA CLASS NA NASSIBU WAPIGWA PINI NA SUPER D BOXING PROMOTION

 


 


NA MWANDISHI WETU


PROMOTA wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amewapiga pini mabondia Ibrahimu class na Nasibu Ramadhani kwa kuingia nao Mkataba wa kuzipiga Septemba 24 jijini Dar esa Salaam 


Akizungumza baada ya kuingia mkataba na mabondia hao uliotiwa saini mbele ya rais wa kamisheni ya ngumi za kulipwa TPBRC Agapeter Basili zilizopo keko Dar 


Super D amesema kuwa anapenda kufungua milango kwa wafadhili mbalimbali kujitokeza kudhamili mpambano uhu kwani mpambano ulikuwa unasubiliwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kwa kuwa hii ni dabi ambayo ina kila kitu katika mchezo wa masumbwi mana mabondia wana uwelewa wa mchezo wa ngumi pamoja na kujulikana kimataifa zaidi


aliongeza kwa kusema kuwa mchezo wa masumbwi sio uhadui kwani michezo ujenga urafiki pamoja na kujenga udugu, mabondia hawa ambao wamekuwa wakifanya kazi za uchambuzi wa mchezo wa ngumi katika TV 


ata hivyo kwa sasa wanaingia katika vita ya kutafuta heshima katika mchezo wa ngumi ambao wanaupambania kila kukicha


mbali na mabondia hao mabondia wengine waliokwisha saini mkataba kupitia kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion ni Issa Nampepeche ambaye atavaana na Juma Choki katika mpambano wa kugombania ubingwa wa taifa


SUPER D AWACHONGANISHA TENA IBRAHIMU CLASS NA NASIBU RAMADHANI KUZIPIGA SEPTEMBA 24

 



Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akiwanyoosha mikono juu mabondia Nasibu Ramadhani kushoto na Ibrahimu Class mara baada ya kusaini mkataba wa kuzichapa Septemba 24 jijini Dar esa Salaam

 Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Nassibu Ramadhani wamesaini mkataba wa kuzipiga kwa mara nyingine tena kupitia kampuni tanzu ya kizarendo ya Super D Boxing Promotion mpambano unaotarajia kuzipiga septembar 24 jijini Dar es salaam akizungumza mara baada ya kuwasainisha mikataba mabondia hawo promota wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' 


Amesema kuwa mpambano uho unakwenda kuweka historia mpya ya mchezo wa masumbwi nchini Tanzania kwa kuwa viwango vya mabondia hawo ni vya kimataifa hata hivyo mabondia hawo wenye wa penzi wengi wa mchezo huo kwa kuwa na vigezo vikubwa vya kujua mchezo wa ngumi

Katika mpambano wa kwanza uliopigwa miaka kadhaa iliyopita Class alibuka na ushindi wa point na Nassibu akakubali mpambano uho ameshindwa hivyo alikuwa anaomba marudiano


ahidha kampuni hiyo imeingia mkataba wa mpambano mwingine tena kati ya Issa Nampepecha na Juma choki ikiwa pia mpambano huo ni wa marudiano


hata hivyo katika mpambano wa kwanza katika chezo uho Choki alishinda kwa T.K.O ya raundi ya tatu na kuibuka na ushindi mara ya Nampepeche kupigwa na kuvuja Damu nyingi sana katika mchezo huo


ambapo mpambano uhuo ulikuwas ukichezeshwa na refarii Antoni Ruta wakigombania mkanda wa ubingwa wa P.S,T mpambano uliokuwa uchezwe kwa raundi kumi


Thursday, June 17, 2021

HAMADI FURAHISHA KUZIPIGA NA KOCHA WAKE GODFREY POLINO JUNE 27 KIFA MBURAHATI

 


HAMAD FURAHISHA

BONDIA HAMAD FURAHISHA ambaye ya sasa ameingia katika ngumi za kulipwa kwa mara ya kwanza june 27  atapanda ulingoni kuzichapa na Godfrey  Polino mpambano wa raund 4 kg 55 katika uwanja wa Kifa uliopo Mburahati

Mpambano huo utafanyika katika uwanja wa kifa uliopo Mburahati umekuwa ukisubiliwa kwa hamu kubwa sana ambapo mabondia hawo ni mtu na kocha wake zamani wakati Polino alikuwa kocha uku Furahisha alikuwa bondia katika ngumi za Ridhaa wote wakiwa katika kam,bi ya JKT

Mabondia hawo watapigana kwa mara ya kwanza wakiwa na historia kubwa ya mchezo wa masumbwi katika ngumi za ridhaa na kuliletea sifa Taifa lakini kwa sasa watapigana katika ngumi za kulipwa uku kila mmoja akitaka kukuonesha

Umwamba wake katika ulingo jinsi anavyozipiga kwa ufundi zaidi majina ya Polino na Furahisha sio mageni katika ulimwengu wa masumbwi nchini ila ni mageni katika ngumi za kulipwa ambapo kupitia mabondia hawo mashabiki watapata burudani ya kutosha ya mchezo wa masumbwi nchini

akizungumza na mwandishi wa habari hizo Hamadi Furahisha anasema kuwa ngumi alianza mwaka 2009 Yombo dovya boxing Clab iliyopo chini ya kocha haji Pela ambaye mpaka leo hii wapo pamoja 

alishiriki katika mashindano mbalimbali ya masumbwi ya Ridhaa yakiwemo mashindano ya clab bingwa pamoja na ya taifa na kufanikiwa kuchaguliwa na timu ya Taifa ya ngumi  mwaka 2016 ambapo alidumu katika timu ya Taifa mpaka mwaka 2018 ambapo alipata nafasi ya kujiunga na JKT hata hivyo baada ya miaka kazaa akakosa ajira na sasa yupo mtaani na ameamua na kujiunga na ngumi za kulipwa 

anakumbuka kipindi hicho yupo JKT walipita mabondia ambao ni maarufu na mashughuli kwa sasa akiwepo Hassani Mwakinyo Salim Matango na wengine ambao nao waliachana na JKT na kujiunga na ngumi za kulipwa mara moja 

katika mchezo wa masumbwi yeye alivutiwa zaidi na Ismail Galiatano ambae nae ni bondia wa jeshi mpaka hivi sasa ndio aliekuwa akimpenda tangu anaanza ngumi mpaka sasa na kwa nje anamkubali zaidi

Bondia Manny Paquai ambaye amekuwa akimkubali zaidi kwa mapigo yake ya kasi na jinsi anavyo zitendea aki ngumi apiganapo ulingoni

Furahisha amemwambia Polino kuwa supu aitiwi nazi ikitiwa nazi inakuwa mchuzi hivyo kipigo atakachompa ni cha pekee kwani kipigo hicho akijawai kutokea tangu aanze mchezo wa masumbwi nchini

akizungumza mabondia wa Tanzania amewasii mabondia wasiwe wanaingia mitini pindi wanapopewa mapambano na yeye kwani yeye anamikono miwili na wao miwili 

pia ilitoa wito kwa wazazi kuwaruhusu vijana wao pamoja na watoto kuwapa sapoti ili wacheze mchezo wa masumbwi kwani kwa sasa ni ajira na inaweza kukutoa sehemu moja kwenda nyingine hii ni kazi kama zilivyo kazi zingine wanazofanya watu maofisini

aliongeza kwa kusema anampiga kocha wake pia mabondia wengine wajipange foleni ambao watakuwa katika uzito wa kg 55 kuwa hizi ni salam kwao

asesema anawaomba sapoti kwa mashabiki zake wote wa dabo kibini wakionozwa na Habib Othumanbig kuja kumunga mkono na kumsapoti kwa ali na mali

mpambano huo ulioratibiwa na Rajabu Mhamila 'Super D' kutoka kampuni Tanzu ya Kizalendo ya Super D Boxing Promotion umeandaliwa na Kwame Sports Promotion chini ya Promota mkuzaji wa Vipaji Kwame Hamisi Matwani mpambano utafanyika june 27

Saturday, January 25, 2020

SUPER D AMUANDAA SUNDAY KIWALE KWA USHINDI WA K,O JANUARY 31 TANGA ATAKAPOZIPIGA NA YOHANA MCHANJA


Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye kwa sasa anamnowa bondia Sunday Kiwale 'Moro Best' kwa ajili ya mpambano wake wa kugombania ubingwa wa Dunia na Yohana Mchanja mpambano utakaofanyika January 31 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga


Akizungumza wakati wa mazoezi ya kumuandaa Kiwale amesema kuwa kiwale yupo fiti sana hivyo mashabiki waje kwa wingi wangalie mchezo wa masumbwi yaliyokwenda shule kwa kuwa Kiwale yupo vizuri kwa asilimia mia moja sina shaka nae

aliongeza kwa kusema kuwa ushindi wa Kiwale ni K,O tu kwani sisi tunaenda Tanga kama wageni hivyo tunamtaka Mchanja ajiandae kweli kweli kwani sisi tunakuja na moto wenye kazi kubwa sana  hivyo atutofanya ajizi katika mpambano huo wa ubingwa wa dania wa U.B.O lazima tutarudi n mkanda Dar es salaam kwa mazoezi tuliyofanya 

aliongeza  kuwa katika mpambano huo pia ataenda na bondia wake mwingine Hassani Mgaya atakaezipiga na Saidi Mundi mpambano wa raundi sita hivyo mashabiki wa tanga waje kuona timu ya Super D inafanya nini siku hiyo ya january 31 katika uwanja wa Mkwakwani

na bondia Sunday Kiwale amesema yeye kama bondia amejiandaa na yupo tayali kwa mchezo ata sasaivi kwani yupo fiti sana ata hivyo tuataanza safari ya kutoka dar siku ya alhamisi na tukifika siku hiyo tutamima uzito kwa ajili ya mpambano siku ya pili yake naomba wakazi wa tanga na vitongoja vyake waje kuangalia ngumi mawe masumbwi
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimfundisha bondia Sunday Kiwale 'Moro Best' jinsi ya kupiga ngumi ya mkunjo wa chini 'UPCAT' kwa ajili ya maandalizi ya mpambano wa bondia huyo utakaofanyika january 31 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga ambapo atazipiga na Yohana Mchanja 

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimwelekeza jinsi ya kupiga ngumi zilizo nyooka bondia Sundasy Kiwale 'Moro Best' ambaye anajiandaa na mpambano wake na Yohana Mchanja utakaofanyika January 31 katika uwanja wa mkwakwani Tanga

Friday, September 27, 2019

BONDIA MAKUBI ATAMBA KUMPIGA ABDALLAH MA MOROGORO OKTOBA 4 KATIKA UKUMBI WA 361 MWENGE


Na Mwandishi wetu 

Bondia Ibrahim Makubi yupo kambini kwa ajili ya mazoezi yake ya kumkabili bondia abdallah kingolwira  wa ( morogoro ) katika pambano lake litakalo fanyika Oktoba 4 katika ukumbi wa 361 uliopo mwenge jeshini mpambano huo ambao umewekwa kwa ajili ya kupandisha viwango mabondia mbalimbali litakuwa ni sehumu moja ya kuwapongeza mabondia

waliofanya vizuri nje ya nchi na kurudi na mikanda mikubwa nchini miongoni mwa mabingwa hao ni Abdalah Pazi ,Tonny Rashidi ,Bruno Vifua Viwili mabondia hawo wameleta mikanda hiyo nchini ndani ya mwezi mmoja tu

Makubi ametamba kumsambalatisha bila huruma yoyote ile Abdalah wa morogoro kwani ushindi wake ndio utakao msafishia njia ya kwenda juu zaidi katika mapambano ya ngumi anajua kuwa ngumi sio mchezo raisi kama ilivyo kwa michezo mingine

nae kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' anaemnowa na kumtafutia mambambano kwa ajili ya kumpandisha Daraja bondia huyo amesema kwa sasa makubi kila pambano lake kwake ni fainal kwani hapa kazi tu No Pain No Gain tutaakikisha tunashinda kila pambano na mpaka atakuwa bingwa wa mabingwa nchini na Duniani alisema Kocha  Super d

BONDIA JUMA CHOKI SASA AWAZIA UBINGWA WA TAIFA BAADA YA KUWA KING OF THE RING


NA MWANDISHI WETU

BONDIA Juma Choki Baada ya kumgalagaza bila ya huruma Emanuel Mwakyembe na kuchukua ubingwa wa King Of The Ring 2019 katika uzito wa KG 58 amesema ato bweteka kwa kuwachua ubingwa huo 

ambapo alipewa zawadi ya pikipiki pamoja na kitita cha shilingi laki tano amesisitiza ato bweteka kwa kuwa bingwa wa mashindano hayo ata hivyo ameomba kuwa andaliwe ubingwa wa taifa ndio matarajio yake kwa sasa akichukuwa ubingwa wa taifa kisha ataenda juu kuchukuwa ubingwa wa Afrika arafu ubingwa wa Dunia

Bondia huyo mwenye ndoto ya kuwa bingwa wa Dunia kupitia mchezo wa masumbwi nchini Tanzania kwa kuchukuwa mikanda nje ya nchi na kuletea sifa Tanzania 

Akizungumza kocha wake ambaye ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa choki ni bondia mzuri na malengo yake ni kufika mbali na kweli atafika anapo pataka kwani kwenye nia pana njia

ikumbukwe kuwa mimi ndio nimewatoa mabondia mabingwa wa dunia ambao wamepita katika mikono yangu kama vile Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Idd Mkwela Vicent Mbilinyi Sunday Kiwale Ibrahimu makubi ambaye kwa sasa yupo mazoezini akijiandaa na mpambano wake na abdallah kingolwira wa morogoro pambano litakalofanyika Oktoba 4 katika ukumbi wa 361 mwenge pale jeshini

hivyo nina uwakika na mabondia wangu wote ninaowafundisha na siku zoto sinaga kazi mbovu

NGUMI KUPIGWA IJUMAA OKTOBA 4 UKUMBI 361 MWENGE

NGUMI KUPIGWA IJUMAA OKTOBA 4 UKUMBI 361 MWENGE

Mabondia wa mgumi za kulipwa nchini walioibuka na ushindi wanatarajia kushiriki katika sherehe za kupongezwa na mashabiki wao Oktoba Nne Club 361Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Mratibu mkuu wa Pambano la kuwapongeza mabondia hao Selemani Semunyu alisema mipango imekamilika ikiwemo mabondia watakaocheza ingawa maombi ni mengi ya mabondia wengi kutaka kushiriki kuonyesha furaha yao na kuwaunga mkono mabondia wenzao .
Aliwataja miongoni mwa mabingwa hao ni Abdalah Pazi ,Tonny Rashidi ,Bruno Vifua Viwili na Nassib Ramadhani kwa pamoja na bondia yeyote bingwa na wameletea taifa heshima kubwa wadau na mashabiki hakuna budi kuwapongeza.

" Serikali na Wabunge wamewapongeza lakini wadau na mashabiki sasa huu ndio wasaa wa kuwapongeza hata kama kuna zawadi ya kuwapa hii ndio sehemu moja lakini sie tunawapongeza kwa pambano" Alisema Semunyu.
Aliongeza kuwa pambano hili pia litatumika kupata mabondia watakaowania mikanda mwezi Desemba ambapo litafanyika pambano la funga mwaka.
" Watakaofanya vizuri katika pambano hili wataweza kupata nafasi katika pambano la mwezi wa 12 ambapo historia ya Ngumi nchini kwa kipindi cha hivi karibuni itawekwa " Alisema Semunyu.
Pia amewashukuru kamisheni ya ngumi za kulipwa kutoa kibali kwa wadhamini Smart Gin na kuomba wadhamini wengine kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha kurejesha hadhi ya mchezo wa ngumi nchini.
Kwa upande wake mratibu wa kiufundi wa mapambano hayo Yassin Abdalah Ustaadh aliwataja mabondia watakaosindikiza sherehe hiyo kuwa ni issa nampechehe (Dsm) vs alli hamisi (morogoro )
Ibrahim Makubi (Dsm)vs abdallah kingolwira ( morogoro )Maganga kulwa (mbagala) vs Said Sudi (M'nyamala) )Hashimu msungo vs Epson john Lewis Salumu omari vs ramadhani chicho
Aliongeza kuwa mapambano yanaweza kuongezeka kutokana na mabondia wengine kutafuta nafasi ya kutaka kushiriki Desemba lakini wengine nao wanataka kushiriki kuonesha furaha ya ushindi huo

Saturday, September 14, 2019

MABONDIA JUMA CHOKI NA EMANUEL MWAKYEMBE WAPIMA UZITO KUPIGANA KESHO SEPTEMBA 15 MASAKI


Bondia Juma Choki akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Emanuel Mwakyembe utakaofanyika katika ukumbi wa Backet Lounger Septemba 15 kushoto ni katibu wa Kamisheni ya ngumi Tanzania TPBRC Yahya Pori

Bondia Juma Choki akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na mpinzani wake Emanuel Mwakyembe kulia mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Backet Lounger Septemba 15 Jumapili 

Bondia Juma Choki na Emanuel Mwakyembe wakitunisha misuli mbelew ya kamera mabondia hawo wamepima uzito na Afya kwa ajili ya mpambano wao wa Septemba 15 katika ukumbi wa Bucket uliopo Masaki jumapili hii

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila Super D kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Jumachoka na kocha Edward Lwiyakwipya na bondia Emanuel Mwakyembe


NA Mwandishi wetu

MABONDIA Juma Choki na Emanuel Mwakyembe wamepima uzito kwa aqjili ya mpambano wao kwa ajili ya mpambano wa King Of The Ring utakaofanyika Septemba 15  katika ukumbi wa Backet Lounger uliopo Masaki Dar ES salaam

Mabondia hawo wamefanikiwa kufika Fainal baada ya kuwashinda wapinzani wao katika hatua za awali mshindi katika mpambano huo atanyakuwa pikipiki pamoja na kitita cha shilingi laki tano na atakaepigwa atachukuwa flat TV kubwa pamoja na kitita cha shilingi laki tano

Promota wa Mpambano huo Crisiani Kisinini amesema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ambapo bondia Issa Nampepeche atazipiga na Emanuel Timtimu na mabondia wengine wengi


Aliongeza kwa kusema kuwa mapambano ya ngumi yataanza saa moja kamili usiku  uki kila likipigwa pambano moja kunakuwa na burudani na mpambano wa mwisho kabisa utafanyika saa tano na saa sita itakuwa mwisho na atajulikana nani ni champion wa mashindano ya King Of The Ring ambapo Mshindi wa kwanza mpaka wa tatu watajinyakulia zawadi kubwa

Mshindi wa kwanza ataondoka na Pikipiki pamoja na laki tano pesa taslim na wa pili atajinyakulia flat TV kubwa pamoja na Laki tano wa tatu atachukuwa kiasi cha pesa Taslim shiling Laki Tano

Hivyo amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi waje waangalie nani bingwa katika uzito wa KG 58 kwa hapa nchini Tanzania

Tuesday, September 10, 2019

JUMA CHOKI AJIFUA KUMKABIRI MWAKYEMBE SEPTEMBA 15


Bondia Juma Choki kushoto akioneshana umwamba na bondia wa Kimataifa ambaye alishawai kuishi nchini Marekani miezi takribani 8 kwa ajili ya mchezo wa masumbwi nchini humu Ibrahimu Class 'KING CLASS MAWE' Choki anajiandaa na mpambano wake wa fainal dhidi ya Emanuel Mwakyembe septemba 15 katika ukumbi wa bucket club uliopo Masaki Dar es salaam

Bondia Juma Choki kushoto akioneshana umwamba na Ibrahimu Makubi wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Super D Coach iliyopo kariakoo

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana umwamba na Juma Choki wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kamba ya Super D coach Shule ya Uhuru Dar es salaam Jana


Bondia Alex Kachelewa kushoto akitupiana makonde na Juma Choki wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Super D coach shule ya Uhuru 


Bondia wa Kimataifa nchini Tanzania ambaye alishawai kuka nchini Marekani kwa Takribani ya miezi nane kwa ajili ya mcheszo wa masumbwi Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto' akioneshana umwamba na Juma Choki anayejiandaa na mpambano wake dhidi ya Emanuel Mwakyembe utakaofanyika septemba 15 katika ukumbi wa Backet club ulipo masaki


Bondia wa Kimataifa nchini Tanzania ambaye alishawai kuka nchini Marekani kwa Takribani ya miezi nane kwa ajili ya mcheszo wa masumbwi Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto' akioneshana umwamba na Juma Choki anayejiandaa na mpambano wake dhidi ya Emanuel Mwakyembe utakaofanyika septemba 15 katika ukumbi wa Backet club ulipo masaki


Na Mwandishi Wetu

Bondia Juma Choki anaye jiandaa na mbambano wake dhidi ya Emanuela Mwakyembe septemba 15 katika ukumbi wa bucket Clab uliopo Masaki jijini Dar es es salaam amejinasibu kumtwanga bondia huyo na kuchukuwa ubingwa wa king of The Ring 

akijinasibu bondia huyo alivyotembelewa kambini kwake kwa Super D Coach iliyopo shule ya Uhuru Jijini Dar es salaam 

Amesema kuwa mwakembe ana uwezo wa kukanyaga moto wake ata siku moja huko alikutana na viande sasa kaja kwenye kazi kazi hapo  ndipo pa kuoneshana uwezo kama anavyosemaga kocha Super D Kazi Kazi No Pain No Gain yani siku hiyo patachimbika hivyo mwakyembe ajipange sana kwana mazoezi ninayofanya na mbinu ninazofundishwa sio za kitoto hatari tupu

Nae kocha wa bondia huyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema hii ni vita kubwa sana kwa kuwa kocha wa mwakyembe  Edward Lwiyakwipya wamesoma nae pamoja katika ngazi kubwa ya kozi ya kimataifa hata hivyo mimi nina mbinu nyingi zaidi yake ata hivyo nita akikisha napata ushindi usiokuwa wa kuwachosha majaji hivyo matumaini yangu ni kumpiga k,o mbaya zaidi

ikumbukwe kuwa mabondia wote wenye viwango vya juu nchini wanatoka kwangu ukiangalia mabondia wote wakubwa wanatoka kwangu na wana viwango vya kimataifa hivyo najivunia kwa hilo ukiangalia mabondia wanaotoka kwangu akuna ata mchovyu mmoja alijinasibu Super D

Aliongeza kwa kusema mikono yake wamepita mabondia wengi sana akiwemo Sanday Kiwale, Idd Mkwera Vicent Mbilinyi Ibrahimu Class' King Class Mawe' Shomali Milundi  Shabani Kaoneka na mabondia mbalimbali nchini wote wamepita katika mikono yangu kwa njia moja au nyingine hapa ndio No Pain No Gain kazi kazi hivyo wapenzi wa ngumi muje kwa wingi kuangalia kazi hii ambayo aita muacha mtu salam

Friday, July 26, 2019

MABONDIA TWAHA KIDUKU NA TSHIBANGU KAYEMBE KUZIPIGA KESHO JULAI 27 ESCAP ONE


Promota Kaike Siraju katikati akiwainua mikono juu mabondia Twaha Kiduku kushoto na Tshibangu Kayembe kutoka Kongo baada ya kupima uzito na afya kwa ajili ya mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia utakaofanyika katika ukuimbi wa Escap One  Mikocheni B 

Bobondia Twaha Kiduku kushoto akitambiana na bondia kutoka Kongo Tshibangu Kayembe baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa Dunia utakaofanyika Julai 27 katika fukwe za Escap One Mikocheni 

Bondia Ibrahimu Makubi akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Adamu Yusufu utakaofanyika Escap One julai 27

Mabondia Adam Yusufu kushoto akitambiana na Ibrahimu Makubi baada ya kupima uzito na Afya kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika katika fukwe za Escap One Mikocheni 

BONDIA TSHIBANGU KAYEMBE AKIPIPWA AFYA NA DR DOLNARD MADONO


BONDIA TSHIBANGU KAYEMBE AKIPIPWA UZITO

Friday, July 19, 2019

SUPER D ATAMBA KUWA CHOKI HATACHUKUWA UBINGWA WA MASHINDANO YA KING OF THE RING 2019



Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akioneshana umwamba na Juma Choki wakati wa Mazozi  yanayoendelea katika kambi ya Super D iliyopo shule ya Uhuru Kariakoo Choki anajiandaa na Mashindano ya King Of The Ring yatakayofanyika julai 28 jijini Dar es salaam

Bondia Ibrahimu Makubi kushoto akioneshana umwamba na Juma Choki wakati wa Mazozi  yanayoendelea katika kambi ya Super D iliyopo shule ya Uhuru Kariakoo Choki anajiandaa na Mashindano ya King Of The Ring yatakayofanyika julai 28 jijini Dar es salaam
                                                Na Mwandishi Wetu

BAADA ya mchujo wa kwanza kupita katika mashindano ya King Of The Ring sasa ni hatua ya nusu fainali itakayowakutanisha mabondia wanne kutoka wilaya za jiji la Dar es salaam ambapo katika Wilaya ya Ilala anatoka Juma Choki ambaye anapeperusha bendera ya wilaya hiyo bondia huyo machachali anatoka katika kambi ya kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye amesema amemuandaa choki kwa ajili ya ushindi

kwani yeye ni mshindani wa kweli ambapo katika mashindano hayo mara ya kwanza katika hatua ya mtoano alimchakaza bondia mgumu zaidi Peter Makundi katika mashindano hayo na sasa yupo katika nusu fainali atuwezi kuwangusha wapenzi wa ngumi kwani ubingwa tunautaka na ninawambiwa king of the Ring 2019 inakwenda Ilala bila kipingamizi wala kikwazo chochote kile

kwa upande wa bondia Choki amesema kuwa yeye yupo fiti kwani anaona mpambano upo mbali anataka ata leo zipigwe kwa kuwa yupo fiti mpaka anajiogopa hivyo basa wapenzi wa mchezo wa ngumi waje kuona nafanya nini siki hiyo katika mchezo wa masumbwi nchini nitandika historia mpya kabisa katika ngumi ambayo aijawai kutokea ila kila mtu atajua kazi ya mikono yangui ni nina na maamuzi yapo katika mikono yangu kwa kutoa vipigo vya paka mwizi

Katika mashindano hayo mabondia wengine waliopita ni Emanuel Mwakembe Issa Nampepeche na Emanuel Timtim mabondia wote hawo ni wa uzito wa kg58

Katika mashindano hayo washindi watapata zawadi kem kem kama kifuta jasho 

JUMA CHOKI AJIANDAA NA MASHINDANO YA KING OF THE RING JULAI 28


Bondia Ibrahimu Makubi kushoto akioneshana umwamba na Juma Choki wakati wa Mazoezi  yanayoendelea katika kambi ya Super D iliyopo shule ya Uhuru Kariakoo Choki anajiandaa na Mashindano ya King Of The Ring yatakayofanyika julai 28 jijini Dar es salaam



Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akioneshana umwamba na Juma Choki wakati wa Mazoezi  yanayoendelea katika kambi ya Super D iliyopo shule ya Uhuru Kariakoo Choki anajiandaa na Mashindano ya King Of The Ring yatakayofanyika julai 28 jijini Dar es salaam

Bondia Ibrahimu Makubi kushoto akioneshana umwamba na Juma Choki wakati wa Mazoezi  yanayoendelea katika kambi ya Super D iliyopo shule ya Uhuru Kariakoo Choki anajiandaa na Mashindano ya King Of The Ring yatakayofanyika julai 28 jijini Dar es salaam

Bondia Ibrahimu Makubi kushoto akioneshana umwamba na Juma Choki wakati wa Mazoezi  yanayoendelea katika kambi ya Super D iliyopo shule ya Uhuru Kariakoo Choki anajiandaa na Mashindano ya King Of The Ring yatakayofanyika julai 28 jijini Dar es salaam

Saturday, June 29, 2019

NGUMI KUPIGWA JULAI 7 CHANIKA MAGENGE MBEGU AHAIDI MAMBO MAKUBWA


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza bondia Ramadhani Mbegu 'Migwede' kupiga ngumi ya Mkunjo wa chini Upcut  wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Super D Coach shule ya Uhuru kariakoo Dar es salaam jana Mbegu anajiandaa na mpambano wake wa julai 7 utakaofanyika katika ukumbi wa manka pub Chanika Magenge


Na Mwandishi Wetu
Baada ya tamba mbalimbali za hapa na pale sasa mabondia Hussein Alli 'Gobosi' na Ramadhani Mbegu' Migwede' watazipiga julai 7 katika ukumbi wa Manka Pub Chanika Magenge mpambano wa raundi 8 


Migwede amea wa ahidi mashabiki zake kuja kwa wingi kwani anacheza katika uwanja wa nyumbani na ato waangusha mashabiki zake ujue nimekuwa nikikimbiwa na mabondia mbalimbali hivyo bondia yoyote anaekuja katika anga zangu nakanyaga tu anakuwa kama ngazi

Mpambano uho ulio andaliwa na Rajabu Mhamila 'Super D' kupitia kampuni ya Super D boxing Promotion amesema kuwa pambano hili ndio litakalo amua nani zaidi bada ya mabondia hawo kuwa na viwango sawa kwa sawa  Ambapo katika viwango vya ubora nchini Tanzania Mbegu yeye ni nambari 10 wakati Hussein Ally yeye ni namba 14 katika ubora

Super D aliongeza kwa kusema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ambapo Hamidu Kwata atazipiga na Luckman Ramadhani na Salum Mandai 'Pacho' atazidunda na Waziri Rosta wakati Juma Zingiziwa ataoneshana umwamba na Alex Kachelewa juma Malenda atavaana na Ibrahimu Makubi na Hussein Shemdoe atazipiga na Juma Kadoda wakati Said Mbelwa atazidunda na Shabni Kaoneka na mapambano mengine mbalimbali ya vijana chipkizi

Super D aliendelea kwa kuseka kuwa siku hiyo ngumi zitaanza mapema sana kutokana na kuwa na mapambano mengi na makali hivyo kuwataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuwai kufika ukumbini ili ngumi zianze kwa wakati

usalamab wa mali zao ni wakutosha kabisa kwani mashabiki wanatakiwa waje na familia zao wapate burudani ya mchezo wa masumbwi

SUPER D AMNOWA RAMADHANI MBEGU 'MIGWEDE' KUPAMBANA JULAI 7 CHANIKA MAGENGE



Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza bondia Ramadhani Mbegu 'Migwede' kupiga ngumi ya Mkunjo wa chini Upcut Mbegu anajiandaa na mpambano wake wa julai 7 utakaofanyika katika ukumbi wa manka pub Chanika Magenge


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza bondia Ramadhani Mbegu 'Migwede' kupiga ngumi ya Mkunjo wa chini Upcut Mbegu anajiandaa na mpambano wake wa julai 7 utakaofanyika katika ukumbi wa manka pub Chanika Magenge

Thursday, June 20, 2019

SUPER D KUWAPAMBANISHA ABDUL ZUGO NA RAMADHANI MBEGU SIKU YA SABASABA DAY CHANIKA


Na Mwandishi Wetu
Baada ya tamba mbalimbali za hapa na pale sasa mabondia Abdul Zugo na Ramadhani Mbegu' Migwede' watazipiga julai 7 katika ukumbi wa Manka Pub Chanika Magenge mpambano wa raundi 8

Mpambano uho ulio andaliwa na Rajabu Mhamila 'Super D' kupitia kampuni ya Super D boxing Promotion amesema kuwa pambano hili ndio litakalo amua nani zaidi bada ya mabondia hawo kuwa na viwango sawa kwa sawa ambapo mabondia hwao wmecheza mapambano yao 12 kila mmoja na kushinda 10 kila mmoja na ku droo 2 kila mmoja katika mapambano yao

mpambano huo utakuwa wa kukata na shoka kwa kuwa kila mmoja anataka kuendeleza wimbi la ushindi

Super D aliongeza kwa kusema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ambapo Hamidu Kwata atazipiga na Luckman Ramadhani na Salum Mandai 'Pacho' atazidunda na Waziri Rosta wakati Juma Zingiziwa ataoneshana umwamba na Alex Kachelewa juma Malenda atavaana na Ibrahimu Makubi na Hussein Shemdoe atazipiga na Juma Kadoda wakati Said Mbelwa atazidunda na Shabni Kaoneka na mapambano mengine mbalimbali ya vijana chipkizi

Super D aliendelea kwa kuseka kuwa siku hiyo ngumi zitaanza mapema sana kutokana na kuwa na mapambano mengi na makali hivyo kuwataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuwai kufika ukumbini ili ngumi zianze kwa wakati

usalamaa wa mali zao ni wakutosha kabisa kwani mashabiki wanatakiwa waje na familia zao wapate burudani ya mchezo wa masumbwi

NGUMI KUPIGWA CHANIKA SIKU YA SABASABA 2019









Wednesday, April 24, 2019

BONDIA RAMADHANMI MBEGU HAPANIA KUMPIGA HASSANI MGAYA KWA K,O APRIL 27 CHANIKA


Na Mwandishi Wetu

BONDIA ramadhani Mbegu 'Migwede' baada ya kumsambalatisha bila huruma mpinzani wake waliyokutana nae katika mpambano wa Pasaka Bilali Rashidi kwa K.O ya raundi ya pili sasa Mbegu atakabiliana na Hassani Mgaya katika mpambano wake wa Aperl 27 utakaofanyika katika ukumbu wa Manka Pub uliopo Chanika Magenge

akizungumza kuhusu mpambano uho Promota wa mchezo wa masumbwi nchini ambapo kiataalamu ni Kocha wa mchezo uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa maandalizi ya mpambano huo yamekamilika na sasa wana hesabu masaa kufikia mpambano uho mabonduia hawo watakuwa wakisindikiza pambano kubwa kati ya Saidi Mbelwa na Selemani Galili 'TOLL'   aliongeza kwa kusema mbali na mapambano hayo kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na mundu ambapo Juma Bilo atakabiliana na Magambo Christopher na Shukuru Samata ataoneshana kazi na Juma Ramasdhani na Mbwana Chinenda atamkabili Mohamed Muhunzi wakati Ismahil Kharidi atakumbana uso kwa uso na Salehe Ubuguyu Anamu Ngange 'Mnyama' atacheza na Saadi Kuchi wakati Abdul Zugo atazipiga na Lumeme Hussein na Idd Mbaruku atazikunja na Mohamed Mshamu

Super D amesema kuwa mapambano yote haya ni kwa ajili ya mabondia kupata ushindani kila wakati na wanatakiwa wawe bize na mazoezi kwa ajili ya mechi mbali mbali zitakazo wakabili ameseka kuwa uzito watapima siku ya ijumaa katika ukumbi uho huo na watacheza siku ya jumamosi ya April 27

Mpambano huu unategemea kufanyika kabla ya kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo kampuni ya kuinuwa vipaji vya mchezo wa masumbwi nchini ya Super D Boxing Promotion itakuwa likizo kwa mda kwa kuandaa mapambano ya masumbwi hata hivyo Super D ametoa wito kwa mabondia kuendelea na mazoezi kwa kipindi choto cha Ramadhani kwani kuna mapambano mengi ya ngumi yatandaliwa na Kampuni yake kwa ajili ya kukuza kuendeleza na kuinua vipaji vipya vya masum,bwi nchini Super D Mbali ya kuandaa mapambano ya ngumi pia anajihusisha moja kwa moja kuuza vifaa vya mchezo huo pamoja na kutoa mafunzo ya ngumi katika GYM yake iliyopo Kariakoo Dar es salaam

Saturday, April 20, 2019

NGUMI KUPIGWA JUMAPILI YA PASAKA CCM MWINYI MKUU MAGOMENI


Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akitunishiana misuli na Rojas Masamu baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika CCM Mwinyi Mkuu magomeni Mapipa katikati ni Promota wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' kutoka SUPER D BOXING PROMOTION
Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kutoka Super D Boxing Promotion akiwainu mikono juu bondia Vicent Mbilinyi kushoto na Rojas Masamu baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa Pasaka utakaofanyika CCM Mwinyimkuu Magomeni Mapipa

Bondia Vicent Mbilinyi akipimwa Afya na DOKTA Dolnad Madono

Bondia Ramadhani Mbegu 'Migwede' akipimwa Afya na DOKTA Dolnad Madono

Bondia Saluim Tandu akipimwa Afya na DOKTA Dolnad Madono

Promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwainua mikono juu mabondia Ramadhani Mbegu 'Migwede' kushoto na Bilali Rashidi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumapili ya Pasaka katika ukumbi wa CCM Mwinyi Mkuu nagomeni Mapipa

Bondia Ramadhani Mbegu 'Migwede' kushoto akitunishiana misuli na Bilali Rashidi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Mwinyi Mkuu Magomeni Mapipa siku ya sikukuu ya Pasaka

Promota Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwainua mikono juu mabondia Salum Tandu kushoto na Gelard Mkude ambao watacheza siku ya jumapili ya pasaka April 4 katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu

Bondia Sunday Kiwale 'Moro Best' kushoto akitunishiana misuli na Luckman Ramadhani baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao uakaofanyika jumapili ya Pasaka April 21 katika ukumbi wa CCM mwinyimkuu Magomeni Mapipa katikati ni Promota wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' KUTOKA SUPER D BOXING PROMOTION

Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu MHAMILA 'Super D' kushoto akiwainua mikono juu mabondia Sunday Kiwale 'Moro Best' na Luckman Ramadhani baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa Pasaka utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Mwinyi Mkuu Magomeni Mapipa

Bondia Bakari Mbede kushoto akitunishiana misuli na Shomari Milundi baada ya kupima uzitio na Afya kwa ajili ya m,pambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka April 21 katika ukumbi wa CCM mwinyi Mkuu katikati ni Promota wa Mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' KUTOKA sUPER d Boxing Promotion


Promota Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwangalia mabondia Salum Tandu kushoto na Gelard Mkude  walivyokuwa wakipigiana mikwala mabondia hawo watacheza siku ya jumapili ya pasaka April 4 katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu

Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwainua mikono juu mabondia Sandal Nyambala kushoto na Ahmad Kombo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa Pasaka utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu Magomeni Mapipa

Mabondia Sandal Nyambala kushoto akitunishiana misuli na Ahmad Kombo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya Pasaka katikati ni Promota Rajabu Mhamila 'Super D' 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...