Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 13, 2014

NMB YASAIDIA KITUO CHA WALIMU TEMEKEMeneja wa kanda ya Dar es salaam NMB, Bw. Salie Mlay akikabidhi kompyuta kwa Afisa elimu manispaa ya Temeke Bi. Honorina Mumba  kwa ajili ya kituo cha walimu wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Msaada huu wa kompyuta mbili pamoja na mashine ya kuchapisha karatasi (Printer) vimetolewa na benki ya NMB kwa ajili ya mafunzo yanayotolewa kwa walimu katika wilaya hii.Hafla ya makabidhiano ilifanyika juzi jijini Dar es salaam. Akishuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa kituo hicho cha walimu Temeke Bw.Daniel Matembele.
Meneja wa tawi la NMB Temeke Bw.Harold Lambileki akimkabidhi sehemu ya Kompyuta Mkuu wa kituo cha walimu Temeke Bw.Daniel Matembele. Msaada huu wa kompyuta mbili Pamoja na mashine ya kuchapisha karatasi (Printer) vimetolewa na benki ya NMB kwa ajili ya mafunzo yanayotolewa kwa walimu katika wilaya hii.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...