Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, April 25, 2014

Mhe Temba, Chegge Waueni sasa!


http://1.bp.blogspot.com/_KpTauCrw3bQ/TQ9SJ2k4PEI/AAAAAAAAEdo/d4omGT6d6H0/s1600/Temba%2Band%2BChege.jpgNYOTA wa muziki wa kizazi kipya wanaotoka kundi la TMK Wanaume Family, Chegge na Mhe Temba wanatarajia kuachia hewani wimbo wao mpya uitwao 'Waue' waliowashirikisha 'membaz' wa Mkubwa wa Wanawe.
Wasanii walioshirikishwa na wakali hao ni Maromboso na YP ambao nao wanatokea 'ukoo' wa TMK Wanaume Family na Mkubwa na Wanae.
Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe na Meneja wa wasanii hao, Said Fella 'Mkubwa' aliiambia MICHARAZO kuwa, wimbo huo utaachiwa 'audio' na video wiki mbili zijazo baada ya kukamilisha baadhi ya mambo.
Mkubwa, alisema wimbo huo umerekodiwa katika studio zao za Mkubwa na Wanae chini na mtayarishaji, Shirko na video imefanywa na Adam Juma kupitia kampuni yake ya Visual Lab.
"Wasanii Temba na Chegge wamekamilisha kurekodi 'audio' na video ya wimbo wao uitwao 'Waue' wallioimba na Maromboso na YP, na tunapanga kuachia kazi hizo kwa pamoja wiki ijayo," alisema.
Chegge na Mhe Temba wamekuwa wakitoa kazi za pamoja mbali na zile za binafsi za kila mmoja nje ya nyimbo za kundi lao la TMK Wanaume Family.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...