Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, April 30, 2014

STEPS SOLAR YAZINDULIWA KIGAMBONI

Mkurugenzi wa Steps Solar Dilesh Solanki kushoto pamoja na wasanii wa filamu ambao ni mabalozi wa Steps Solar ,Salma Jabu 'Nisha' na Amri Athumani 'Mzee Majuto' wakiomkabidhi zawadi ya solar kwa ajili ya kutumia nyumbani Mbunge wa jimbo la Kigamboni, DR, Faustine Ndugulile wakati wa tafrija ya uzindudhi wa bidhaa hizo zilizofanyika mji mwema kigamboni Dar es salaam Picha na www.burudan.blogspot.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Steps Solar Jairaj wa pili kulia akimuonesha Mbunge wa jimbo la Kigamboni, DR, Faustine Ndugulile wakati wa tafrija ya uzindudhi wa bidhaa hizo zilizofanyika mji mwema kigamboni Dar es salaam katikati ni
Mkurugenzi wa Steps Solar Dilesh Solanki 
Picha na www.burudan.blogspot.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Steps Solar Jairaj  kulia akimuonesha Mbunge wa jimbo la Kigamboni, DR, Faustine Ndugulile pasi jinsi ilivyopata moto wakati wa tafrija ya uzindudhi wa bidhaa hizo zilizofanyika mji mwema kigamboni Dar es salaam katikati ni
Mkurugenzi wa Steps Solar Dilesh Solanki  na Ofisa wa kampuni hiyo Moses Mwanyilu
Picha na www.burudan.blogspot.com
Ofisa wa kampuni ya Steps Solar Moses Mwanyilu akimwelekeza
Mbunge wa jimbo la Kigamboni, DR, Faustine Ndugulile wa pili kushoto jinsi wa umeme unavyopatikana kupitia mashine ndogo ya kuifadhia umeme wa jua kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Steps Solar Jairaj
katikati ni
Mkurugenzi wa Steps Solar Dilesh Solanki na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya temeke Sikunjema Shabani

Picha na www.burudan.blogspot.com


Tuesday, April 29, 2014

DVD MPYA ZA MASUMBWI KUTOKA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION DVD HII YA MASUMBWI IKIMUHUSISHA IBRAHUMU CLASS .KING CLASS MAWE.  MAPAMBANO MAKALI YA NGUMI ZOTE KALI LIPO KWENYE DVD MOJA SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania


DVD MPYA ZA MASUMBWI ZIKIMSHILIKISHA BONDIA IBRAHIMU CLASS KING CLASS MAWE
MPAMBANO WA MASUMBWI AMBAO UMEACHA HISTORIA KATIKA MCHEZO WA NGUMI DUNIANI

EAST AFRICA MELODY KUWASHA MOTO MEI MOSI TRAVENTINE MAGOMENI MEI MOSINa Mwandishi wetu

BENDI ya taaarabu ya East African Melody  itatoa burudani katika ukumbi wa traventine Dar es salaam kwa ajili ya kusherekea siku kuu ya wafanyakazi Duniani Mei mosi

akizungumza onesho hilo muhandaaji wake Abbass Chezntemba 'Abbas  Chez' Cash Money' amethibitisha kufanyika onesho hilo ambali litakuwa la kihistoria jijini 

ambapo wasanii mbalimbali wamealikwa kushiriki kutoa burudani siku hiyoambayo imepewa jina la Usiku wa habiti za sauti za dhahabu ambapo watasindikizwa na ngwiji wa mziki wa dansi nchini

king kiki mzee sugu na kitambaa cheupe na Pr, Muhamed Issa  Matona,Rukia Ramadhani,Sabaha Muchacho, Hadija Yusuph ,Shakila Said, Ustadh Muhamed

na wasanii wengine wengi
kingilio kitakuwa ni  shilingi 7000 na 10,000 kwa watu watakaokaa V.I.P pia kutakuwa na zawadi kumi tofauti kwa ajili ya sikukuu hiyo itakayotolewa na Cash Money siku hiyo katika ukumbi wa traventine kwa watakaofika kuangalia onesho hilo

MSONDO WATOA BURUDANI KWA WAFANYAKAZIMwimbaji wa bend ya msondo ngoma Shaban Dede akiimba wakati wa maonesho ya mahadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam

Waimbaji wa bendi ya Msondo ngoma wakitoa burudani wakati wa siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam
Wapuliza hara wa bendi ya msondo ngoma wakiwajibika wakati wa mahadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini kutoka kushoto ni Shabani Lendi, Hamisi Mnyupe na Roman Mn'gande

IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE SASA ATAKA KUWANIA UBINGWAIbrahimu Class King Class Mawe birth place Iringa, Tanzania won 10,
birthdate 1990-10-10 (age 23)
division light welterweight
Ibrahimu Class King Class Mawe birth place Iringa, Tanzania won 10,
birthdate 1990-10-10 (age 23)
division light welterweight
Ibrahimu Class King Class Mawe birth place Iringa, Tanzania won 10,
birthdate 1990-10-10 (age 23)
division light welterweight

Monday, April 28, 2014

EAST AFRICA MELODY KUWASHA MOTO MEI MOSI TRAVENTINE MAGOMENI MEI MOSI

Na Mwandishi wetu

BENDI ya taaarabu ya East African Melody  itatoa burudani katika ukumbi wa traventine Dar es salaam kwa ajili ya kusherekea siku kuu ya wafanyakazi Duniani Mei mosi

akizungumza onesho hilo muhandaaji wake Abbass Chezntemba 'Abbas  Chez' Cash Money' amethibitisha kufanyika onesho hilo ambali litakuwa la kihistoria jijini 

ambapo wasanii mbalimbali wamealikwa kushiriki kutoa burudani siku hiyoambayo imepewa jina la Usiku wa habiti za sauti za dhahabu ambapo watasindikizwa na ngwiji wa mziki wa dansi nchini

king kiki mzee sugu na kitambaa cheupe na Pr, Muhamed Issa  Matona,Rukia Ramadhani,Sabaha Muchacho, Hadija Yusuph ,Shakila Said, Ustadh Muhamed

na wasanii wengine wengi
kingilio kitakuwa ni  shilingi 7000 na 10,000 kwa watu watakaokaa V.I.P pia kutakuwa na zawadi kumi tofauti kwa ajili ya sikukuu hiyo itakayotolewa na Cash Money siku hiyo katika ukumbi wa traventine kwa watakaofika kuangalia onesho hilo

MSONDO WATOA BURUDANI KWA WAFANYAKAZI

Mwimbaji wa bend ya msondo ngoma Shaban Dede akiimba wakati wa maonesho ya mahadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam

Waimbaji wa bendi ya Msondo ngoma wakitoa burudani wakati wa siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam
Wapuliza hara wa bendi ya msondo ngoma wakiwajibika wakati wa mahadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini kutoka kushoto ni Shabani Lendi, Hamisi Mnyupe na Roman Mn'gande

Subira ya Shaa apewa Adam Juma


MTAYARISHAJI mahiri wa video za muziki wa kizazi kipya nchini, Adam Juma wa Visual Lab, amepewa shavu la kurekodi video ya wimbo mpya wa mwanadada Sarah Kais 'Shaa' uitwao 'Subira'.
Wimbo huo ambao awali ulikuwa ukifahamika kama 'Sifa Ujinga' kabla ya kubadilishwa jina, unatarajiwa kurekodiwa video yake wiki ijayo.
Mmoja wa mabosi wa Shaa ambaye anafanya kazi na Mkubwa na Wanae kwa mkataba maalum, Said Fella aliiambia MICHARAZO kuwa, wameamua kumpa 'shavu' Adam Juma kuiandaa video ya wimbo huo ambao umekamilika tangu mwishoni mwa mwaka jana.
"Baada ya kutafakari kwa kina tumeamua kumpa nafsi nyingine mkali Adam Juma kufyatua video ya wimbo mpya wa Shaa uitwao 'Subira' na kazi ya kurekodi inatarajiwa kuanza wiki ijayo hapa jijini Dar es Salaam," alisema.
Fella alisema wanatarajia video hiyo iwe kali kufunika hata ile ya wimbo wa 'Sugua Gaga' ambao umekuwa ukifanya vyema kwenye vituo vya runinga nchini ikiwa ni kati ya kazi za kwanza za Shaa chini ya Mkubwa na Wanae.

MAMA SHUJAA WA CHAKULA WAINGIA RASMI KIJIJI CHA MAISHA PLUS, PROFESA ANNA TIBAIJUKA MGENI RASMI KATIKA SHEREHE HIZO


Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa pili  kutoka kulia pamoja na Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwasalimia  akina mama Shujaa wa Chakula ambao wameingia Rasmi Kijiji cha Maisha  Plus Jana usiku.
Akina Mama Shujaa wa Chakula Wakiwa wanamuimbia wimbo maalum Profesa Anna  Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi mara baada ya  kuwasili Kijijini hapo.
Hawa ndio Mama Shujaa wa Chakula ambao jana usiku wameingia Rasmi katika Kijiji Cha Maisha Plus
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudia Kukaribishwa Rasmi kwa Mama shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.
Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sister Anna Mwasu wa tatu kutoka kulia akiwa katika sherehe za kuwakaribisha mama Shujaa wa  Chakula ambao  wameingia rasmi katika Kijiji cha Maisha Plus Jana.
Mwakilishi kutoka Forum CC Faidhari akizungumza jambo wakati wa kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.
Teresa Yates Mwakilishi kutoka OXFAM akitoa salama za Shukurani kwa wadau wote

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA USALAMA NA AFYA DUNIANI,KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA DAR


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo April 28-2014, kwa ajili ya kuhutubia wananchi kwenye maadhimisho ya siku ya usalama na Afya Duniani.
 Afisa mkuu mwandamizi wa mazingira katika mamlaka ya Bandari Thobias Sonda akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, juu ya utumiaji wa vifaa vya kupimia hewa, wakati alipotembelea Banda la maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya  Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.  
 Mtaalam wa uchunguzi wa vyakula katika maabara ya mkemia mkuu wa Serikali Edith Wilbald akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipotembelea Banda la maabara ya uchunguzi wa vyakula kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya  Duniani.
 Mtaalam wa uchimbaji wa madini katika mgodi wa Noth Mara Gold Mine Paul Kagodi akimuonesha Makamu wa Rais vifaa vinavyotumika katika kazi ya uchimbaji wa madini wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya  Duniani yaliyoadhimishwa leo.
 Watumishi wa taasisi mbalimbali wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014 kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Watumishi wa taasisi mbalimbali wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014 kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Watumishi wa taasisi mbalimbali wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014 kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea maandamano kwenye maaadhimisho ya siku ya Usalama na Afya yaliyoadhimishwa leo April 28-2014  katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Wanamuziki wa bendi ya 'OUT Jaz Band' wakitumbuiza kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani  yaliyoadhimishwa leo.
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi Nicolas Mgaya akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani  yaliyoadhimishwa leo April 28-2014  katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabizi zawadi K. Lwakatare mkuu wa usalama na mazingira Vodacom kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya yaliyoadhimishwa leo April 28-2014  katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabizi zawadi maalum Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Makongoro Mahanga wakati wa  maaadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014  katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akihutubia kwenye hafla hiyo.
 Picha ya pamoja...
 Picha ya pamoja....
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...