Marquee
tangazo
Monday, October 11, 2021
BONDIA RAMADHANI MIGWEDE ASAINI KUZIPIGA NA HABIBU PENGO OKTOBA 12 AWAITA MASHABIKI WA CHANIKA KUJITOKEZA SIKU HIYO
NA MWANDISHI WETU BONDIA RAMADHANI MIGWEDE amesaini mkataba wa kuzipiga na
Habibu Pengo Novemba 12 mpambnano wa raundi kumi utakaofanyika jijini Dar es
salaam akizungumza na wahandishi wa habari kocha wa kimataifa wa mchezo wa
masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa Migede kasaini mkataba uho
mbele ya katibu wa kamisheni ya ngumi za kulipwa Yahya Poli mpambano
utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao bondia huyo mwenye maskani yake chanika
nje kidogo ya jiji la Dar es salaam atapambana na Pengo mpambano ambao utakuwa
autabiliki kwani mabondia wote hawo wana uzoefu mkubwa katika mchezo wa masumbwi
mbali na uzoefu waliokuwa nao pia wamekuwa wakiwapa vipondo wapinzani wao kadri
wakutanapo nao ulingoni ambapo bondia migwede hivi karibuni alimchakaza vibaya
tena bila huruma bondia keis ally kwa k,o ya raundi za awali nae Pengo amekuwa
tishio katika kipindi cha hivi karibuni kwani alikuwa akicheza mapambano makubwa
na yenye msisimko zaidi na kufurahisha mashabiki awapo ulingoni Pengo mwenye
mashabiki luluki katika kitongoji cha mabibo na viunga vyake vya jirani
amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuja kuangalia mchezo uho bila ya kukosa
nae Migwede amesema alikuwa anamtafuta sana Pengo kwa udi na uvumba hivyo kwa
sasa kaingia katika choo cha watoto hivyo kaingia katika 18 zangu hivyo nawaomba
mashabiki wake wote wajitokeze kwani siku hiyo atafanya atakachotumwa na
mashabiki zake wa chanika pamoja na vitongoji vya jirani hivyo wasikose kuja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment