Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, April 28, 2014

Subira ya Shaa apewa Adam Juma


MTAYARISHAJI mahiri wa video za muziki wa kizazi kipya nchini, Adam Juma wa Visual Lab, amepewa shavu la kurekodi video ya wimbo mpya wa mwanadada Sarah Kais 'Shaa' uitwao 'Subira'.
Wimbo huo ambao awali ulikuwa ukifahamika kama 'Sifa Ujinga' kabla ya kubadilishwa jina, unatarajiwa kurekodiwa video yake wiki ijayo.
Mmoja wa mabosi wa Shaa ambaye anafanya kazi na Mkubwa na Wanae kwa mkataba maalum, Said Fella aliiambia MICHARAZO kuwa, wameamua kumpa 'shavu' Adam Juma kuiandaa video ya wimbo huo ambao umekamilika tangu mwishoni mwa mwaka jana.
"Baada ya kutafakari kwa kina tumeamua kumpa nafsi nyingine mkali Adam Juma kufyatua video ya wimbo mpya wa Shaa uitwao 'Subira' na kazi ya kurekodi inatarajiwa kuanza wiki ijayo hapa jijini Dar es Salaam," alisema.
Fella alisema wanatarajia video hiyo iwe kali kufunika hata ile ya wimbo wa 'Sugua Gaga' ambao umekuwa ukifanya vyema kwenye vituo vya runinga nchini ikiwa ni kati ya kazi za kwanza za Shaa chini ya Mkubwa na Wanae.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...