Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 17, 2014

Makamu wa Rais,Dkt. Bilal atembelea banda ya Bunge kwenye Maonyesho ya Muungano jijini DarMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ghalib Mohamed Bilal akipata maelezo ya Historia, Muundo, Kazi na Utendaji wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Afisa Habari wa Bunge Bw. Prosper Minja wakati kiongozi huyo alipotembelea banda la Bunge lililopo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo lijini Dar es Salaam. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miongoni mwa washiriki wa maonesho ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano. Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi zinashiriki katika kuonesha mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha Miaka 50 Muungano.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad (kulia) akisaini Kitabu cha Wageni Mashuhuri alipotembelea banda la Ofisi ya Bunge lililoko katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam wakati wa maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano. Picha na Prosper Minja - Minja

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...