Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 10, 2014

MASHINDANO YA TANZANIA MOVIE TALENTS KUHAMIA KANDA YA KATI MKOANI DODOMA, ZOEZI LA KUTAFUTA WASHINDI KUANZA JUMAMOSI YA WIKI HII


Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mwanza

Hatimaye Kikosi Kazi cha Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ndio waratibu na waandaaji wa Mashindano ya Kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania yajulikanayo kama Tanzania Movie Talents (TMT) kinaondoka leo asubuhi Mkoani Mwanza Kuelekea Mkoani Dodoma kwaajili ya kuendelea na shindano la kusaka vipaji vya kuigiza katika Kanda ya Kati ambapo mashindano yatafanyika Mkoani Dodoma katika Ukumbi wa African Dream kuanzia Jumamosi ya tarehe 12 April 2014 kuanzia Saa moja asubuhi hadi tarehe 15 April 2014, kabla ya mashindano hayo kufanyika Mkoani Dodoma mnamo Siku ya Ijumaa tarehe 11 April 2014 kutakuwa na Promo pati itakayofanyika katika Ukumbi wa Disco wa 84 Mjini Dodoma na Wasanii Lulu, Joti, Rich Rich, Monalisa na MC Pilipili watakuwepo ndani ya nyumba.

Mashindano haya yatakuwa ni muendelezo wa mshindano yaliyoanza kufanyika katika Kanda ya ziwa Mkoani Mwanza ambapo Washindi watatu kutoka Mkoani Mwanza wakiwakilisha Kanda ya Ziwa wakiwa wameshapatikana na kila mshindi aliweza kupewa zawadi ya shilingi laki tano kila mmoja na kusubiria kwenda Mkoani Dar Es Salaam kwaajili ya kuungana na washindi wengine Wa kanda zilizobaki kwaajili ya Fainali kubwa itakayofanyika mkoani Dar Es Salaam na mshindi katika Fainali hizo ataibuka na Kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania pamoja na Mikataba minono kutoka Kampuni ya Proin Promotions Limited na washindi kumi bora watakaopatikana katika Fainali hiyo watacheza filamu ya kwao na hatimaye itauzwa Nchini Nzima.

Katika Mashindano haya ya Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania yajulikanayo kama Tanzania Movie Talents yatajumuisha kanda ya Juu Kusini ambapo yatafanyika Mkoani Mbeya, Kanda ya Kaskazini ambapo usaili utafanyika Mkoani Arusha, Kanda ya Kati zoezi litafanyika Mkoani Dodoma, Kanda ya Kusini ambapoo usaili utafanyika Mkoani Mtwara, Kanda ya Pwani ambapo usaili utafanyika Mkoani Dar Es Salaam na hatimaye mashindano haya yakapewa upendeleo tena kufanyika Kanda ya Ziwa Mkoani Kigoma Kwa kuelewa kuwa Kigoma ni Mkoa ambao una wasanii wengi wa muziki wa bongo fleva na Proin Promotions Limited kutoa nafasi ya Upendelo kwa kuhisi pia wanaweza kupata Vipaji vya uigizaji Tanzania katika Mkoa Huo. Mshindi katika Fainali ya mwisho ataibuka na Shilingi Milioni 50 za kitanzania.

Katika Mashindano haya Fomu zitapatikana siku ya Usaili na hakuna gharama zozote zile zitakazotozwa kwaajili ya usaili na tunawaomba Wakazi wa Kanda ya kati kujitokeza kwa wingi Mkoani Dodoma siku ya usaili na kuweza kuonyesha vipaji vyao maana hii ndio fursa pekee ambayo watanzania wanaipata kutoka Kampuni ya Proin Promotions Limited na hatimaye kuweza kutimiza ndoto zao za kuwa waigizaji katika tasnia ya filamu nchini .

Shindano hili la Tanzania Movie Talents lina lengo la kusaka na kuibua Vipaji vya kuigiza na kukuza tasnia ya filamu nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...